Kamweneeee!
Awali niwape Pole kwa mihangaiko ya kila siku katika harakati za kujitafutia mkate wetu wa kila siku. Pili, kama uzi huu umewahi kuwepo hapa basi nitaomba Mods muufunge huu wangu haraka sana, Vinginevyo twende kwenye Mada mezani.
Uangaliaji wa Filamu za Katuni umekua ni kitu kinachotupotezea mawazo na muda na kuleta burudani kwa sisi watazamaji. Binafsi nimekua na mapenzi na Katuni tangu zama za ITV na Chanel 10 kidogo kwa maana katuni zao hazikua nzuri sana kama ITV DAIMA katika kipindi cha watoto na mtangazaji Eddy ambacho kilikua kikionesha katuni mbalimbali zenye kufurahisha na kuleta burudani si kwa watoto tu bali hata kwa watu wazima baadhi. Katuni hizo kwa uchache ni kama zifuatazo;
- Popeye and Son (Spinach sandwich)
- Double Dragons (the twins Jimmy and Billy against Shadow and his warriors)
- Sonet/Sonic
- Scooby Doo
- Flintstones (Yabba dabba dooo)
- Tom&Jerry
- The Simpsons
- Looney Tunes
- Batman
Tukija katika Filamu( movies) mpaka kufikia sasa nimebahatika kuzitazama zifuatazo;
nataraji kuzitazama hizi siku za baadae
THE LION KING
FROZEN
ALADIN
MULAN NK...
Ongeza za kwako uzipendazo na zilizokukamata haswa