Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hahaa nalipiza kisasi wewe jana mi nimejikaza kisabuni kumuwish maza hausi basi wewe ukafanya sherehe. Mkuki kwa nguruwe eeh?
mimi mwenyewe jana nilipita kimya kimya baada ya kuona Bae suzy amejaaa kwenye thread, nikabaki kujiuliza bae suzy amejiunga jamii forums?
 
Damushin nimeonelea nikuitage sunbae kwa sababu umenitangulia saana kwenye kdrama...unajua vingi sana kwenye kdrama world kuliko mimi. I hope you will accept this[emoji13]
 
hahahaaaaa amini maneno yangu japo kuwa sio sheria
lee seung gi, ji chang wook,im si wan wote wake yeye
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Tell me about it...ye anadhani hatumuoni anavyochepuka ila mimi nikitaka nimchepushe bae wake anavimba eti nimefika mbali. Karibu ni wapi aminas kwa Wook au Siwan?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Tell me about it...ye anadhani hatumuoni anavyochepuka ila mimi nikitaka nimchepushe bae wake anavimba eti nimefika mbali. Karibu ni wapi aminas kwa Wook au Siwan?
na ikifika tarehe 31/10/2017 ningependa uwe wa kwanza kufika kambi ya jeshi kwa ajili ya kumpokea lee seung gi, hivyo basi unapaswa uvunje ratiba ya kuhudhuria harusi ya song couples siku hiyo

hahahaaaaaa lazima aminas akaombe msaada upande wa korea kaskazini akitaka asitake
 
aigooo itanibidi nikubali offer yako ila wengi wenu sijui kwenye nafsi zenu munanichukuliaje?
We respect you...sio vema kuwasemea na wengine ila I guess they feel the same. Whoever you are, unafanya nini, una umri gani, una kimo gani I really don't care...ninachojua mimi ni kwamba unaplay part kubwa sana katika kukiendeleza kijiwe hiki. Wewe na wenzio wote mnaotuhabarisha pamoja na mwanzisha thread (sijui kapotelea wapi) kazi yenu ni njema sana..stay blessed
 
Hahaa wee sithubutu asije akaniibia na mimi ntakufwaa
 
Umenena vema, Mkuu!
Na mimi kuanzia leo naanza kumuita Sunbae-nim.. lol
 
mimi mwenyewe jana nilipita kimya kimya baada ya kuona Bae suzy amejaaa kwenye thread, nikabaki kujiuliza bae suzy amejiunga jamii forums?
Daaah!!!! Siamini Macho yangu Mpka APA Nimeamini Kuwa Ata wewe Tegemeo Uko Kwenye Njia Moja Na Huyu Anayetaka kufanya Jaribio La Kuharibu Mahusiano Yangu Na Boo Lee Dahh!!!
 
naamini alikuwa anajisemea nafsini mwake nafasi ya Khantwe bora ingelikuwa yake.

hahahaaaa fitina za damu kwa sauti ya aminas
Daaahh!! Bado Siamini Kama Ni Wewe Au Umempa Mwengine iyo User Name Etiiii!???

Mi najua Kabisaa Siwezi Ingia Pale Sababu Ao Washindani Wake Ni Hatari, na Nikawa Tayari Kuwa Bega Kwa Bega Na kuwa Mzalendo Lakini Naona Uzalendo Utanishinda Kwa Aya Mnayonifanyia
Hahahahahhaahah Damushin .
 

ahsante sana na mungu azidi kukubariki pamoja na familia yako yote na sote kwa ujumla.
kama utaniamini mpaka 2013 mwezi kama wa 8 kama sikosei nilikuwa sina uelewa wowote kuhusiana na korean drama, nakumbuka zamani marafiki zangu walikuwa wananihadithia tamthilia kama jumong, queen seondeok wakati zilipokuwa zikionyeshwa kwenye ITV ila mimi nilikuwa wala sina habari nazo kabisa.
ndipo siku moja mama yangu kipenzi alinituma nyumba ya jirani nilipofika kwenye nyumba nikawakuta wanaangalia drama ya jumong tena episode ile ya jumong anataka kuuliwa na bubunno na ndipo nikawa najiuliza.
mbona wamevaa maguo mazito na wanafuga ndevu?
nimehadithiwa jumong ni mzee mbona humu ni kijana?
mbona wanatembea na mapanga ndio maisha gani haya wanayoishi kwenye vijumba vya nyasi?
inawezekana vipi jumong aliyekuwepo zama za zamani akawa hai?

