Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

“100 Days My Prince”
kuna aliyebahatika kuiangalia hii drama iliyoanza wiki hii kupitia kituo cha TvN?
inazungumzia maisha ya crown prince Lee Yool ambaye amepatwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana na hatimaye kushindwa kurudi mji mkuu kwa siku 100 jambo lililopelekea kufunga ndoa na mwanamke mwengine akiwa mafichoni.
  1. kabla ya hapo alikuwa tayari ameshafunga ndoa na mtoto wa left councillor ambaye ni kama waziri mkuu ila kama kawaida ya ndoa za kisiasa hakuvutiwa na mke wake, kibaya zaidi mke wake alibeba ujauzito na cha kushangaza hajawahi kulala na mume wake hata sekunde moja. humu ndani kwa episode mbili za mwanzo zimejikita zaidi kwenye vita ya kisiasa kati ya pande tatu kuu zinazokinzana.

  • malikia ana mtoto wake hivyo basi anataka arithi nafasi ya crown prince lee yool anaamua kufanya kila namna amsambaratishe bwana mdogo ambaye ni mtoto wake wa kambo (step mother)
  • mfalme aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi baada ya kumpindua kaka yake, na muongozaji mkuu wa mapinduzi baada ya kufanikisha azma yake alimuomba mfalme aruhusu ndoa kati ya mtoto wake wa kike na crown prince. Hivyo basi nguvu kubwa ya kiuongozi ipo chini ya huyu left councillor Kim Cha-Eon.

  1. kwa watazamaji wa bongo movies naomba wanisaidie kunitajia waigizaji bora wenye umri chini ya miaka 15 tafadhali, dakika 40 za episode ya mwanzo zilikuwa za kuvutia sana, hawa watoto wawili ambao ni jung ji hoon na heo jung eun uigizaji wao umenifurahisha zaidi ya kuangalia uigizaji wa ray na wema sepetu.Nimevutiwa zaidi na uhusiano wao wa kimapenzi ulivyoanza kuchipua tokea wakiwa wadogo ila ndio hivyo tena siasa ikatenganisha uhusiano wao, sijui kitatokezea kitu gani siku ambayo mwanadada Hong-Sim atakapogundua ya kwamba aliyeongoza kampeni ya mauaji ya wazazi wake ni mfalme ambaye ndiye baba wa crown prince lee yool. Nisiandike sana nikawachosha ila kwa anayehitaji kuangalia historical drama basi hii ipo vizuri na love story yake itakuwa onfire.


cherry blossom tree nitakapokutana na bibi yenu miaka 5 ijayo
EXO D.O
na mwanadada Nam Ji Hyun ndio waigizaji wakuu wa hii drama.
hivi hawa wakorea kwa nini wanapenda kutuwaminisha ya kwamba ni rahisi sana kumtongoza mwenza wako.
ukiziangalia mara kwa mara hizi drama zinazozungumzia tawala ya joseon utagundua ya kwamba love story kati ya wawili kwa kiasi kikubwa huchangiwa na mti wa cherry blossom.
yaani binti ukimpeleka sehemu yenye miti hii hujisikia furaha sana kama mcheza kamari anaposhinda kitita kikubwa na itokezee vipande vya barafu na maua (snow flower) viwe vinaanguka kwa wakati mmoja
daebak siku hiyo hiyo atakuwa mchumba wako.
pumbavu zao wakorea kwa kuzidi kunitia ujinga na umri huu nilionao wa miaka 75.


ost 1 ameimba mwanadada gummy na unaitwa erase.
 

Attachments

  • 1536866418674.png
    67.4 KB · Views: 37
  • 1536867282987.png
    743.8 KB · Views: 50
Huyu Takashi Mori ni Zaidi ya Muigizaji yaani hata lee Wan ik Amuingii
huwezi amini lile tukio la kuuliwa lee wan ik na mwanadada ae shin nimeliangalia mara mbili.
hahahahahahaaaaa nilifikiri lee wan ik yupo kwenye ndoto.
takashi mori naye ni shetani aliyevuka mipaka na mipango mingi ya kwake yeye inafanikiwa.
ila natamani lee wan ik angeliendelea kushiriki uhusika wake japo kwa episode 1.
asije akamtoa roho kudo hina wangu nitamchukia muandishi mpaka kesho

