adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 12,207
- 26,521
Naitafuta sana siku nikitokea sehemu ya Wi-Fi nitaanza na hiyo.Weweee uliachaje The great queen? Ni nzuri sana bwana hebu irudie hutojuta kabisa [emoji16]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naitafuta sana siku nikitokea sehemu ya Wi-Fi nitaanza na hiyo.Weweee uliachaje The great queen? Ni nzuri sana bwana hebu irudie hutojuta kabisa [emoji16]
Nilifanikiwa kuona kidogo tu zamani sana na sikuanzia mwanzo na nikatoka kuilewa ujasusi na mipango iliyopo mule.Queen Seon Deok ni nzuri zaidi hata ya 6 flying dragon
Kwenye Jang Yeong Sill (pichani kwenye avatar yangu) uasi ulitaka kuibuka Loyalist wa Gugreyo walitaka kufanya mapinduzi .Nilianza na hiyo kwanza na kwa mara ya kwanza nikakuta Joseon sikujua historia ya Joseon jinsi ilivyoanzishwa mpaka nilivyooona Six flying dragon nikaunganisha dots na kuelewa mchongo mzima.talnam
Picha: General Yi Songgye Vs General Choi Young
View attachment 2725445
Kuna hii kazi inaitwa Jeong do Jeon,. Ni drama ambayo infanana na hiyo six flying dragon zote zinaelezea jinsi Joseon ilianzishwa. Six flying dragon imeandaliwa na SBS na ilitoka mwaka 2015. Wakati Jeong Do Jeon ilitoka mwaka 2014 na imeandaliwa na KBS.
JEONG DO JEON
Hiii drama inamuelezea zaidi Jeong do Jeon a.k.a Sambong ambaye ni moja ya wasomi wakubwa katika historia ya Korea, pia alikuwa Neo Confuciunist Philosopher, waziri mkuu wa kwanza wa Joseon. Pia Lee Songgye( King Taejo) mfalme wa kwanza wa Joseon. Naweza kusema kwenye hii drama General Choi Young uhusika wake umeoneshwa zaidi kuliko hata Yi Bang Won.
Kwa sababu hao watubwa 3 ndio walikuwa na funguo za Goryeo ibaki na iangushwe. Ingawa hatuwezi kumbeza Yi Bang Won( King Taejong) mfalme wa 3 wa Joseon, kwa maana yeye ndiye aliyetuma wapambe wakamuue Joeng Mong Ju a.k.a Peoun ambaye alionekana kama kikwazo kwq mapinduzi ambayo Sambong pamoja na Lee Songgye( King Taejo) alikuwa ameyapanga.
Joeng Mong Ju ( Peoun) Huyu ni moja ya wasomi wakubwa kwenye hisoria ya Korea na alikuwa ndiye Waziri mkuu wa mwisho wa Koryeo. licha ya kuwa alikuwa mpinzani mkubwa wa Joeng Do Jeon ( Sambong) hawa walikuwa ni marafiki wakubwa toka utotoni mwao na ndoto yao ilikuwa ni kuleta mapinduzi kwenye Taifa lao lilikuwa linanuka rushwa na ufisadi. Kwahiyo Peoun na Sambong hawa wamesoma shule moja na wote walikuwa ni Confuciunist Philosophers. Baada ya mtihani wa Taifa Peoun aliongoza kisha Sambong akishika nafasi ya 3. Uadui wao wakisiasa ulikuja pale ambapo wawili hao walitofautiana kiitikadi kwa maana
View attachment 2725733
SAMBONG aliamini kuwa Goryeo ilipofika haiwezi kurudishwa nyuma Kwahiyo inapswa kuzamishwa kisha ianzishwe Dynasty nyingine ambayo itakuwa na mifumo bora ya utoaji huduma kwa watu na kiutawala mpaka sera za kijeshi mpya.
PEOUN aliamini kuwa kubadilisha Taifa jina sio suluu kwa matatizo yaliyopo kwenye Nchi yao bali wale viongozi wabadhilifu ambao wanafanya maisha ya watu kua magumu wachukuliwe hatua kaili za kuajibishwaji.
