Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!


Atakayemtambua Uyu Nina Zawadi Yake.
ingependeza zaidi kama ungeliweka hadharani aina ya zawadi utakayompa mshindi,naogopa nisije nikazawadiwa zawadi ya nyoka aina ya koboko (black mamba).
natania tu.
hahahahaaaaa wiki nzima nimekuwa nikiifuatilia thread yenye kuzungumzia simulizi za nyoka huyu, huwezi amini kuna watu wanafahamu maisha ya nyoka utafikiri wanaishi nao nyumba moja, na cha kushangaza thread yake inakwenda kwa kasi ya 4G kuliko thread ya toa like pata likes.
aigoooooo ndio maana najikuta nashindwa kuacha kuitembelea JF kwa sababu nitajinyima mambo mengi sana kuyafahamu katika ulimwengu huu wenye raha na karaha.
Yoon Shi Yoon a.k.a grand prince hwi
 
Hahahahahahah,Utapata Zawadi Ya Ftari InshaAllah
 
Nilijua tu hakuna zawadi yeyote ndio maana nikapiga kimya.
Damushin sunbae, POLE!
inamaana dongsaeng ulishafahamu kitakachotokezea na bado ulishindwa kunitaarifu?
naisubiri ramadhani ifike nihudhurie futari itakayoandaliwa na iron lady.
gwenchanah gwenchanah
 
Suzy And Lee Seung Gi In Talks To Reunite Through Upcoming SBS Drama
kwa mujibu wa taarifa mwanadada bae suzy na lee seung gi wamepata offer ya kushiriki kwenye spy action drama inayokwenda kwa jina la vagabond itakayoonyeshwa na kituo cha sbs.
kama wawili hao watakubali kushiriki kwenye drama hiyo basi itakuwa ni mara ya pili kuongoza drama wakiwa pamoja. mnamo mwaka 2013 wawili hao walishiriki kwenye drama inayoitwa gu family book na kilichotokezea kimeendelea kubaki ni historia yenye kuvutia.


huyu the one sauti yake inaweza kumfanya black mamba apate usingizi wa ghafla.
 
Heheehe! Nimejikuta nacheka bila ya sababu ya msingi. LOL
 
Tale of Gyeryong Fairy
mwanadada moon chae won amethibitisha kushiriki kwenye drama inayoitwa Tale of Gyeryong Fairy, ni drama ambayo hadithi yake inatokana na webtoon na inatazamiwa kuonyeshwa kwenye kituo cha tvN.
inazungumzia hadithi ya old fairy aliyeishi kuanzia utawala wa goryeo hadi joseon dynasty lakini katika maisha ya karne hii ya 21 anafanya kazi ya barista (mtoa huduma kwenye mghahawa unaouza kinywaji cha kahawa) na hatimaye baada ya miaka 699 anafanikiwa kukutana na wanaume wawili ambao anawafananisha na mume wake wa zamani ambaye amezaliwa katika nafsi mpya lakini cha kushangaza katika wanaume hao wawili hamjui ni yupi aliyekuwa mume wake.

Sun Ok-Nam ni mwanadada ambaye ni fairy ambaye ametoka mbinguni na kujikuta akiwa kwenye utawala wa goryeo.
siku moja aliamua kwenda kukoga kwenye maporomoko ya maji kwenye milima ya gyeryong,wakati akiendelea kukoga alitokezea mtafuta mbao na kuamua kuzichukua nguo zake na kuzificha jambo lilimpelekea ashindwe kuziona nguo zake na pia kupelekea kushindwa kurudi peponi alikotokea.
baadae akakubali kufunga ndoa na mtafuta mbao na kufanikiwa kupata watoto wawili lakini kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho mume wake akafariki dunia baada ya kuanguka kwenye maporomoko ya milima.
sun ok nam aliendelea kuhangaika kuzitafuta nguo zake lakini bado hakufanikiwa kuziona na pia aliendelea kusubiri karne na karne kurudi kwa mume wake japo kwa njia ya kuzaliwa upya (reincarneted).
starring
moon chae woon = criminal mind, good doctor, innocent man.
yoon hyun min =tunnel, beautiful mind
seo ji hoon = prison play book, misty​
NB:
hawa wakorea sasa wamezidi na hadithi zao za time travel lakini cha kufurahisha hazichoshi kuziangalia japokuwa unafahamu fika ni fixed.
  • my love from the star
  • legend of the blue sea
  • black knight
  • dr jin
  • goblin
  • ........................
hii drama ya good doctor joo won alijua kunifanya nidondoshe machozi kama namenya vitunguu vya maandalizi ya futari.
jamaa anajua kuigiza na ana sauti nzuri sana anapoimba.
 
Damn! Love Triangle zishaanza kunichosha. Sujui nichukue likizo?
 
Kim Ji Won And Song Joong Ki To Possibly Reunite After 2 Years In New Drama

a source from King Kong by Starship Entertainment said, “Kim Ji Won received the offer for tvN’s new drama ‘Asadal’ (working title) and is in the process of positively reviewing it.”
Song Joong Ki was also offered a role in this new historical drama and announced that he has not yet made any decisions.
“Asadal” will be co-written by Kim Young Hyun and Park Sang Yeon of “Tree with Deep Roots and “Six Flying Dragons.”
Kim Ji Won and Song Joong Ki previously appeared on the KBS 2TV’s popular drama “Descendants of the Sun.”

