DAEMUSHIN
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,428
- 120,464
“100 Days My Prince”
kuna aliyebahatika kuiangalia hii drama iliyoanza wiki hii kupitia kituo cha TvN?inazungumzia maisha ya crown prince Lee Yool ambaye amepatwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana na hatimaye kushindwa kurudi mji mkuu kwa siku 100 jambo lililopelekea kufunga ndoa na mwanamke mwengine akiwa mafichoni.
- kabla ya hapo alikuwa tayari ameshafunga ndoa na mtoto wa left councillor ambaye ni kama waziri mkuu ila kama kawaida ya ndoa za kisiasa hakuvutiwa na mke wake, kibaya zaidi mke wake alibeba ujauzito na cha kushangaza hajawahi kulala na mume wake hata sekunde moja. humu ndani kwa episode mbili za mwanzo zimejikita zaidi kwenye vita ya kisiasa kati ya pande tatu kuu zinazokinzana.
- malikia ana mtoto wake hivyo basi anataka arithi nafasi ya crown prince lee yool anaamua kufanya kila namna amsambaratishe bwana mdogo ambaye ni mtoto wake wa kambo (step mother)
- mfalme aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi baada ya kumpindua kaka yake, na muongozaji mkuu wa mapinduzi baada ya kufanikisha azma yake alimuomba mfalme aruhusu ndoa kati ya mtoto wake wa kike na crown prince. Hivyo basi nguvu kubwa ya kiuongozi ipo chini ya huyu left councillor Kim Cha-Eon.
- kwa watazamaji wa bongo movies naomba wanisaidie kunitajia waigizaji bora wenye umri chini ya miaka 15 tafadhali, dakika 40 za episode ya mwanzo zilikuwa za kuvutia sana, hawa watoto wawili ambao ni jung ji hoon na heo jung eun uigizaji wao umenifurahisha zaidi ya kuangalia uigizaji wa ray na wema sepetu.Nimevutiwa zaidi na uhusiano wao wa kimapenzi ulivyoanza kuchipua tokea wakiwa wadogo ila ndio hivyo tena siasa ikatenganisha uhusiano wao, sijui kitatokezea kitu gani siku ambayo mwanadada Hong-Sim atakapogundua ya kwamba aliyeongoza kampeni ya mauaji ya wazazi wake ni mfalme ambaye ndiye baba wa crown prince lee yool. Nisiandike sana nikawachosha ila kwa anayehitaji kuangalia historical drama basi hii ipo vizuri na love story yake itakuwa onfire.
cherry blossom tree nitakapokutana na bibi yenu miaka 5 ijayo
EXO D.O na mwanadada Nam Ji Hyun ndio waigizaji wakuu wa hii drama.
hivi hawa wakorea kwa nini wanapenda kutuwaminisha ya kwamba ni rahisi sana kumtongoza mwenza wako.
ukiziangalia mara kwa mara hizi drama zinazozungumzia tawala ya joseon utagundua ya kwamba love story kati ya wawili kwa kiasi kikubwa huchangiwa na mti wa cherry blossom.
yaani binti ukimpeleka sehemu yenye miti hii hujisikia furaha sana kama mcheza kamari anaposhinda kitita kikubwa na itokezee vipande vya barafu na maua (snow flower) viwe vinaanguka kwa wakati mmoja
daebak siku hiyo hiyo atakuwa mchumba wako.
pumbavu zao wakorea kwa kuzidi kunitia ujinga na umri huu nilionao wa miaka 75.
- Watch 100 Days My Prince Episode 1 online at Dramanice
- Watch 100 Days My Prince Episode 2 online at Dramanice
ost 1 ameimba mwanadada gummy na unaitwa erase.