Kwa wanaotaka kujiua, soma hapa ujue namna ya kujizuia

Kwa wanaotaka kujiua, soma hapa ujue namna ya kujizuia

Midnight

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2021
Posts
229
Reaction score
681
Pumzika kwa amani ndugu Jonathan, member na mwanachama mkongwe wa JF.

Kwa wapenzi wa jukwaa la biashara kule kuna mtu mmoja najua mtamkosa sana, muhimu ni kutambua kuwa sisi ni mapito na duniani tunapita tu.

Nawasalimu kwa jina la jamuhuri. Kazi iendelee.

Naomba niende moja kwa moja kwenye lengo langu kuu la nyuzi hii.

Kwanza kabisa natanguliza pole na kuwatakia mema wanajumuiya wote wa jamii forums kwa kuwa natambua tunaguswa na nyakati zote za huzuni na furaha

Nikiwa kama mmoja wapo wa watu tuliopitia misukosuko mingi hata hollywood hawawezi kutoa movie ikaisha, leo napenda nizungumze na ndugu zetu wengi waliovunjika moyo na hata kutamani kujitoa uhai.

Kiukweli hivi karibuni niliguswa sana na habari kumuhusu ndugu yetu na mwanafamilia mwenzetu, Mkuu Mpauko.

Pumzika kwa amani ndugu. Ma-great thinker wengi wameguswa na hata kujiona wana hatia kabisa.

Niliona wakuu wakitafakari namna nzuri na bora ya kuwasaidia ndugu zetu wanaovunjika moyo na kutishia uhai wao na wa watu wao wa karibu, nami pia nikaona kupitia nyuzi hii tunaweza kuwapa moyo na kuwafanya wawe watu wapya.

Niliporejea kutoka nje ya nchi nilikozamia kwa miaka kadhaa, nilipokelewa na taarifa nyingi mbaya masikioni mwangu ( Bado huwa NASHINDWA kuzuia machozi kabisa kutoka machoni mwangu, sipendi kukumbuka mengi Ila nafanya hivi kwaajiri ya ndugu zangu nyie mnaofikia tamati ya kujitoa uhai)

Nataka msome huku mkijenga hisia na kuona maswahibu mazito kuliko mliyonayo ninyi!! Nataka mjipambanue na kuacha mkituacha tukijiona tuna hatia nanyi kwa kushindwa kuwapa moyo na mifano.

Nilikuta wazazi wamefariki, marafiki baadhi wa karibu kabisa wamakufa, msichana pekee niliyewahi kumpenda toka nizaliwe hadi hii leo hajatokea tena maishani mwangu, nae niliambiwa alitangulia mbele za haki muda mrefu. Usisikie kwa mtu, yakukute ndio utaelewa nini namaanisha.

Kama mnakumbuka kwenye ule Uzi wangu wa safari ya dhahabu Botswana, mwanzoni kabisa kuna sehemu nilisema nitaenda kulitafuta kabuli la huyo binti na kulia kwa sauti kubwaaa, kubwa sana namaanisha ijapokuwa sijui ni Tanga sehemu gani lakini nitatimiza ahadi YANGU.

Nilitamani kufa, nilitaka kujiua, nilifikiri na kujaribu kila baya unalolijua either nipunguze mawazo au ni log off kabisa duniani.

Na nakubali kabisa ya kuwa usimlaumu mtu anayefikiria kujitoa uhai, ukweli ni kwamba inafika wakati mahali unahisi na kuona kujiua ndio njia pekee ya kutuliza moyo wako na kupumzika kati ya mizigo mingi ya mateso ya ulimwengu na walimwengu wake.

Napenda kumnukuu hayati ndugu Mpauko, pale aliposema
"Kuna stage ikifika hata sense ya kupambana inakufa pia, huwezi kupambana halafu kila kitu kikawa kibaya kwako tu, hakuna jema kwako hakuna kabisa tangu uzaliwe kwa kweli sio vizuri kabisa"

Bila shaka hii ni kati ya kauli zake za mwisho mwisho kabisa hapa ndani.

