USISOME KAMA HUNA MIAKA 90 YA KUZALIWA
nimesoma sehemu fulani sijui kama ni kweli au ni kasumba za vibaraza vya kahawa.
" During the
Goryeo dynasty, same-sex sexual activity was not explicitly prohibited".
unaikumbuka movie ya
frozen flower, unajua yule mfalme baradhuli (kwetu tunamwita khanithi) alikuwa ni wa taifa la Goryeo japokuwa uhusika wake ni wa kidhahania, nafikiri ni rahisi kuzungumzia homosexuality kupitia utaifa wa Goryeo iliojengwa kwa imani ya kuvumiliana (buddhism) kuliko utaifa wa Joseon iliojengwa kwa misingi ya
neo Confucianism
chukua na hii:
rikodi tofauti za waandishi wale zinatuaminisha ya kwamba mfalme Mokjong (karne ya 10) ambaye ndiye huyo unayemuona ndani ya hiyo drama alikuwa anavutiwa zaidi na watumishi wa kiume kuliko watumishi wa kike na aliwafanya kama vile ni wapenzi wake (
wonchung ), si ajabu bwana muandishi wa hiyo drama akajaribu kutuonyesha upande huo.
mwengine aliitwa
Gongmin naye alitawala Goryeo kwenye karne ya 13, huyu bwana baada ya kumpoteza mke wake mpendwa
malikia Noguk kutoka Yuan Mongolia maisha yake ya dunia ni kama vile yalisimamishwa kutokana huzuni ndeefu iliotapakaa kwenye nafsi yake.... katika kutafuta kwake utulivu waandishi wale wanadai bwana huyo aliamua kujiweka karibu zaidi na vijana wa kiume aliowatumia kama walinzi wake na watumishi wake wa ndani zaidiii.
waandishi wakaenda mbali zaidi kwa kudai ya kwamba hata mtoto aliyezaa baadae hakuwa ni wake bali alikuwa ni mtoto wa Monk aitwae
Shin Don (tafuta drama yake utamfahamu), masikini baadae yule mtoto aliondoshwa madarakani na kuuliwa.
Lakini usisahau hadithi hizi za vibarazani zilichochewa zaidi na Team Yi Seong Gye (bila ya shaka unajua bwana huyo ndiye aliyeanzisha Utawala wa joseon baada ya kuanguka kwa Goryeo). kuna wajinga wanadai maisha yote mshindi ndiye anayeandika historia atakavyo, si unazikumbuka bibiye hadithi za IDDI AMINI na kukata kwake matiti ya wanawake?
======================
JOSEON
nimeikuta sehemu
During the Joseon Dynasty, however, Korean society experienced a draconian shift as the neo-Confucian elite and scholars declared homosexuality wicked and depraved, forcing homosexual activity to go underground and in secrecy.
unamjua Crown Princess Bong?
alikuwa ni mke wa mfalme Munjong wa Joseon, huyu bwana ndiye alirithi madaraka kutoka kwa baba yake aitwa SEJONG THE GREAT, inamaana alikuwa ni mtawala wa tano wa ukoo wa YI.
kabla ya mume wake kutawazwa kuwa mfalme, huyu dada alitimuliwa ndani ya familia ya kifalme kwa sababu ya kulala na mtumishi wa kike (inasemekana walikuwa wawili), ina maana bidada alikuwa ni lesbian na hiyo ilikuwa ni karne ya 14, kuna mengi aliyapitia ndani ya ndoa yake mpaka akafikia hatua ya kujifurahisha na wasichana wenzake (hakupendwa sana na mume wake). Hatimaye sejong the great akaamua kumtimua.
Je unafahamu japo kidogo stori ya
Sa bang ji?
nyaraka za Joseon zimeandika ya kwamba huyu kiumbe alikuwa anashare pande zote mbili za jinsia.
mwaka 1988 nchini korea muandishi fulani na director wake waliamua kutengeneza movie inayomzungumzia huyu kiumbe, wanadai huyu alikuwa anashare dozi kwa walioachwa mpaka kwa wale mabuddha wanyoa vipara wa kike (Bhikkhunī)
kuna neno linaitwa
Hypospadias nimelikuta kijiweni
maana yake ipo google
=======================
SILLA DYNASTY
mfalme Hyegong of Silla alipata kuishi mnamo karne ya 7 nchini korea ya leo, alitawazwa mfalme akiwa na miaka 8. huyu bwana wanadai hakuvutiwa sana na uwanaume wake, muandishi mmoja anaitwa Ahn Jeong-bok amefikia hatua ya kudai huyu bwana alikuwa ni mwanamke zaidi kuliko mwanaume, alifikia hatua ya kuvaa nguo za kike.
bila ya shaka tunawafahamu HWARANG, stori za vibaraza vya kahawa pia zinatutanabahisha ya kwamba eti wale vijana nao walikuwa na chembe chembe za kufungia kwao (ushoga)
kwa kunukuu zaidi baadhi ya mashairi ya nyimbo zao ambazo zimenukuliwa kwenye kitabu cha the chronocle of three kingdom.
neno hwarang kwa dunia ya leo nchini korea limesababisha kuzaliwa kwa maneno kama vile hwallyangi au hwangangnom (yenye maana ya play boy au good for nothing)
Song of Yearning for the Flower Boy Taemara
The whole world weeps sadly
The departing Spring.
Wrinkles lance
Your once handsome face,
For the space of a glance
May we meet again.
Fair Lord, what hope for my burning heart?
How can I sleep in my alley hovel?
Ch’oyong’s Song
Playing in the moonlight of the capital
Till the morning comes,
I return home
To see four legs in my bed.
Two belong to me.
Whose are the other two?
But what was my own
Has been taken from me, what now?
mpaka sasa sijui nimeandika nini.
mjinga
D A E M U S H I N