Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

aisee mwenye korean drama inayokwenda kwa jina la DEVIL au aliyewahi kuiona akaimaliza naomba anipe jibu la kitendawili cha yale mauaji yaliyokua yanatumia tarrot cards...je ni yule wakili au detective ndio alikuwa akihusika
 
omo omo omo nimeshajua sababu itakayokufanya uiangalie drama ya BLACK.
Tafadhali aminas nakuomba umuongeze SONG SEUNG HUN katika list ya bae wako.


[HASHTAG]#uchochezi[/HASHTAG]
Iyo Hashtag Yako...
Mi Wale Wawili Kwanza Mpaka Wanichoke Nikitahitaji Mwengine Labda Lee Joon-gi..
 
omo omo omo nimeshajua sababu itakayokufanya uiangalie drama ya BLACK.
Tafadhali aminas nakuomba umuongeze SONG SEUNG HUN katika list ya bae wako.


[HASHTAG]#uchochezi[/HASHTAG]
Whoa (ile shangaa ya Kinyumbani Korea) huu uchochezi sio wa nchi hii.
 
Damushin tuonyeshe hao watoto wakiwa na mama yao
mama yao anaitwa Jung Seung Yeon ambaye ni judge wa Incheon District Court, sheria za korea zinawabana majudge kuonekana hadharani kwenye vyombo vya habari,ni ngumu sana kuona picha yake na hata kwenye show ya the return of superman alionekana mara moja tu na ilikuwa episode ya mwisho kwa song family kushiriki kwenye show.
siku moja song il kook alipoulizwa kuhusiana na mke wake alijibu
mke wangu si mrembo kama wanawake wengine lakini ni mcheshi sana.
mnamo 09/11/2015 television ya Tvn ilitoa list ya wanawake wenye mafanikio walioolewa na celebrity wa korea kusini mwanamama jung seong yeon alishika nafasi ya pili.
  1. mnamo mwaka 2000 alishika nafasi ya kwanza shuleni kwao
  2. baadae alichaguliwa kusoma Seoul National University’s Department of Justice na kufanikiwa kusoma Masters na phd.
  3. alipata alama za juu sana kwenye Judicial Research and Training Institute
  4. akiwa na miaka 33 alichaguliwa kuwa ni jaji kwenye mahakama ya Busan ambako leo zimefanyika sherehe za BIFF ( Busan District Court judge)
  5. Ana uwezo wa kuzungumza kwa ufasaha lugha ya korea,japan,kiingereza na kifaransa.
 
Ma oppa wote hawa tuanze kupigana ngumi kisa nini? Af kizuri kula na nduguyo
sasa aminas hataki wewe umuongeze kwenye list yako lee seung gi, anataka amgande yeye tu kama kupe, halafu nimegundua yeye ni mshabiki mkubwa wa diamond na inapendeza zaidi shabiki aige kile anachofanya role model wake.diamond ana wengi hivyo basi na yeye anapaswa amuache lee seung gi awe na wengi
[HASHTAG]#uchochezi[/HASHTAG]
 
Daebak...ametisha sana nipo najiuliza huyu Song alianzaje kumuimbisha
 
Hahahahahahahahahahahhaha!!! Daah Unajua Umenifanya Nicheke Mpaka Apa Nilipo Kuna Mtu Kanishangaa..

Kwaiyo Nimfate Ninaemshabikia Niwe Nao Wengi?? Hahahahah Kumbeee Ndo Zakoo, Nishakujuaa...
 
Hahaa wewe ni mchochezi wa kiwango cha PhD aisee ila ngoja nimuachie bwana mbona ninao wengi tu ila akijitia kuleta ujuaji tutabanana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…