Kwa wanawake wote mliofunga PM

Duuh!!! Hivyo Baba Mchungaji kitufe cha kufunga PM kiliwekwa kwa ajili ya wanawake pekee?
Mama mchungaji, kwanza jiulize kwanini kitufe cha kufunga PM hakipo kwenye Jf Application..!!??
Hapa jibu ni kwamba, lazima uingie Jf kwa browser ndipo utafanikiwa kuifunga PM yako, na hii italazimika mtu aifanye ikiwa tu atakuwa amepata kero na usumbufu wa kutosha.

Na katika hali ya kawaida kati ya mwanamke na mwanaume, nani humuanza kumzoza mwengine..??
Kama ikiwa jibu ni mwanaume, basi mwanamke anayo haki ya kuifunga PM yake kwasababu yeye ndie muhanga mkubwa wa kuzozwa ambapo ikipita kiasi hubadilika na kuwa usumbufu.

Naomba kuwasilisha hoja mama mchungaji....
 
Mkuu, lakini mimi naamini kwamba hao wa kwenye daladala za posta-mwenge, mbagala, sinza, tabata na kadhalia.... ndio hawa hawa tunao pishana nao humu ndani kila kukicha.
Ni sawa lakini ukipishana nao mbagala,sinza,posta inakuwa unathaminisha moja kwa moja tofauti na humu unachizika na Avatar kumbe kihalisia ni Polygon au Morijo.
 
Kwanza Baba Mchungaji niseme tu mi si mpenzi wa kutumia hiyo Application na ndio nasikia leo kwamba huko hamna kitufe cha kufunga PM.

Hivyo Baba mchungaji unataka kuniaminisha kwamba sababu ya kufunga Pm ni kukwepa kero na usumbufu eee? 🀣🀣🀣

Lakini usisahau kuna wale wanaoogopa wasiojulikana hivyo wanaona kufunga PM ndio salama yao Baba mchungaji. Yaani majukwaani wanamwaga sumu zao weee juu ya gavamenti wakitegemea hakuna wa kuwapata kwa njia ambayo itahusisha mawasiliano ya faragha ambayo mwisho wa siku yanaeza kuwa ushawishi wa wao kupatikana.
 
Mama mchungaji, naomba usinichonganishe na ndugu wasomaji maana leo nimefunga kwaajili ya kufanya maombi kwa wote walio funga PM zao
Hahahaaa. Nilivyoona ndugu yangu kaitikia "Oooh" basi nikajua limempata dongo lako Baba Mchungaji.

Kila la kheri Baba Mchungaji huenda yakapokelewa woote wakawacha hiyo tabia.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwa hiyo tunao kuwa nashida tofaut na mitongozo tufanyeje watufungulie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…