JOKA55
Senior Member
- Nov 1, 2014
- 110
- 74
Nina rafiki yangu ni msomi wa Falisafa, anasimulia kuwa kipindi anasoma masomo hayo pasua kichwa pale Morogoro, siku moja muhadhiri aliingia darasani na mishumaa akaiwasha na akawaambia wanafunzi "jamani tuko katika maombolezo Mungu wenu mnayemuabudu amekufa" kila mtu alishtuka na walikaa mkao wa kula kujua kulikoni?
Kumbe huyu mwalimu ndo alikua anaanza mada ya Western Contemporary Philosophy ambapo moja ya magwiji wa zama hizo ni mjerumani maarufu Fridrich Nietzsche (1844 - 1900) ambaye kwa kipindi hicho aliibuka na nadharia ya Mungu amekufa na akaijengea hoja nadharia hiyo. Katika vitabu vyake maarufu kama Thus Spoke Zarathustra, Master–slave morality, Will to power na vingine vingi anajenga hoja kuwa binadamu wote wanazaliwa HURU hizi sheria ni dunia tu inakuja kuziweka ambazo kimsingi zinaubana ule uhuru wa kweli kila binadamu. Hapo ndipo akazishutumu dini kwa masharti makali na vitisho kwamba mbinguni ipo kama zawadi kwa wale wanaofanikiwa kutenda mema hapa duniani. Yeye anapingana na hili kuwa kazi ya Mungu isiingiliwe na binadamu ambaye anajiwekea masharti magumu kumfikia huyo Mungu. Mfano dhuluma zilizopo duniani kwa nini Mungu haingilii kati?
ktika hoja yake ya uhuru wa kujitawala katika kila nafsi bila ya kuingiliwa na mtu mwingine anaijenga katika kitabu chake cha 'Will to power' hapo anasema ikifikia haki inatendeka duniani kwa msukumo wa kila mtu mwenyewe bila kulazimishwa na sheria ndipo jamii inawaza kuwajenga watu aliowaita "SUPER MAN" kiumbe ambaye anatenda haki kutoka moyoni, kiumbe ambaye hawezi kuwa na ziada (kitu asichokitumia) kiumbe ambaye maendeleo ya jamii nzima ni kazi yake ya msingi, kiumbe ambaye anaipenda nchi yake, kiumbe ambaye hata akienda dukani ukamzidishia chenchi anakurudishia na kukuambia 'umenizidishia'.
Hapa hoja yake inasimama kuwa kila binadamu anazaliwa sawan mwingine bila hata nguo na mali zote baada ya kuzaliwa ni mali ya jamii, jamii ndio yenye utatajiri. Sasa ukumuana mtu anasufika kwa hela nyingi lazima amedhulumu baadhi ya wanajamii, mali ya jamii ameifanya kuwa yake.
Baadishi ya mjerumani huyu japo yalikua yanapingana na imani za dini yalikua na mchango mkubwa sana ktk maendeleo ya nchi hiyo. Inasemekana vita ya kwanza na ya pili ya dunia kila mwanajeshi mjerumani alipata kopi ya kazi za huyu bwana na kuamishwa kuwa Mungu amekufa na Mungu aliyebaki ni taifa lake, iliwapo mori kuipigania nchi yao ambayo ndio Mungu.
Kwa karene zetu hizi hatupaswi kujenga hizo hoja za Mungu amekufa ila tunapaswa tujenge hoja za kizalendo za kitaifa, tujenge Ma-super men wa kitaifa wenye uzalendo, wenye uchungu na nchi yao (Tanzania) ambao watapasua vichwa kwa ajili ya manufaa ya watanzania hasa kipindi hiki tunavyoelekea uchaguzi mkuu. Tumpate raisi mkweli asiyependa rushwa, mwenye huruma na watanzania, mweye huruma na afya za watanzania wenzake.
Bahati mbaya zipo taarifa kuwa wengi wa wanaccm waliotia nia WAMETUMWA na mataifa mengine kwa manufaa ya mataifa hayo. Kwa vile wametuona sisi ni vichwa maji, kati ya waliochukua fomu kuna watu waliowekwa na:
-CIA
-Chama cha Labor cha Uingereza
-Wafanyabiashara wakubwa wa Uarabuni
-Makaburu
-China
-Umoja wa Ulaya
-India
- Pakstani
-Ujerumani
-Israel
Hii yote ni kutaka kugawana rasilimali zetu. Tujiulize chama kimoja wagombea wote hao wa nini. Wapo wanaoahidi mambo kibao ilhali karibu maisha yao yote walikua watumishi wa serikali hiyo walikua wapi kuyafanya hayo wanayoyaahidi?
Wapo wezi, wauaji, wadini, wakabila nk lakini bado tunawashabikia! Jamani tuweni wazalendo? Naamini wapo watanzania wazuri. Tuwasupport wawe chama tawala au upinzani