Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Wakuu,
Kila mtu anapenda akitoka kwenda mahali fulani ajisikie salama na awe huru kutoka sehemu moja au nyingine bila bugudha yoyote.
Hii ni changamoto kidogo kwa wasichana/wanawake wanapotoka kwenda sehemu mbalimbali iwe ni kwaajili ya kutafuta riziki au mtoko wa sherehe, huku wakati wa usiku ukiwa changamoto zaidi.
Baadhi ya changamoto wanazokutana nazo ni kushikwashikwa/kutomaswa hovyo bila ridhaa yao, matusi, na hali ya usalama kwa ujumla ni mambo ambayo yanafanya wanawake wengi kuwa na uoga, kwa ujumla kero kubwa ni usumbufu unaoletwa na wanaume njiani.
Kuna sehemu ukienda inabidi mtu avae kigumu ili apunguze kero za kuzongwa zongwa, au ukitaka ujihisi salama kabisaaa unaongozana jamaa au rafiki yako wa kiume.
Tukirudi kwenye swali, wakati gani wewe dada/mama unajihisi salama zaidi na huru kutembea peke yako mtaani/kwenda kwenye shughuli zako?
Nini kikibadilika kitafanya ujihisi salama kutembea peke yako mtaani?
Wanaume mna maoni gani kwenye hili?