Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hahaahaahahaaa!! Sunbae hapo mwisho umeuwaaa.
hahahahaaaa nimejaribu kuweka hisia zangu hadharani, unajua ninapenda sana kusoma comment za wachangiaji hata kama tunatofautiana kimtazamo, ninafurahi sana ninapooona wachangiaji wanaongezeka kwenye thread na kinyume chake nina chukia ninapoona wachangiaji wanapungua.
kama Khantwe atapumzika kufuatilia korean drama tafsiri yake ni kwamba pia atapumzika kuchangia kwenye thread, dongsaeng unahisi nitajisikia furaha?
kila member ndani ya JF kuna kitu kilimvutia ndio maana akaomba uanachama na kwangu mimi kivutio changu kikubwa ni thread hii na siku ya kwanza kujiunga na JF ujumbe wangu wa kwanza niliuandika kwenye thread hii ila bahati mbaya kadri siku zinavyosogea wale member walionifanya nijiunge humu ndani kutokana na kuvutiwa na michango yao wamepotea na inawezekana sababu ni majukumu mazito ya kimaisha wanayokabiliana nayo.
Nifah amepotea,
Prishaz amepotea na ndie member wa kwanza kuanza kumzoea,
Khantwe ataendelea kuwepo Jf lakini atakuwa anachungulia tu kwenye thread hii.
na wengineo ambao niliwakuta humu ndani kama hiwalisi,mkorea,kuna mmoja alikuwa anapenda historical drama na alikuwa anajiita balozi wa goguryeo kupitia ngome ya Ansi .kadri wachangiaji watakapoendelea kupungua itakuwa ni balaa na
kiukweli itafika wakati nitajisikia
  • na wae ro hwo - im lonely
  • na shim shim hae - im bored
  • moo suh wo - nitaogopa kutembelea thread kwa sababu nitakuwa peke yangu
  • jja jeung na - nitakasirika kutembelea thread
  • chang pee hae - nitajisikia aibu kutembelea thread
  • gah seum ah pah - nitavunjika moyo
  • dap dap hae - nitachanganyikiwa
  • na seul puh - nitakuwa na huzuni
 
Kweli sunbae-nim lakini usijali. Roho zikiendelea kuwepo tutakuwa bega kwa bega hadi Mungu atakapopenda.

Damushin sunbae,
Huyo mzee kwenye avatar yako ndio nani?
 

siku ya leo (14/11/2017) kituo cha polisi cha gangnam kimeweka hadharani taarifa ya uchunguzi kuhusiana na kifo cha muigizaji kim joo hyuk aliyefariki kutokana na ajali ya gari mwishoni mwa mwezi oktoba.
polisi wametangaza ya kwamba wamefanikiwa kupata black box baada ya National Forensic Service kulifanyia uchunguzi gari la marehemu na kufanikiwa kupata black box chini ya kiti cha abiria.
"tumefanikiwa kuangalia video lakini hatujapata kusikia sauti yoyote hivyo basi national forensic service bado wanaendelea kufuatilia ikiwa kama itawezekana kupata audio yoyote ile lilisema jeshi la polisi".
"kwa jinsi inavyoonekana hakuna audio yoyote iliorekodiwa hii ni kwa sababu audio function ilikuwa imezimwa, hivyo basi NSF bado wanaendelea kufuatilia kama kuna file lolote limehifadhiwa", jeshi la polisi limeendelea kusema.
baada ya uchunguzi National forensic service wanasema ya kwamba sababu ya mwisho iliopelekea kifo cha kim joo hyuk ni cranial fracture (skull fracture).
hatujaona dalili yeyote ya myocardial infarction (heart attack) na vipimo vyetu vya toxicology vilionyesha kiwango kidogo cha antihistamine.
vipimo vyetu pia havijaonyesha dalili ya coronary artery damage,abnormal blood vessel au inflammation.
jeshi la polisi limesema halitaendelea kufanya tena medical examination labda wapate ushahidi mwengine kwenye gari, hivyo basi wameshindwa kujua sababu haswa iliosababisha ajali.
matokeo ya uchunguzi wa kifo cha kim joo hyuk yatatolewa tena baadae mwezi huu.
 
Kweli sunbae-nim lakini usijali. Roho zikiendelea kuwepo tutakuwa bega kwa bega hadi Mungu atakapopenda.

Damushin sunbae,
Huyo mzee kwenye avatar yako ndio nani?
ahsante sana dongsaeng.
hahahaaaa unataka kumkera Khantwe, si mzee ni mtoto wa tatu wa song il kook anaitwa song manse.siku hiyo walikwenda kutembelea film location drama ya jang yeong sil inayozungumzia maisha ya mwanadamu aliyezaliwa katika utumwa lakini akajaaliwa vipaji teleeeeeeeee kwenye utawala wa joseon chini ya mfalme sejong mpaka badhi ya viongozi wakamwekea bifu.
alikuwa ni astronomy wa kwanza nchini korea, alitengeneza saa tofauti kwa mfano inayotumia maji,aligundua silaha nyingi sana za kivita zilizotumiwa na jeshi la joseon.

 
aigooo pumzika kuangalia drama lakini ningependa niendelee kusoma comment zako.
Ohhh eotteoke?!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] ila wewe. Nikiendelea kutembelea kama hivi mnakuwa mnanitamanisha si unajua tena ilivyo kazi kuacha ulevi sasa mbaya zaidi ni pale unataka kuacha af kila siku unajipitisha karibu na bar unawaona walevi wenzio wanagonga cheers...inataka uvumilivu kushinda hiyo vita. Nitaendelea kupita mpaka drama hizi mbili zitakapoisha ndo ntajaribu kupunguza spidi...vilevile kuna zingine ninazo kwenye flash nitaendelea kuangalia hizo laptop yangu ikitengamaa
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] umenichekesha eti utaonekana umechanganikiwa. Huko siwezi kuelewa maana nahisi nitatajiwa recipe ambazo sujawahi hata kuziona
 
Hii Drama nishaiona lakini kwa bahati mbaya sikulijua hilo hivyo inawezekana niliwaona ila sikuwatia akilini.

Hivi kule mwisho ndiyo yaliyomkuta kweli maishani mwake? Daah! Nilitamani kulia haki ya nani.
Huyo scientist ni kati ya watu ninaowakubali sana katika historia ya ancient Korea.

Wengine wakiwa ni Jumong, Lee Bang Woo, Sejong the Great, Yi San, Dong Yi na yule Peha wake, na Gwanggaeto the Great.
 
Witch court naona kama inafanana na suspicious partner,nimeangalia episode moja tu.
 
hahahahaa umenifanya nicheke kama zuzu, tafadhali agiza bakuli la urojo nitalipa.
uyo gream reaper bishoo ananimaliza sana tabia zake.
mwolago?
Usijari Nishaagiza La Asubuhi Subuh Na Nishamaliza sasa Wananidai Nimewaambia Kuwa Kuna Mtu Anatoka Seoul Anakuja Kulipa....Naona Wananitolea Vyombo Niwasaidie Kuosha Wakati Tayri Nishawadekia
Damushin Izi Mambo Zako Siyo Kabisaa..
 
Usijari Nishaagiza La Asubuhi Subuh Na Nishamaliza sasa Wananidai Nimewaambia Kuwa Kuna Mtu Anatoka Seoul Anakuja Kulipa....Naona Wananitolea Vyombo Niwasaidie Kuosha Wakati Tayri Nishawadekia
Damushin Izi Mambo Zako Siyo Kabisaa..
Mtumie namba yako akutumie hela,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…