Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Daebak...ametisha sana nipo najiuliza huyu Song alianzaje kumuimbisha
Nikimnukuu Song il kook anasema alikutana kwa mara ya kwanza na mwanadada jung seong yeon kwa msaada wa muandishi wa habari na alipokutana naye siku hiyo alimpenda na akagundua ya kwamba anafaa kuwa mke wake.
kimbembe wakati wa kumchumbia
song il kook ni mwanadamu mwenye aibu sana, anasema aliamua kuchagua eneo maarufu la Namsan Tower kwa ajili ya kumchumbia mke wake na ilikuwa ni christmas eve na alifanya maandalizi yote lakini alishindwa kufanya hivyo kwa sababu kipindi hicho alikuwa ndiye muigizaji mkuu wa drama ya jumong ambayo iliangaliwa na 50% ya watu wote wa korea.
hahahaaaaaaa matokeo yake akamchumbia mwanadada jung seong yeon kwenye gari.
matokeo yake kwenye return of superman episode ya 89 kama sikosei akaamua kuwachukua watoto wake na kwenda kumchumbia mke wake kwenye Namsan Tower.
 
Kwaiyo Nimfate Ninaemshabikia Niwe Nao Wengi?? Hahahahah Kumbeee Ndo Zakoo, Nishakujuaa.
hahahaaaaaa umeninukuu vibaya,lee seung gi ndio anapaswa awe na wengi.
diamond ana zari,mobeto,wema,wolper, penny
 
Hawa watoto jamaniiii.. Why are they soooo cute?? Nimecheka jamani eti wanamsaidia baba yao kupropose kale kamoja kanasema 'than you for marrying me' macho na mawazo yote yako kwenye pipi...eti can I eat it now?
 
Wamependeza Sana Sana Yaani...Mi Izo Coat Zao Tuuh..Uyo Wa Miwani Mbona Bae!
uyo mwenye miwani anaitwa daehan (republic= jamhuri)
  1. ndiye wa mwanzo
  2. handsome na mrefu kama baba yake
  3. ni mwajibikaji tokea akiwa tumboni kwa sababu yeye alikuwa chini na ndugu zake wawili walikuwa juu ndio maana amepewa heshima ya kaka
  4. ni mwenye aibu kama baba yake
  5. ana weak eye sight hivyo basi atavaa miwani kwa maisha yake yote
  6. mashabiki wengi duniani wameshindwa kumtabiri daehan akiwa mkubwa atakuwa anapenda nini, kwa sababu ana umbile zuri la kuwa muigizaji,mwanamitindo, daktari au msomi wa sheria kama mama yake.

 
Hawa watoto jamaniiii.. Why are they soooo cute?? Nimecheka jamani eti wanamsaidia baba yao kupropose kale kamoja kanasema 'than you for marrying me' macho na mawazo yote yako kwenye pipi...eti can I eat it now?
hahahaaaa apo mwenye balaaa uyo wa mwisho song manse, yaani kama utamchukua kwako nusu saa tu utamrudisha kwao
 
Mkuu damushini nipe ripoti za strongest deliveryman
  1. nipo episode ya 5 muda huu ninaoandika comment hii na kiukweli inanivutia kwa sababu inaonekana huyu bwana mdogo anakutana na changamoto nyingi sana mpaka kufikia kumiliki kampuni yake binafsi .mwanadamu hapaswi kukata tamaa ya maisha
  2. nimesoma maoni ya mashabiki wengi walioangalia drama hii wamevutiwa zaidi na muigizaji msaidizi wa kiume kuliko muigizaji mkuu
  3. huyu binti anapenda kupiga wenziwe balaa lakini yupo vizuri sana
 
Hata Mimi nimevutiwa Sana yooh ho yule mtoto wa tajiri aliyeingia mtaan na kuungana na main lead ku deliver
 
Daah leo nimeshinda na hawa watoto kuanzia kwenye page ya baba yao insta, page za mashabiki YouTube huko yaani acha tu
 
kwa ambaye hajaona LOVE IN THE MOONLIGHT... hii ni kali iliifanya hadi moonlovers isipate watazamaji wengi kama walivyodhania nawashauri muichek
 
kwa ambaye hajaona LOVE IN THE MOONLIGHT... hii ni kali iliifanya hadi moonlovers isipate watazamaji wengi kama walivyodhania nawashauri muichek
Lakini sababu ni kwamba moon lovers ilioneshwa kwenye channel ya kulipia na moon light drawn by cloud ilioneshwa television ya taifa tena Siku na muda mmoja
 
Nimechunguza wakorea wanaiga sana movie za wajapan,hawa wajapan huwa wana story nzuri ila mie huigizaji wao huwa siuelewi kabisa.

Mfano nilitaka kujaribu kuiangalia "Liar Game" ya wenyewe wajapan ila imenishinda.
 
Nimechunguza wakorea wanaiga sana movie za wajapan,hawa wajapan huwa wana story nzuri ila mie huigizaji wao huwa siuelewi kabisa.

Mfano nilitaka kujaribu kuiangalia "Liar Game" ya wenyewe wajapan ila imenishinda.
Huelewi uigizaji wao ila umeelewa kuwa wakorea wanaiga...hii nayo kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…