NB:
nakumbuka niliwahi kuwasimulia simulizi nzuri inayohusu mji wa asadal pamoja na yaliotokezea kwenye gojoseon ya zamani.
gwenchanah gwenchanah
kama unaona ni uongo katafute kitanda ulale ili kesho asubuhi uwahi shuleni kusafisha vyoo pamoja na kusafisha uwanja wa parade.
nimeona andiko langu nilirejee tena
  1. Kwa mujibu wa vitabu vya kihistoria ni kwamba Asadal ulikuwa ndio mji mkuu wa nchi ya Gojoseon ambayo ilikuwa ndio kingdom ya kwanza kutawala kwenye peninsula ya korea.
  2. muanzilishi wa gojoseon alikuwa anaitwa Dang gun, aigoooooooooo wanasema ya kwamba dang gun ni mjukuu wa mmiliki wa pepo (lord of heaven) ambaye alikuwa anaitwa Hwanin.
  3. Hwanin alikuwa na mtoto wake anaitwa Hwanung ambaye aliamua kuja kuishi duniani kwenye mabonde na milima, hivyo basi hwanin alimruhusu mwanawe hwanung aje aishi duniani pamoja na watumishi 3000 kwenye milima ya baekdu.
  4. hwanung akafanikiwa kuanzisha mji wa sinsi (city of god) akishirikiana na mawaziri wake ambao ni mbingu, ardhi ,mvua na walitunga sheria na miongozo kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu na vile vile aliwafunza binadamu fani mbali mbali kama sanaa, udaktari n.k.
  5. alikuwepo chui (tiger) na dubu (bear) ambao walitaka kuwa binadamu hivyo basi hwanung alisikia maombi yao na akawapa 20 gloves of garlic watumie kama chakula na hawapaswi kukaa juani kwa siku 100.
  6. baada ya siku 20 bwana chui uvumilivu ukamshinda na kuamua kutoka kwenye pango lakini bear (dubu) aliendelea kuvumilia hadi siku zilipokwisha na hatimae akawa mwanamke.
  7. baada ya kuwa mwanamke aliitwa ung-nyeo lakini bahati mbaya hakuwa na mwanamme hivyo basi hwanung akaamua kumfanya kama mke wake na wakafanikiwa kuzaa mtoto ambaye ni danggun wang geom.
  8. baadae dang gun alirithi madaraka na akajenga mji wenye kuitwa Asadal ambao ulikuwa upo karibu na mji wa Pyongyang (mji mkuu wa korea kaskazini) na inakadiriwa ilikuwa ni mwaka 233 BC. gwenchanah gwenchanah nilikuwa nishazaliwa wala musinibishie.
  9. baada ya miaka na miaka kwenda mbele muheshimiwa dang gun alirudi peponi.
  10. miaka ilikwenda mbele wajukuu wangu hadi mnamo mwaka 108 na 109 BC ambapo Han dynsty walifanikiwa kuangusha utawala wa gojoseon na kuigawanya gojoseon kupitia mikoa minne. kampeni ya kuivamia gojoseon iliongozwa na general yang fu na wanajeshi 50000.
  11. Hadithi yangu imeishia hapo, kunjeni mabusati na majamvi tukalaleni watoto wazuri kesho asubuhi muwahi darasani kabla ya mwalimu wa darasa hajaingia kwa ajili kuwasomesha.
 
Damn! Love Triangle zishaanza kunichosha. Sujui nichukue likizo?
uzuri wa drama ni kwamba hulazimiki kuzifuatilia zote kwa sababu hujibii mtihani wa form 4 wala form 6 kwa ajili ya uhakiki.
unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.
 
Yoo In Na In Talks As Female Lead For New KBS Drama
On May 8, Yoo In Na’s agency YG Entertainment announced that the actress received an offer to play the female lead for KBS’s new drama “Hitting on the Blind Boss” (literal translation) and is currently looking it over.

“Hitting on the Blind Boss” is about a boss named Dominic with facial recognition disorder and his secretary Jung Gal Hee who falls in love with him. Dominic was diagnosed with the disorder after he was attacked by an unknown assailant. Love blossoms after Jung Gal Hee pretends to be Veronica Park, the heiress of K Group, during a blind date.
Yoo In Na was offered the role of Jung Gal Hee. If she accepts the offer, she will be starring in a Korean drama for the first time in two years since “Goblin.”
 
Yoon Shi Yoon May Star As Identical Twins In New SBS Drama
baada ya kumalizika drama ya grand prince hatimaye kwa mara nyengine tena muigizaji yoon shi yoon amepata ofa ya kuigiza kwenye drama inayoitwa DEAR JUDGE itakayoonyeshwa na kituo cha SBS.
ni drama inayozungumzia hadithi ya mapacha wawili wanaofanana kwa sura ambao ni Han Soo Ho na Han Kang Ho lakini wanatofautiana kitabia na mfumo mzima wa maisha wanayoishi.
Han Soo Ho ni judge anayeheshimika sana kwenye jamii na Han Kang Ho ni mtuhumiwa wa kihalifu na ni mwenye kurudia kufanya makosa mara kwa mara.
ghafla Han Soo Ho anapata dharura na kutokomea ghafla bila ya kujulikana wapi amekwenda na hatimaye mdogo wake ambaye ni mkorofi anamua kubeba uhusika wa han soo ho na kuigiza kama ni jaji.

안녕히 주무세요!
annyeonghi jumuseyo!

usiku mwema
 
Sounds interesting! Japo sijibii mtihani ila nitaitazama.
 
EXO Member Kai’s Father Passes Away
On May 8, a source from SM Entertainment revealed, “Kai’s father passed away yesterday due to a chronic illness. Kai is currently staying at the wake, and the funeral will be held quietly with family and relatives

EMPTY dongsaeng tunapaswa tutoe salamu za pole kwa gream reaper wetu wa kwenye the miracle we met.
aigoooo ina maana gream reaper wetu kaamua kuchukua roho ya baba yake au ndio kafanya makosa tena kama alivyofanya kwa song hyun chul?

안녕히 주무세요!
annyeonghi jumuseyo!
usiku mwema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…