Nina muda mrefu kidogo nawasaidia wanawake na wanaume kuoana.Nawashauri mambo yafuatayo:
1.Usitafute mtakatifu, hayupo hutampata.
2.Punguzeni vigezo vya kuchagua umtakaye, dunia imebadilika
3.Chagua mwenye vigezo japo 2 vya sifa uzitakazo, mambo mengine mtabadilishana mkiwa kwenye ndoa
4.Msiogope kuchagua mchumba asiye wa dini yako au kabila yako, huyo ndio atakayekuwa mwandani wako
1. Watakatifu wapo. Hata kama ni Wawili Tanzania nzima. Lakini wapo. Dunia inawatu wa Aina zote.
Atafute mwenza anayefanana naye.
2. Huwezi punguza vigezo Kwa MTU unayetaka kufanya naye Maisha. Hasa vigezo vikuu vitakavyoifanya ndoa iwe na utulivu na Amani.
Labda vigezo vya kitoto. Lakini vigezo vikuu vya ndoa ni hivi;
a) Upendo
b) Uaminifu
c) Mvuto (Hii ni kulingana na vile MTU atazamapo, inahusu Uzuri na maumbile)
d) Uchumi
Lazima awe mchapakazi ili ipatikane Pesa ya kutunza familia na kutimiza mahitaji ya kila mwanafamilia.
e) Akili na Elimu.
Sio unachukua MTU hana lolote ajualo, hamuwezi kukaa na kujadili Jambo mkatoa kitu kizuri. Kitu kidogo mnagombana kama majinga.
f) Tabia NJEMA kulingana na Imani na tamaduni.
3. Mtu habadilishwi. Huwezi mbadilisha MTU ndani ya Ndoa.
Mtu anabadilika yeye mwenyewe. Unatafuta MTU asiye mlevi, tafuta. Sio utafute mlevi alafu utake abadilike asinywe Pombe. Huo ni ukosefu wa maarifa.
4. Ndoa inajengwa na Nguzo tatu, Akili(ubongo) Imani(Roho) na Upendo(Moyo)
Unaposema asitafute mtu wa Imani yake unakosea na hakuna ndoa ya hivyo. Ni suala la muda tuu hiyo Ndoa itafikia ukomo tuu.
Lazima MTU atafute mwenza wanaofanana hayo mambo Matatu hapo juu.