unataka mission yako ifanikiwe kwa urahisi?
wasiliana na kudo hina
full stop
 

Attachments

  • 1536870439017.png
    4.3 KB · Views: 31
Mi mgeni kabisa jukwaa hili, vipi hakuna series nyingine nzuri inayo-trend mwaka huu
Maana nimefuatilia uzi asilimia kubwa stori ni Mr. Sunshine tu. Wafuatiliaji wazuri wa Korean drama mtujuze na zingine basi.
  1. mother
  2. welcome to waikiki
  3. my mister (my ahjussi)
  4. whats wrong with secretary kim
  5. come and hug me
  6. are you human?
  7. prison play book
  8. a korean odyssey (hwayugi)
  9. wok of love
  10. the miracle we met
  11. grand prince
  12. life on mars
  13. misty
  14. should we kiss first?
  15. 30 but 17
  16. switch change the world
  17. voice season 2
  18. mistress
  19. bad guy vile city season 2
  20. good bye to good bye
  21. suits
  22. lawless lawyer
  23. life
  24. ms hammurabi
  25. your honor
  26. your house helper
  27. the undeteables
  28. pretty noona who buys me food (something in the rain)
  29. sketch
  30. return
  31. partner for justice drama
  32. a poem a day.
 
Me natembeaga na Wireless za maofisi na za watu binafsi tu nanyonya episode za kutosha izi drama zenye episode 24 ni jambo la masaa tu zinakuwa kwny cmu yng ikifika jioni ni kucheki
 
“Room No. 9” Releases Chilling Official Posters
“Room No. 9” ni drama itakayozungumzia hadithi ya mwanadada Eulji Hae-Yi (kim hee seon) ambaye ni mwanasheria aliyeajiriwa na kampuni maarufu nchini korea inayotoa huduma za kisheria. Ni mwanasheria ambaye huwapembejekea (flatters) sana watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa kwenye jamii huku akiwakandamiza watu wasio na uwezo.

Ki Yoo-Jin (kim young kwang) ni rafiki wa kiume wa mwanadada Eulji Hae-Yi ambapo yeye ni medical doctor, anaonekana ni kijana mashuhuri na mchapa kazi lakini kumbe ana tabia za kihuni nyuma pazia.

siku moja katika harakati zake za kazi mwanadada Eulji Hae-Yi anakutana na mwanamama Jang Hwa-Sa (kim hae sook) ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama, wawili hao walikutana kwenye chumba namba 9 ambacho ni maalum kwa kuwatembelea wafungwa.
kwenye chumba namba 9 walipokutana wawili hao walijikuta wakitokezewa na tukio la ajabu lililosababisha mabadiliko makubwa ya kimaisha (fate) kwa wawili hao.
unajua kilitokezea kitu gani?
miili yao ilibadilika.
kwa mfano mwili wa bakhressa ndio uwe mwili wa damushin na mwili wa damushin ndio uwe mwili wa bakhressa.

woyoooooooo bakhressa atalia kama panya aliyeshikwa na nyau huku damushin akifurahi kama panya aliyemuuwa nyau kwa mara ya kwanza katika historia ya ulimwengu.
unafikiri kuna atakayemuamini bakhressa madai yake?

drama hii itaonyeshwa na kituo cha TvN kuanzia 06/10/2018.
itakapomaliza drama ya MR SUNSHINE ndio itaanza drama hii.
stori yake imeshanivutia na kituo cha tv ni TvN.

huyu binti nimemuona kwenye drama ya FAITH na amezaliwa miaka 41 iliopita.
huyu ahjumma hakuna asiyefahamu uwezo wake kwa mfuatiliaji wa korean drama.

daebak mwezi wa 10 inshaallah itabidi nimuige Numbisa, ni mwendo wa kudownload episode nyingi halafu naziangalia.
 
Lee Je Hoon And Chae Soo Bin’s Upcoming Airport Drama Releases Character Posters
“Where Stars Land
ni drama itakayoonyeshwa na kituo cha SBS kuanzia 01/10/2018 baada ya kumalizika drama ya 30 but 17.
Lee Soo Yeon ni muajiriwa mpya kwenye uwanja wa ndege wa Incheon International Airport uliopo nchini korea, maisha yake ya elimu ni mhitimu wa Korea Advanced Institute of Science and Technology, ni mwanadamu ambaye hapendi kujichanganya na wafanya kazi wenzake.
picha yake imeandikwa maneno yafuatayo
nimekutana na yule anayenikumbuka

lee so yeon anafanikiwa kukutana na mwanadada Han Yeo Reum ambaye naye pia ni muajiriwa mpya ila maisha yake amepitia changamoto nyingi sana zenye kukatisha tamaa, kazi yake kubwa ni kuwahudumikia abiria wanaosafiri.
picha yake imeandikwa maneno yafuatayo kwa kiswahili kisicho rasmi
unapaswa uwe hapa
Lee Dong Gun ataigiza nafasi ya kiongozi mkuu wa operations department na mwanadada Kim Ji Soo ataigiza nafasi ya mkuu wa idara inayoshughulika na utoaji huduma kwa wasafiri.
mwezi wa 9, 10, 11, 12 unaweza ukajikuta umechukua likizo bila ya idhini ya bosi wako.
 