Kwahiyo pamoja na tofauti zao bado Sambong pamoja na Lee Songgye walikuwa bado wanamuheshimu sana Peoun kwa maana ndiye aliyekuwa kiongozi( Waziri)mwadilifu kupita hata Nyumba ya kifalme( Ukoo wa Wang) pia kiongozi mkuu wa Majeshi Choi Young alikuwa na heshima kubwa sana kwa wadilifu wake.
Tofauti ya Jeong Do Jeon (Sambong) na Lee Bang Won ilianzia hapo baada ya Yi Bang Won kumuua Joeng Mong Ju ( Peoun) baada ya hili tukio Sambong alimkataa kabisa Lee Bang Won ingawa mwanzoni Sambong alionekana kumpenda Bang Won sababu ndiye alikuwa brightest kati ya watoto wote wa Yi Songgye. Hata Yi Songgye alimkataa Bang Won baada ya Jambo hili la kumuua Peoun ambaye alionekana mwiba mkali kwa kina Lee Songgye na Sambong Ingawa tukio hili liliwapoa kina Sambong kufanya mapinduzi so Sambong akamwbia Chukua jEshi ukakamilishe kazi mie huku kwenye siasa tayari.
kifupi moja kati ya sababu ya Sambong kuuliwa na Lee Bang Won ilianziapo baada ya Sambong kumkataa na ikumbukwe Lee Songgye alikuwa anamsikiliza sana Sambong hata katika utawala wake mambo mengi alikuwa anapanga Sambong. Sambong hakutaka yaliyotokea Goryeo yajirudie tena Joseon hivyo alitaka kuanzisha mfumo wa Constitutional Monarch ambapo Waziri mkuu ndiye kiongozi wa mambo ya serikali na atachaguliwa na watu, hivyo familia ya kifalme kwakua wao wanarithi madaraka hivyo watakuwa tu kama Wakuu wa Nchi. Yi Songgye ( King Taejo) hakuwa na shida alikubali, baada ya Lee bang won kusikia hayo akafanya njama akamuua Sambong kisha Akachukua Nchi maana aliona kama mzee wake kila kitu anachoambiwa na Sambong anafuata na aliona kama Sambong anaidhalilisha nyumba ya kifalme. Kifupi Lee Bang Won alikuwa ni moja ya Viongozi bora wa Joseon licha ya kuwa aliichukua Nchi kwa njia mbaya na aliongoza kwa sheria kali mno. Pia Lee Bang Won alikuwa akiwapenda watu wa Joseon ingawa alikuwa akijuta sana kwa namna ambavyo alimwaga damu za watu ndio maana drama nyingi zina muhusisha na neno 'TEARS'
Hii drama utajifunza siasa, Falsafa pia vita zimo. pia imejikita zaidi katika historia kama unataka kuelewa kwa undani jinsi Joseon ilivyoanzishwa hii ndio first recommendation then ufanye revision na Six flying dragon.
View attachment 2725732
SIX FLYING DRAGON
Hii drama imejikita zaidi kuelezea maisha ya Yi Bang Won jinsi alivyopambana na Sambong mpaka Joseon ikaanzishwa, cha kushangaza humu ndani Lee Songgye hakupewa attention kubwa kiiivyo.
Kwenye hii drama ya six flying dragon kuna baadhi ya washiriki katika historia hawapo au visa katika historia havipo ila directors walijiongeza hivyo ilikuleta utofauti na ile drama ya Jeong do Jeon.
Ndani ya Six flying dragon utajifunza Siasa, Falsafa pia utaenjoy Action humu ndani, kuna mdada anaitwa sijui Chuksangwa anagawa dozi huyo!!!..