Ndugu zangu wakati wewe ukiona una tatizo moja gumu kabisa, jipe moyo uku ukijua Mshana ana matatizo elfu moja magumu na sugu kwelikweli, Melo alipitia nyakati ngumu sana hapo nyuma na yote ni kwa ajili yetu lakini alipambana na kuushinda moyo dhaifu wa kushindwa, kuna watanzania mamilioni wanapitia hali ambazo hata kwenye ubaya zimepitiliza na bado wanaamini kuna nafasi ya ushindi

Kuna watu tumewakosea watu na wazazi ambao tunatamani waamke leo tuwaombe radhi lakini haiwezekani na bado tunaishi na kuazimia kutenda ipasavyo, kuvunjika moyo kila mtu anavunjika sio peke yako au matatizo na shida sio zako pekee.

Japo najua ni ngumu kuzuia jaribio au matamanio ya kujitoa uhai lakini jaribu kujipa muda, tafakali na ukiona hali hiyo inakusonga zaidi wajulishe watu wako wa karibu kwa msaada zaidi, na usijione mpweke sana au unachelewa kufa Bali tambua kuwa ukweli ni kwamba issue ya kutaka kujiua haipo kwako tu ni karibu watu wote inawatokea hivyo kutokana na maswala ya mahusiano, mifarakano, kukosa kazi, kukosa pesa na mengine mengiii hivyo kama na sisi tukiamua hivyo hatobaki mtu wa kukuzika wewe wala kukuokoa, muhimu ni kuacha yote na maisha kuendelea, naamini wewe ni shujaa, wewe ni imara, wewe ni simba.

"SHUJAA IMARA KAMA SIMBA"
 
Ubatili ni kama kumeza upepo, hakuna sababu ya kujitoa uhai narudia tena hakuna sababu ya kujitoa uhai, hayo ni majaribu tu na lazima kuna najia ya kuyashinda,wewe sio wa kwanza kupita katika hali kama hiyo wapo wengine waliopita wakashinda,zaidi ni kwamba ukivumilia kidogo tu mambo yatakuwa sasa, then kunasiku utakumbuka na kucheka sana kwanini nlitaka ku commit suicide.
 
Kabla haujaondoka Basi jitaidi wategemezi wako unawaachia mazingira mazuri mfano wazazi na watoto
Nikutakia kila la kheri kurudisha moyo nyuma
Mazingira mazuri una maanisha nini
 
The next is me sidhani kama huu mwezi utaisha,kwaherini wana jf
Kwa bahati mbaya sana maneno uumba, tunatengeneza uhalisia wa maisha yetu ya baadae kwa maneno yetu, matendo yetu, pia maneno ya wengine na matendo yao.
Mkuu mdukuzi wewe ni imara, usiamini katika kushindwa wala kukaribisha mawazo maovu ya kishetani moyoni mwako.
 
Kwa bahati mbaya sana maneno uumba, tunatengeneza uhalisia wa maisha yetu ya baadae kwa maneno yetu, matendo yetu, pia maneno ya wengine na matendo yao.
Mkuu mdukuzi wewe ni imara, usiamini katika kushindwa wala kukaribisha mawazo maovu ya kishetani moyoni mwako.
Nimejitahidi ila sasa nimesalim amri sioni namna ya kueouka hiki kikombe
 
Nimejitahidi ila sasa nimesalim amri sioni namna ya kueouka hiki kikombe
Mkuu Mdukuzi, binafsi nimewahi kuvunjika moyo kwa idadi isiyo na mfano hapa.
Hali unayopitia sasa ni kipimo kidogo sana mkuu, unaweza ukaniambia kuwa unatatizwa zaidi ya wale wagonjwa mahututi waliolala vitandani kwa miaka sasa?. Na bado wanatumaini. Mimi naamini kama upo hapa JF wewe ni wathamani sana maana mwana JF mmoja ni thamani kubwa kuliko watu 100 wasiojua hapa au kushindwa kuwa nasi hapa kwa changamoto, shida na matatizo mengi zaidi yako Mdukuzi, zaidi YANGU na pengine zaidi ya members wote wa JF, lakini bado wanatumaini la ushindi.
Niamini. Wewe ni jasiri, hodari na bingwa mtatua changamoto.
 
Back
Top Bottom