Kuna jamaa alikua anamuona mke wake yupo busy sana na group flani la WhatsApp. Limeandikwa "Wanawake Tu" sasa jamaa akawa anatamani sana kuona ndani wanadiscuss nini, so akachukua simu ya mke wake anakuta mke amefuta kila kitu. Duh.
Sasa kuna siku akachukua simu ya mke wake, akamtext Admin akamwambia hii namba ya shosti wangu naomba muunge, afu akafuta izo meseji baada ya kujibiwa. Jamaa akaungwa.
Aisee, aliyoyakuta mke wake anayaongea huko alichoka. Kuhusu michepuko, kuhusu yeye kutoperform vizuri, yaan alijuta.