Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

THE END
I62WWzJ.jpg
 
Naom beni jina la series linalozungumzia battle kati mongols empire dhidi ya japan. Ambapo kablai khan alipoivamia empire of japan.
Naombeni jibu
 
Uzuri wa tamthilia za Korea za kihistoria zinanishawishi kuwananga watunzi na watengenezaji ya sinema na tamthilia za hapa nyumbani kuwa ni waigizaji wa senema za Nolywood. Tunayo historia tajiri ya mila na utamaduni wetu, mapambano ya makabila, mapenzi, utawala wa watemi, vita na mapambano dhidi ya utawala wa kigeni, na mengi ya kufundisha watoto na kizazi cha kesho kuhusu Tanzania ya mababu zetu.

Hivyo, kwa kuanzia, kwa watayarishaji, kuna haja ya kurejea vitabu vya historia kutetengeza filamu au tamthilia
 
Kweli mkuu tunaweza kutengeneza tamthiliya nzuri sana kwa kutumia historia yetu. Ila mimi nadhani kikwazo kitakuwa uchumi maana kutengeneza mazingira ya kizamani haitakuwa kazi rahisi
 
Kweli mkuu tunaweza kutengeneza tamthiliya nzuri sana kwa kutumia historia yetu. Ila mimi nadhani kikwazo kitakuwa uchumi maana kutengeneza mazingira ya kizamani haitakuwa kazi rahisi

Pesa siyo msingi wa maendeleo. Kwanza wazo na kisha kulifanyia kazi. Naamini kiasi kinachotumika kugharamia filamu na tamthilia za kuigiza tamaduni za nje na mwishowe kukosa soko la uhakika, hakuwaletei tija waandaji na wachezaji. Mwanzo mugumu lakini matunda yake makubwa.

Kwa mfano, nani asingependa kuona vita ya majimaji au maisha na mapambano ya Mkwawa dhidi ya mkoloni, katika tamthilia au filamu, kuliko kuisoma tu historia ya matukio hayo!

Nina uhakika kuna watu wenye pesa za kugharamia utengezezaji wa filamu/tamthilia za kihistoria, wenye nia ya dhati na kuhifadhu na kukuza mila na utamaduni wetu. Kwamba wanaJF tunashabikia filamu/tamthilia za wenzetu, hasa hizi za Korea, ni wazi kuna soko kubwa.

Makampuni ya simu, kupitia Baraza la Taifa la Sanaa, Muziki na filamu, yana uwezo kifedha kugharamia utengenezaji wa hizo filamu/tamthilia. Taasisi na vyuo vya elimu vina uwezo mkubwa wa kutafsiri historia ya nchi yetu katika filamu/tamthilia.

Tuanzie hapo kwanza badala ya Makampuni ya simu kuendesha tu bahati nasibu kila kukicha kwa kuwakamua Watz masikini, ambao nadhani hiyo michezo ya bahati nasibu ndiyo dawa ya umaskini, kumbe wanachangiana kuwa maskini zaidi.
 
Mi natafuta Korean drama zenye comedy flani hivi dizain ya kama coffee prince..
 
Back
Top Bottom