Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

ahsante sana brother pongezi zako nimezipokea kwa mikono miwili,bae suzy na lee jong suk walistahili sana kupata tunzo.hata mimi nina huzuni kwa sababu jung hae in hajapata nafasi yoyote.
 
ahsante sana brother pongezi zako nimezipokea kwa mikono miwili,bae suzy na lee jong suk walistahili sana kupata tunzo.hata mimi nina huzuni kwa sababu jung hae in hajapata nafasi yoyote.
Shukrani sana kwa kupokea kidogo hicho In Shaa Allah vikubwa vinakuja, wadau wa huu uzi mkae tayari niko na zawadi yenu.

Brother Damushin kuna wale Polisi kwenye Black Crazy Dog na yule mwenzake(nimesahau jina) aisee watu kama wale yaani ata tunzo moja hamna kweli.!! Ukitoa Mr Black (Sung Seung Hun) basi wale Polisi ndio walikuwa wananivutia sana aisee.
 
Mzee Baba ile ni Ocn Mkuu Ni Tofauti Na Izi Za Leo Mwaka Ushaanza Ivyo.
 
ahsante sana brother pongezi zako nimezipokea kwa mikono miwili,bae suzy na lee jong suk walistahili sana kupata tunzo.hata mimi nina huzuni kwa sababu jung hae in hajapata nafasi yoyote.
Namfananishaga ni Kim Soo-Hyun.
 
ahsante sana brother pongezi zako nimezipokea kwa mikono miwili,bae suzy na lee jong suk walistahili sana kupata tunzo.hata mimi nina huzuni kwa sababu jung hae in hajapata nafasi yoyote.
Means Izi Tunzo ni Za Ushindani Sana Ndomana mpka wengine Wanalia.
Suzy Tangu Alivyoaanza Kuigiza Naona Huwa Hakosagi Izi na Jong Suk Pia.
Ata Ha ji Won Pia.
 
  • mjr95 dongsaeng, black drama ilionyeshwa na televisheni ya OCN ambayo ni cable tv, hivyo basi kama ni tunzo inapaswa iwanie kupitia kituo cha OCN.lakini sidhani kama kuna tunzo za OCN drama awards.
  • ila kuna korean cable tv drama awards ambazo mwaka huu zilifanyika mwezi machi na hushindanishwa drama zote zilizoonyeshwa na cable tv kama vile OCN, Tvn.
  • KBS ni shirika la serikali na leo hii ndio wamefanya sherehe za korean drama zilizoonyeshwa na vituo vya kbs tu.
  • SBS (seoul broadcasting station) nalo ni shirika la utangazaji nchini korea nalo pia wana haki miliki ya kuonyesha drama.
  • MBC (munhwa broadcasting corporation) nao pia wana hakimiliki ya kuonyesha drama.
 
Nae Salang amenielewesha hapo juu. Shukrani pia brother, Mapenzi juu ya hao watu yananifanya chiz aisee. Kwahiyo sielewi wala sisikii juu yao aisee.
 
Jal Ja Guys Mola Awe Nanyi Msheherekea Kisalama.
Take Care.
Muwe na Nyoyo Za Upendo Zilizojaa Imani.
Mukawapende Vizuri Mabby Zenu (Hahahaha)
Nimejikuta Tuh Nsema Hili.
Bye Guys
Happy New Year Tena.
Lot's of Love.
And JAL JA Yo.

Sijuh Nimekula Nini Leo Mbona Ivyi..
 
Utakuwa umekula mrenda
 
song joong ki
Nimerudi hapa baada ya mwaka na ninaogopa sana kuona watu mashuhuri wapo mbele yangu
alisema huku akitabasamu, wakati nilipokuwa naangalia kbs drama mwaka huu nilivutiwa sana na father is strange, heshima kwako mzee wangu kim young chul umefanya kazi nzuri sana.
niheshima kubwa sana kushinda daesang awards na leo hii nipo hapa kama presenter.

Siwezi kusahau jinsi nilivyokuwa na hofu wakati ninafngua ukurasa wa mwisho baada ya kupokea script ya 'Descendants of the Sun' miaka mitatu iliyopita. mwaka 2017 ni mwaka ambao sitaweza kuusahau kamwe kwenye maisha yangu, napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru tena timu nzima ya descendent of the sun na mashabiki wote kwa ujumla.
ingelipendeza zaidi kama na mke wangu hye kyo angelikuwepo hapa ila bahati mbaya ana shughuli nyengine muhimu sana siku ya leo.
alipoulizwa kuhusiana na maisha yake mapya ya ndoa alisema:
kiukweli nimekutana na mpenzi wangu wa maisha ambaye ninampenda sana na mwaka huu sitaweza kuusahau.
 
Namkubali sana huyu Mbwana mdogo Song joong ki nakumbuka mara ya kwanza nilimuona kwenye Frozen Flower.
 
aigooooo jamani mimi mwenzenu nam se hee mwaka mpya nimeuanza vibaya na hii tabia yangu ya kupenda kwa moyoni tu na kutamka naogopa itaendelea kunitafuna mpaka nikatubu, ni mwendo wa kuliwazana na my woori.

jung so min na lee joon wametangaza hadharani ya kwamba wana mahusiano ya kimapenzi.
kwa mujibu wa Jellyfish Entertainment jung so min alikutana kwa mara ya kwanza lee joon kwenye drama location ya my father is strange ambapo wawili hao walishiriki kwa pamoja na mahusiano yao kuanza rasmi mwezi october.
Kwa niaba ya lee joon kampuni ya Prain TPC nao wameweka hadharani taarifa ya mahusiano ya kimapenzi ya lee joon ambapo nao wamesema ya kwamba mteja wao alikutana na jung so min kwenye father is strange na ndipo wakaanza mahusiano yao.
kwa sasa lee joon yupo jeshini tokea mwezi october.
hongera kwao kwa kuanza maisha rasmi ya kimahusiano, mungu awajaalie wapendane kwa dhati na mwishoni wafunge ndoa.
nataka niamini ya kwamba mzee kim young chul ametoa baraka zake zote kwenye mahusiano haya.


nawaomba wajoseon wenzangu kila comment itakayoandikwa humu imalizae na neno hili ili kuonyesha furaha yetu kwa waigizaji hawa wakongwe walioshinda tunzo za daesang
wazee manseeeee.
 
Hadi ndoa nayo unafunga kwa ajili ya rent! Lazima tu ukatubu.

wazee manseeeee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…