Kifupi drama zote ni nzuri, na kila moja inaupekee wake. Na zote ni fupi tu zina episode 50 kwa 50
NOTE: SAMBONG anahesabika kama msomi wa Joseon na msaliti wa Koryeo while PEOUN anahesabika kama msomi wa Goryeo na mwaminifu wa Goryeo
General Choi Young anahesabika kama Shujaa wa Goryeo wakati Lee Songgye anahesabika kama shujaa wa Joseon.
Recommendation
Drama yenye Story mwendelezo wa hizo mbili ni
THE GREAT KING SEJONG inamuelezea mtoto wa Lee Bang Won aitwaye Lee Do au Yi Do( Sejong the Great), ingawa Tree with Deep root nayo inaelezea japo nayo wamejiongeza director, Jang young sil pia
zote hizo zinamgusa Sejong na utawala wake.
Hawa ndio Wafalme 5 bora wa Joseon
1. Sejong the Great( mtoto wa Yi Bang Won)
2. Jeong Jo( mtoto wa Prince Sado na Mjukuu wa Yeong Jo)
3. Yeong Jo( mtoto wa Dong yi na Sukjong)
4. Taejong ( Lee Bang Won)
5.... utajaza hapa.
TAHADHALI: Chunga ulevi wa Historical drama usije ukakuathiri bure.
Alamsiki.
Nimeona Jang yeong sill na Six flying dragon mpaka namaliza sijawahi kugundua kama Lee Bang Won yupo mule.Hahah sijui kama utakuwa na moyo ilau ukitaka kumjua Sejong the Great vizuri itabidi uitazame hiyo drama iliyoandaliwa kwa jina lake. Naweza kusema humo ndani kumejaa siasa si mchezo, technology pia utajifunza. Kama sikosei ina episodes 64 au 84. Najua unaweza kuwa haujawahi kuona drama ndefu kwa namna hii. Okay ukishindwa basi itafute Jang young sil hii imefupisha mambo na imefocus zaidi kwa Jang young sil. Cha kuvitia ni kua kaicheza Song il Kook, pia wale walovaa uhusika wa Taejong( Yi Bang Won) na Sejong the Great( Yi Do) kwenye drama ya The Great King Sejong ndio hao hao wamevaa uhusika huo tena kwenye Jang young sil. Hii ina episodes 24 tu.
View attachment 2726191
Picha: Princess' Man
Story mwendelezo baada ya Sejong ni drama iitwayo Princess' Man nadhni episode 24. Na Grand Prince. Drama zote mbili zinazungumzia maisha baada ya Utawala wa Sejong the Great
View attachment 2726194
Picha: Grand Prince
Aliyavaa uhusika wa Sambong kwenye Six flying dragon kipindi yuko kijana na watoto mapangoni sura yake inakuja kama Young Pobrother wake Daeso wa kwenye Jumong.Hali ya Goryeo ilikuwa ni mbovu, ufisadi na Rushwa vilikithiri na watu walitaabika sana. Ukifuatilia drama ya Jeong do Jeon imeinesha kwa jinsi gani Goryeo ilikuwa imeoza. So ilikuwa ni Lazimq kushabikia mapinduzi ya Kina Sambong.
By the way Alovaa uhusika wa Sambong kwenye Six flying dragon nampa big up alitishq, pia alovaa uhusika wa Sambong kwenye Jeong do Jeon, wow! Alitisha sana. Hakuna aloharibu.
Pia nimeipenda sana yule dogo aliyevaa uhusika wa Lee Bang Won akiwa utotoni ile ongea yake na usiriaz latisha sana mule.Hali ya Goryeo ilikuwa ni mbovu, ufisadi na Rushwa vilikithiri na watu walitaabika sana. Ukifuatilia drama ya Jeong do Jeon imeinesha kwa jinsi gani Goryeo ilikuwa imeoza. So ilikuwa ni Lazimq kushabikia mapinduzi ya Kina Sambong.
By the way Alovaa uhusika wa Sambong kwenye Six flying dragon nampa big up alitishq, pia alovaa uhusika wa Sambong kwenye Jeong do Jeon, wow! Alitisha sana. Hakuna aloharibu.
