Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Queen Seon Deok ni nzuri zaidi hata ya 6 flying dragon
 
Ndo naambiwa hapa
Bora sikuifuta

Yani nataman mtiririko wa visa vya wafalme cha baada ya hii six dragon

Nasikia bang won alikuja kuua ndugu zake baada ya kupata u king
Hii drama natamani niimalizie ila nahisi nitaanza kuumia upya na Yoo ah in jamani [emoji24][emoji24][emoji24]
 
talnam
Picha: General Yi Songgye Vs General Choi Young

Kuna hii kazi inaitwa Jeong do Jeon,. Ni drama ambayo infanana na hiyo six flying dragon zote zinaelezea jinsi Joseon ilianzishwa. Six flying dragon imeandaliwa na SBS na ilitoka mwaka 2015. Wakati Jeong Do Jeon ilitoka mwaka 2014 na imeandaliwa na KBS.
JEONG DO JEON
Hiii drama inamuelezea zaidi Jeong do Jeon a.k.a Sambong ambaye ni moja ya wasomi wakubwa katika historia ya Korea, pia alikuwa Neo Confuciunist Philosopher, waziri mkuu wa kwanza wa Joseon. Pia Lee Songgye( King Taejo) mfalme wa kwanza wa Joseon. Naweza kusema kwenye hii drama General Choi Young uhusika wake umeoneshwa zaidi kuliko hata Yi Bang Won.
Kwa sababu hao watubwa 3 ndio walikuwa na funguo za Goryeo ibaki na iangushwe. Ingawa hatuwezi kumbeza Yi Bang Won( King Taejong) mfalme wa 3 wa Joseon, kwa maana yeye ndiye aliyetuma wapambe wakamuue Joeng Mong Ju a.k.a Peoun ambaye alionekana kama kikwazo kwq mapinduzi ambayo Sambong pamoja na Lee Songgye( King Taejo) alikuwa ameyapanga.
Joeng Mong Ju ( Peoun) Huyu ni moja ya wasomi wakubwa kwenye hisoria ya Korea na alikuwa ndiye Waziri mkuu wa mwisho wa Koryeo. licha ya kuwa alikuwa mpinzani mkubwa wa Joeng Do Jeon ( Sambong) hawa walikuwa ni marafiki wakubwa toka utotoni mwao na ndoto yao ilikuwa ni kuleta mapinduzi kwenye Taifa lao lilikuwa linanuka rushwa na ufisadi. Kwahiyo Peoun na Sambong hawa wamesoma shule moja na wote walikuwa ni Confuciunist Philosophers. Baada ya mtihani wa Taifa Peoun aliongoza kisha Sambong akishika nafasi ya 3. Uadui wao wakisiasa ulikuja pale ambapo wawili hao walitofautiana kiitikadi kwa maana


SAMBONG aliamini kuwa Goryeo ilipofika haiwezi kurudishwa nyuma Kwahiyo inapswa kuzamishwa kisha ianzishwe Dynasty nyingine ambayo itakuwa na mifumo bora ya utoaji huduma kwa watu na kiutawala mpaka sera za kijeshi mpya.

PEOUN aliamini kuwa kubadilisha Taifa jina sio suluu kwa matatizo yaliyopo kwenye Nchi yao bali wale viongozi wabadhilifu ambao wanafanya maisha ya watu kua magumu wachukuliwe hatua kaili za kuajibishwaji.

Kwahiyo pamoja na tofauti zao bado Sambong pamoja na Lee Songgye walikuwa bado wanamuheshimu sana Peoun kwa maana ndiye aliyekuwa kiongozi( Waziri)mwadilifu kupita hata Nyumba ya kifalme( Ukoo wa Wang) pia kiongozi mkuu wa Majeshi Choi Young alikuwa na heshima kubwa sana kwa wadilifu wake.
Tofauti ya Jeong Do Jeon (Sambong) na Lee Bang Won ilianzia hapo baada ya Yi Bang Won kumuua Joeng Mong Ju ( Peoun) baada ya hili tukio Sambong alimkataa kabisa Lee Bang Won ingawa mwanzoni Sambong alionekana kumpenda Bang Won sababu ndiye alikuwa brightest kati ya watoto wote wa Yi Songgye. Hata Yi Songgye alimkataa Bang Won baada ya Jambo hili la kumuua Peoun ambaye alionekana mwiba mkali kwa kina Lee Songgye na Sambong Ingawa tukio hili liliwapoa kina Sambong kufanya mapinduzi so Sambong akamwbia Chukua jEshi ukakamilishe kazi mie huku kwenye siasa tayari.
kifupi moja kati ya sababu ya Sambong kuuliwa na Lee Bang Won ilianziapo baada ya Sambong kumkataa na ikumbukwe Lee Songgye alikuwa anamsikiliza sana Sambong hata katika utawala wake mambo mengi alikuwa anapanga Sambong. Sambong hakutaka yaliyotokea Goryeo yajirudie tena Joseon hivyo alitaka kuanzisha mfumo wa Constitutional Monarch ambapo Waziri mkuu ndiye kiongozi wa mambo ya serikali na atachaguliwa na watu, hivyo familia ya kifalme kwakua wao wanarithi madaraka hivyo watakuwa tu kama Wakuu wa Nchi. Yi Songgye ( King Taejo) hakuwa na shida alikubali, baada ya Lee bang won kusikia hayo akafanya njama akamuua Sambong kisha Akachukua Nchi maana aliona kama mzee wake kila kitu anachoambiwa na Sambong anafuata na aliona kama Sambong anaidhalilisha nyumba ya kifalme. Kifupi Lee Bang Won alikuwa ni moja ya Viongozi bora wa Joseon licha ya kuwa aliichukua Nchi kwa njia mbaya na aliongoza kwa sheria kali mno. Pia Lee Bang Won alikuwa akiwapenda watu wa Joseon ingawa alikuwa akijuta sana kwa namna ambavyo alimwaga damu za watu ndio maana drama nyingi zina muhusisha na neno 'TEARS'