Attachments

  • 1536939025274.png
    460.3 KB · Views: 40
Aisee,
Prison Playbook - "Pengujaniiiim " bonge la sirizi
 
[emoji23][emoji23][emoji23]huo mfano wa bakhresa na damushin umenichekesha sana

Nipo na application ya dramania,huwa nacheza na shows pale,naangalia latest naiweka favourite(ili nisiisahau) huku nikisubiria iishe niivute(through Wikipedia huwa naona namba za episode ya movie husika) . wakati nasubiria huwa naangalia nyingine zilizoisha,vikorea vipo vingi jaman daah!
Utamu wa vikorea ni kuwa na movie nzima raha sana.
 
upcoming korean drama
“The Smile Has Left Your Eyes”
Release Date: October 3, 2018

  • Yoo Jin-Kook ni detective ambaye anahusika na upelelezi wa tukio la mauaji ya mwanafunzi wa kike wa chuo kikuu.
  • pia ana mdogo wake wa kike ambaye anatokezea kumpenda mvulana ambaye hakumbuki maisha yake ya utotoni aliyoyapitia na pia mvulana huyo hana mwenendo mzuri wa kivitendo.
  • upande wa pili detective amekuwa akimshutumu mvulana huyo kuwa ndio muhusika wa mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu.
usiyempenda kaja nyumbani kwako na anataka chakula ulichokitafuta kwa nguvu zako.
aigoooooo
poster limeshaonyesha kitakachotokezea humu ndani.
hahahahhahaaaaa detective huenda akanyoosha mikono juu.

mapenzi yamemfanya choi eugene aghairishe safari ya kwenda marekani kwa kisingizio eti amesikia kelele za wajapani.
pumbavu zake eugene ndio maana nasubiria nitimize miaka 70 ndio nifikirie kuingia kwenye ulimwengu wa lavu kwa sauti ya lady aeshin
starring
seo in guk = (shopping king louis, king face, reply 1997 drama)
jung so min = (because this is my first life, father is strange drama)
park sung woong = (life on mars, man 2 man, waikiki drama)


  1. itakapomaliza drama ya familiar wife ndipo itakapoanza drama hii kupitia kituo cha TvN.
  2. itakapomaliza drama hii itafuata drama ya boyfriend na waigizai wakuu ni song hye kyo na park bo gum.
 
team korean family drama fans
ingizo jipya (15/08/2018)
My Only One
Kim Do-Ran ni msichana mwenye tabia njema, mcheshi, anajituma licha ya kuwa anakabiliwa na tatizo la ukosefu wa fedha. Ndoto yake kubwa ni kumaliza elimu yake ya chuo kikuu ili awe mtumishi wa umma. Baada ya miaka 28 siku moja anafanikiwa kuiona sura ya baba yake ambaye walipoteana na ndipo baba yake anamuelezea sababu iliyomfanya afiche uhusika wake kwa miaka 28.
pia baba yake kwa mujibu wa episode mbili za mwanzo amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la mauaji na kumtelekeza mtoto wake
  • kwa mujibu wa Nielsen korea episode ya kwanza iliangaliwa na 21.2% ya watu wanaoishi korea kwa siku ya jana.
  • episode ya pili iliangaliwa na 24.3% ya watu wanaoishi korea kwa siku ya jana.
ina maana wakorea ni wapenzi wakubwa sana wa family drama.
starring

choi soo jong ahjussi = (emperor wang guhn, emperor of the sea, dae jo young, comrade drama)
uee noona = (my husband oh jak doo, manhole, marriage contract, white night drama)
Lee Jang-Woo hyungnim = rosy lovers drama na pia itakuwa ni drama yake ya kwanza baada ya kutoka jeshini.
 
Inapatikanaje??
 
Na kwa Tanzania ni asilimia moja tu imetizama episode ya kwanza ambayo ni mimi tu [emoji23][emoji23][emoji23]. Leo nashusha episode ya pili. Bonge la drama ile sehemu hukumu inapitishwa unaweza mwaga machozi. Mwanzo wa episode wazazi wote wawili wanaonyesha upendo wa dhati kwa mtoto wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…