Hivi hakuna series inayoonesha majuto ya baadhi ya makosa ya wakorea waliyoyafanya zamani?Kwenye Jang Yeong Sill (pichani kwenye avatar yangu) uasi ulitaka kuibuka Loyalist wa Gugreyo walitaka kufanya mapinduzi .Nilianza na hiyo kwanza na kwa mara ya kwanza nikakuta Joseon sikujua historia ya Joseon jinsi ilivyoanzishwa mpaka nilivyooona Six flying dragon nikaunganisha dots na kuelewa mchongo mzima.
Karibu kundini mkuu. Kwa kuanzia hizi zitakufaaMie mgeni wa korean drama biambie series kalii za romance na action za kikorea ili nienjoy
Hongera sana, mie Jumong ndio ilinifungulia Safari ya Wakorea, mwaka 2008 enzi hizo ITV ila sikufanikiwa kuielewa maana kuna episode nilikuwa zinanipita maana enzi hIzo ikifika saa 3 unapelekwa kitandani n bakora, so nilikuwa naivizia marudio J. Mosi.Umenikumbusha Time between dog and wolf ni kati kdrama za mwanzomwanzo kabisa kuzitama naweza kusema ndio zilizoniingiza kwenye ulevi. Yule mwenzie na Lee joon ki pamoja na kutazama drama zake nyingi jina lake nimeshindwa kulishika...🤣🤣
Kaanze na Bridal Mask, vyote utavikuta humo mapenzi na Action. Mkono unapigwa humo ndani balaa.Mie mgeni wa korean drama biambie series kalii za romance na action za kikorea ili nienjoy
Asante sanaKaanze na Bridal Mask, vyote utavikuta humo mapenzi na Action. Mkono unapigwa humo ndani balaa.
Asante kakaKaribu kundini mkuu. Kwa kuanzia hizi zitakufaa
Romance:
What is wrong with secretary Kim
Moon lovers: Scarlet heart ryeo
The world of the married
Descendants of the sun
Uncontrollably fond
Goblin
Action:
K2
Iris
Healer
Vagabond
Squid game
Six flying dragon
All of us are dead
The man called god
Warrior Baek Dong-soo
Pia nimeipenda sana yule dogo aliyevaa uhusika wa Lee Bang Won akiwa utotoni ile ongea yake na usiriaz latisha sana mule
Hii series niliangalia 2014 ndo series iliyonifanya nipende wakorea mpaka leo , nimeshailudia kuiangalia mara 3Kaanze na Bridal Mask, vyote utavikuta humo mapenzi na Action. Mkono unapigwa humo ndani balaa.
Giant,Kwa wale wanaopenda Thriller/ Action au drama za Kijasusi, ipi ni kali zaidi? Naomba unipe 5 zako za moto zaidi
1. Vagabond
2. Iris
3. A man Called God
4. Fugitive Plan B
5. 3 days
City hunter
The Veil
Healer
The K2
Golden cross
View attachment 2703441
Kaangalie my country huto jutia Mvaa KobaziHii series niliangalia 2014 ndo series iliyonifanya nipende wakorea mpaka leo , nimeshailudia kuiangalia mara 3
Hio ipo kwenye watchlist yangu sasa hivi naangalia bloodhound's. Vipi ni kali au nitapoteza bando langu?Kaangalie my country huto jutia Mvaa Kobazi
Wana jua mpaka wame pitiliza 🔥🔥Hio ipo kwenye watchlist yangu sasa hivi naangalia bloodhound's. Vipi ni kali au nitapoteza bando langu?
Nimeipakua leo. Episode ya Kwanza tu namuona Jang Hyuk bila shaka litakua dude kali jamaa hana kazi mbovu🔥Kaangalie my country huto jutia Mvaa Kobazi
Mzee Ina Anza mwishoni, halafu ndo Wana Anza kuleta pocha halisi.Nimeipakua leo. Episode ya Kwanza tu namuona Jang Hyuk bila shaka litakua dude kali jamaa hana kazi mbovu🔥