Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nilikua najiuliza umepotelea wapi mzee wa spoilers. Endelezeni stories maana mnanipa mzuka wa kuangalia realities
Jukwaa huwa linajifunga nakosa access leo nimejaribu kufuta app na kupakua tena ndio imekubali
 
talnam i think nimekata tamaa kwa Dong Jin & Dahye ni muda wa bibie kumuacha jamaa aende kiroho safi,hatakuwa na majuto badala yake ataishi na historia ya loyal girlfriend miaka 13 kuspend na mwanaume mmoja ni nadra sana kutokea kwa hulka za wanawake wengi.

Nimehamia kwa Chang Jin na Yu Jung-hapa panaonekana pagumu ila soon tutakuwa tunashangilia huyo Bibie bado ana hisia na jamaa ila hasira na kinyongo cha jamaa kutomjibu meseji ya breakup akidhani atamstop ndio kinachomfanya awe cold mbele ya mshkaji na kuamua kujiweka kwa Juwon.

Anasema hataki kurudiana na jamaa halafu akimuona anacheka kwa furaha na wanawake wengine wivu na hasira vinamshika anasema eti Chang Jin is so rude to her(kwenye preview ya episode ijayo vicheko vya Changjin na Dahye vitamkosesha raha tena ataamua kukaa na jamaa waongee)

Changjin atalalamika kuhusu Yu Jung kuonesha sura tofauti kwake tangu anafika,mtoto wa kike atareact kwamba na yeye pia kaona sura za tofauti kwa jamaa kitu ambacho kimemtia wazimu,atatiririka hadi ishu ya kukosa usingizi ile siku ambayo asubuhi yake alilia sana kitendo cha kusikia jamaa anapiga story na kucheka sana na Dahye.
I think moments zao zitaanzia hapo

Kuhusu Jong Eun na Kwang Tae nitatoa views zaidi nimemuelewa sana huyu bibie wanaendana na kijana
 
Yap mkuu, achana na marekani Kuna mdada namjua mbongo ana imba na kuelewa maana ya maneno.

Kikubwa tafuta ost zao, zikiwa na English subtitles Ina saidia Sana.
Na kuangalia series yenyewe, hata uki sikia Nyimbo una Elewa Ina relate vipi
Siri kubwa ya kuelewa kikorea ni kukisoma (Hangul) ili uelewe misingi na kanuni za uandishi, kisha rudi kwenye matamshi ya maneno, fanya hivyo hata kwa youtube tutorials. Baada ya hapo engage sana page za wakorea kwenye mitandao ya kijamii.

OST na drama mara nyingi zitakupa uelewa wa baadhi ya maneno maarufu ila namna ya kuyatumia katika mawasiliano inakuwa ngumu sana.

NB: Waafrika wengi sana (wakiwemo waTz) sikuhizi wanakijua sana kikorea.
 
Hebu weka link hapa kama hautojali, kuna drama za zamani napata tabu sana kuzipata kwenye sites nyingine.
 
talnam vp umeangalia episodes za Ijumaa za show pendwa?
Zooote yan hapa excited kutizama ya next week… hye won kaniboa, napenda juwon anavyopendana na yu jung ilaa mnh seo kyung akimsway juwon, hana chake tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…