Hii drama utajifunza siasa, Falsafa pia vita zimo. pia imejikita zaidi katika historia kama unataka kuelewa kwa undani jinsi Joseon ilivyoanzishwa hii ndio first recommendation then ufanye revision na Six flying dragon.


SIX FLYING DRAGON
Hii drama imejikita zaidi kuelezea maisha ya Yi Bang Won jinsi alivyopambana na Sambong mpaka Joseon ikaanzishwa, cha kushangaza humu ndani Lee Songgye hakupewa attention kubwa kiiivyo.
Kwenye hii drama ya six flying dragon kuna baadhi ya washiriki katika historia hawapo au visa katika historia havipo ila directors walijiongeza hivyo ilikuleta utofauti na ile drama ya Jeong do Jeon.
Ndani ya Six flying dragon utajifunza Siasa, Falsafa pia utaenjoy Action humu ndani, kuna mdada anaitwa sijui Chuksangwa anagawa dozi huyo!!!..

Kifupi drama zote ni nzuri, na kila moja inaupekee wake. Na zote ni fupi tu zina episode 50 kwa 50
NOTE: SAMBONG anahesabika kama msomi wa Joseon na msaliti wa Koryeo while PEOUN anahesabika kama msomi wa Goryeo na mwaminifu wa Goryeo

General Choi Young anahesabika kama Shujaa wa Goryeo wakati Lee Songgye anahesabika kama shujaa wa Joseon.

Recommendation
Drama yenye Story mwendelezo wa hizo mbili ni
THE GREAT KING SEJONG inamuelezea mtoto wa Lee Bang Won aitwaye Lee Do au Yi Do( Sejong the Great), ingawa Tree with Deep root nayo inaelezea japo nayo wamejiongeza director, Jang young sil pia
zote hizo zinamgusa Sejong na utawala wake.

Hawa ndio Wafalme 5 bora wa Joseon
1. Sejong the Great( mtoto wa Yi Bang Won)
2. Jeong Jo( mtoto wa Prince Sado na Mjukuu wa Yeong Jo)
3. Yeong Jo( mtoto wa Dong yi na Sukjong)
4. Taejong ( Lee Bang Won)
5.... utajaza hapa.

TAHADHALI: Chunga ulevi wa Historical drama usije ukakuathiri bure.

Alamsiki.
 

[mention]Gwanggaeto the Great [/mention] Shukrani Sana nimepata Mwanga, historia yao inavutia na hizo recom nitazifanyia kazi

Yani sijui ni waigizaji au ni namna historia ilivyo unajikuta unashabikia mapinduzi.

Na hii nyimbo yao wakati Lee bang ji anaiimba nikajikuta roho inauma kabisa.

King sejong, dah bang won alimuua sambong[emoji17]
 
Hahah sijui kama utakuwa na moyo ilau ukitaka kumjua Sejong the Great vizuri itabidi uitazame hiyo drama iliyoandaliwa kwa jina lake. Naweza kusema humo ndani kumejaa siasa si mchezo, technology pia utajifunza. Kama sikosei ina episodes 64 au 84. Najua unaweza kuwa haujawahi kuona drama ndefu kwa namna hii. Okay ukishindwa basi itafute Jang young sil hii imefupisha mambo na imefocus zaidi kwa Jang young sil. Cha kuvitia ni kua kaicheza Song il Kook, pia wale walovaa uhusika wa Taejong( Yi Bang Won) na Sejong the Great( Yi Do) kwenye drama ya The Great King Sejong ndio hao hao wamevaa uhusika huo tena kwenye Jang young sil. Hii ina episodes 24 tu.