hahahaaaaa nilikuwa mjinga sana
kumbe sikujua kama malaika wa korean drama ananiita kwenye ulimwengu wake
basi siku ya pili nilikwenda kwa rafiki yangu nikamkuta anaangalia drama ya IRIS 1 nikabaki kujiuliza ina maana hawa wakorea nisiowafahamu ni mimi tu?
nikawa najiuliza season ndio nini kwa sababu aliniambia ni season 1 episode 2.

nikafanya mpango nikapata shilingi 1000 kwa ajili ya kununua cd zinazotafsiriwa na nakumbuka jumong ilikuwa ni drama yangu ya kwanza kuiangalia lakini bado nikawa naona kizungu zungu kwa sababu nilikuwa sifahamu chochote kuhusiana na buyeo, han dynasty, goguryeo na mambo mengine ila sikukata tamaa.
kadri nilivyokuwa naangalia ndipo malaika wa korean drama alizidi kuniingiza kwenye utawala wake mpaka nikaanza kufuatilia na sound track na nakumbuka sound track ya kwanza kuipakua ilikuwa ni
dont forget me = baek ji young
baadae nikanunua cd za drama ya IRIS nakumbuka niliiangalia kwa siku 4 na nilivutiwa sana na kim hyun jun (lee byung hun), baadae niliangalia bridal mask, swallow the sun, city hunter, slave hunter, gutale of the fox child, kingdom of the wind na nyenginezo.
ni ngumu sana kuniamini ila sifikishi drama 150 nilizoangalia ila mimi napenda sana kufuatilia story za korean drama kwenye mitandao tokea nimiliki computer.

tokea niwafahamu wakorea
  • sijawahi kuangalia movie yoyote ya kihindi nikaimaliza hata kama utanipa million 1 unipe zoezi la kutaja movies za kihindi nitashindwa
  • film yangu ya mwanzo na mwisho kuangalia ya kiswahili ni ndoa yangu ya steven kanumba na niliiangalia kwa sababu nilikuwa sijawahi kuangalia film yoyote ya kanumba mpaka anakufa
  • sijasikiliza nyimbo ya kizungu zaidi ya mwaka wa 2 na hata ukinipa million 1 nitashindwa kukutajia nyimbo za waimbaji maarufu kama bieber,chris brown,katty perry
  • sijawahi kusikiliza na wala kuangalia kipindi chochote cha bongo flavor na kama si jamii forums basi hata taarifa za celebrity kama diamond,ally kiba pamoja na nyimbo zao nisingeweza kuzifahamu

maswali ninayoulizwa mara kwa mara
  • je unaishi korea : sijawahi kuishi korea na wala sina uwezo wa kwenda korea.
  • je unajua kikorea: sijui kuzungumza lugha ya kikorea ila internet ndio inanisaidia kujua maneno ya kikorea na kuyatafsiri pamoja na kupata lyrics za nyimbo
changamoto ninazokutana nazo
  • utakuta mtu ananishangaa kufuatilia korean drama lakini yeye anafuatilia bollywood, hollywood lakini hajishangai.
  • utakuta mtu ananishangaa kukuta nafuatilia nyimbo za korea na waimbaji lakini yeye hajishangai kwa nini anafuatilia nyimbo za kihindi au za marekani.
inafikia wakati huwa naona ni bora nisitembelee kwenye thread hii kwani naamini kila ninapotembelea thread hii ndio nazidi kuwa na mzuka wa kufuatilia korean drama ila nashindwa kwa sababu nahisi nitakuwa siwatendei haki hususan pale mtu anapo niquote naona tabu kukaa bila ya kumjibu kwa sababu naogopa atanihisi nina dharau.
tafadhali Khantwe usinicheke nilikuwa mjinga sana ila nashangaa humu munaniona shujaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…