Picha: Princess' Man

Story mwendelezo baada ya Sejong ni drama iitwayo Princess' Man nadhni episode 24. Na Grand Prince. Drama zote mbili zinazungumzia maisha baada ya Utawala wa Sejong the Great

Picha: Grand Prince
 
Yani sijui ni waigizaji au ni namna historia ilivyo unajikuta unashabikia mapinduzi.
Hali ya Goryeo ilikuwa ni mbovu, ufisadi na Rushwa vilikithiri na watu walitaabika sana. Ukifuatilia drama ya Jeong do Jeon imeinesha kwa jinsi gani Goryeo ilikuwa imeoza. So ilikuwa ni Lazimq kushabikia mapinduzi ya Kina Sambong.
By the way Alovaa uhusika wa Sambong kwenye Six flying dragon nampa big up alitishq, pia alovaa uhusika wa Sambong kwenye Jeong do Jeon, wow! Alitisha sana. Hakuna aloharibu.
 
Nimempenda sana huyu yoo ah in
Kwa huu uchezaji, labda wanaweza kuichukulia kesi yake kama victim

Kwenye chicago typewriter sikumuelewa ila nitairudia tu.
Mmh sidhani. Wakorea wana nongwa sana...Kuna video nilimuona ndio katoka kuhojiwa si wakaanza kumrushia mayai hadi chozi lilinitoka[emoji24]
 

Shukran sana
Sijategemea kipindi hichi nita concentrate na historical hii tu, uhusika wao umevalika haswaa.
 
Mmh sidhani. Wakorea wana nongwa sana...Kuna video nilimuona ndio katoka kuhojiwa si wakaanza kumrushia mayai hadi chozi lilinitoka[emoji24]

Ikifika hapo wakorea nawachukia
Kwani alikua anauza?
Maana yake si alikua anaanza uteja kwanin wamlaum
Ah korea panaboa namna wanaeza mdrag mtu hata wasimpe nafasi ya kujifunza.

Nimekerekwa
 
Ikifika hapo wakorea nawachukia
Kwani alikua anauza?
Maana yake si alikua anaanza uteja kwanin wamlaum
Ah korea panaboa namna wanaeza mdrag mtu hata wasimpe nafasi ya kujifunza.

Nimekerekwa
Ni wapuuzi wale watu sijui wanajisikiaje kuwanyanyasa mastaa wao
 
Jang hyun:
smart kichwani and a very skilled warrior mwenye upendo dhidi ya watu wake wa karibu (marafiki) pamoja na wananchi wa tabaka la chini. Wapi anatokea bado haijulikani but nina wasiwasi kwa kuangalia haiba na muonekano wake wa kimavazi, tafakuri na hata nguvu yake ya utoaji msaada kwa wahitaji na connection alionayo huenda anatokea katika familia za tabaka la juu.

je? anatokea familia ya kifalme au kizazi chake kiliwahi kuwa na uhusiano wa karibu na royal families?
kama ni hivyo bila ya shaka huenda atakuwa ni miongoni mwa wahanga wa mapinduzi yaliofanywa ya kumuondoa mfalme Gwanghae yalioongozwa na different political factions waliokasirishwa na utawala wa Gwanghae.
nguvu ya theory hii inatiwa nguvu na kitendo cha Lee jang Hyun kumchukia sana mfalme Injo, huyu bwana Injo ndiye aliyewekwa madarakani baada ya kuondolewa kwa Gwanghae. Lee jang hyun hakuwa tayari kumwaga hata tone la nguvu na jasho lake kwa ajili ya kumpigania mfalme Injo dhidi ya uvamizi wa Taifa la QING.

Hopefully tutajifunza historia yake kwenye sehemu hii ya kwanza iliobakisha episode 4 kumalizika.

My Dearest drama
 
episode 5
nimependezwa na jang hyun kumsifia Gil chae kwa kutumia kisu alichomkabidhi kwa ajili ya kujilinda dhidi ya wavamizi, anafahamu fika ya kwamba yeye (gil chae) si mwanamke shujaa ila ni resilient pindi anapopatwa na majaribu.

hakutaka tambo wala kurusha samahani za kijinga kwa binti,
maybe aliona samahani za kijinga kwa jambo lililokwisha pita ni useless
baadhi ya nyakati samahani za kijinga humfanya mpokea msamaha ajihisi yeye si lolote bila ya msaada wa mtu mwengine iwe rafiki, mzee au hata mpenzi.
misamaha ya kijinga kutoka kwa mwanamme humfanya msichana awe damsel in distress muda wote.

ohh binti samahani kwa kukuacha katika hatari
ohh samahani kwa kuchelewa kuja kukuchukua
ohh samahani kwa kushindwa kukutumia fedha ya salon
blah blah

"nimefurahishwa nawe kwa kitendo chako cha kumkamata yule panya, niliwahi kukwambia wewe ni shujaa zaidi ya wabunge wetu waliopo bungeni"

hata kama panya wenyewe ni mjukuu wa panya maguire...
msifie bwanaaa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…