BogoshipseyoMBC Announces It No Longer Plans To Air New Drama “Prometheus
kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka shirika la habari la MBC wamethibitisha kutokuendelea na mipango ya kuisimamia action spy drama itakayokwenda kwa jina la prometheus ambayo inakadiriwa kugharimu 26 million dollar ambazo ni wastani wa 60 billion za kitanzania.
chanzo hicho kutoka MBC kimedai ya kwamba maamuzi ya kuachana na mpango wa kuisimamia drama hiyo umefikiwa muda mrefu kabla hata muigizaji Ha Ji Won hajatangaza uamuzi wa kutokushiriki kwenye drama hiyo.
Mi Kuna Aina Hii Pia Ya Watu huwaga Nabishana Nao kuhusu Izi Drama.OK nimekuelewa.
kwa mawazo yangu uyo DJ alitakiwa ahakiki kwanza taarifa zake kabla hajaamua kuiweka sokoni project yake aliyoitafsiri ila bahati mbaya ameshindwa kufanya hivyo au pengine amesahau.
Alitakiwa afahamu ya kwamba hiyo project itaangaliwa na jamii ya watu tofauti wakiwemo wafuatiliaji wa korean entertainment na wasiofuatilia hallyu star kwenye mitandao.
Tatizo linakuja pale kwa wasiofuatilia habari za mitandaoni atakuwa amewadanganya kwa kitendo chake cha kuweka maelezo yasiokuwa sahihi kwenye project yake na kusababisha kujipotezea heshima yake kwenye kazi.
Hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa ya kwamba land of war ni jina jengine la gwanggaeto drama ndio maana nilikuuliza land of war ndio ipi?Profile
View attachment 906154
- Drama: Gwanggaeto, The Great Conqueror (English title) / King Gwanggaeto the Great (literal title)
- Revised romanization:Kwanggaeto Taehwang
- Hangul: 광개토태왕
- Director: Kim Jong-Sun
- Writer: Jo Myung-Joo, Jang Ki-Chang
- Network: KBS1
- Episodes: 92
- Release Date: June 4, 2011 - April 29, 2012
- Runtime: Saturday & Sunday 21:40
- Language: Korean
- Country: South Korea
nashindwa kuelewa sababu ipi hasa ya msingi inayonifanya nipate usingizi pindi ninapoiangalia hii drama ya The Smile has left you Eyes.
Hmmsee you again
Hmm! Unayako! Mbona Ni Drama Nzuri Sananashindwa kuelewa sababu ipi hasa ya msingi inayonifanya nipate usingizi pindi ninapoiangalia hii drama ya The Smile has left you Eyes.
ahjummaaa mtarajiwa miaka 20 ijayo hii avatar yako naomba uiondoe tafadhali.Devilish joy kamera wanayotumia duh utadhan wanashutia kwa tecno zetu
On going inayonitesa kuisubiria kila mwisho wa week
100days my prince ,another ongoing tamu
Hii ipi tena?
ahjummaaa mtarajiwa miaka 20 ijayo hii avatar yako naomba uiondoe tafadhali.
inanifanya niwe uncomfortable kwa sauti ya won deuk.
utani
hahahahahaaaaaaa meok goo ana vituko kama watu wa south african walio ondoka juzi baada ya kumrudisha tajiri wao aminas.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]damushin,yes you damushin of all the people u choose to scam a kid(avatar) in meok goo's voice and lines
Haka katoto nimekapenda kama njaa ya meok mpaka kumtapeli governor,chezea ndoto ya kula bakuli zima la supu na wali
hahahahahaaaaaaa meok goo ana vituko kama watu wa south african walio ondoka juzi baada ya kumrudisha tajiri wao aminas.
lakini sijafurahishwa kiupande fulani kitendo cha yule bwana mdogo kutokupewa muda wa kutosha kwenye drama, alipaswa apewe screen time ya kutosha apate kuzidi kujiamini na kukuza kipaji chake cha uigizaji.
mfano mdogo angalia jinsi gani ko woo rim alivyokuwa anapewa screen time ya kutosha kwenye drama ya Mr Sunshine mpaka inafikia kipindi ule uoga wa kufanya kazi na waigizaji wakubwa kama lee byung hun unaondoka.
upo sahihi kadri atakapopata project za kufanya ndio uwezo wake utaongezeka.Ila kwa nafasi ndogo alizopewa kazitendea haki hope atapata dili jingine mbeleni la kumkuza zaidi
yes majibu yako yapo sahihi dongsaeng.Kwa takwimu gani zilizofanyika? Watu wanajua wengi ila ni wachache wenye moyo was kusaidia watu! Chief he's too quite good
Uko makinikama ni mtihani wa darasani alama zako ni 50%.
- katikati ya wiki simba walikunyima furaha ila manchester united walikupa furaha
- leo hii nasikia simba wamekupa furaha ila manchester united wamekunyima furaha
yap nimejikuta napata mapumziko ya kuangalia korean drama bila ya kutarajia, wiki inamalizika nimeangalia episode 6 tena kwa siku moja jambo ambalo ni nadra kutokezea.
natamani hii hali ninayokumbana nayo wiki hii iendelee kiupande wangu japo kwa wiki moja nyegine.
dah huwezi amini nimeamua kufukua makaburi muda huu humu ndani ila bahati nzuri marehemu wote wamebaki vile vile na harufu yenye kuvutia, inaonekana safari yao ni mapumziko ya peponi kama wafiwa wa mv nyerere.
july 5 / 2017 ndio ilikuwa ni mara ya kwanza kusoma comment zako, daebak. Ni mwaka mmoja na miezi 2 tokea nikufahamu japo kwa maandishi ila umekuwa zaidi ya rafiki ambaye tunaonana kila siku.
unazikumbuka hizi comment zako?kupitia comment ya mwanzo ulinifanya na mimi niitafute hii drama ya queen for seven days na sikujutia maamuzi yangu.
- Yaani naomba uangalie iyo Queen of Seven days ni Nomaaa yaani utaichoka inasisimua balaa,Na ina Ost nzuri sana kam ni mpenzi wa zile nyimbo
- Hivi na lee seung gi naye bado ajatoka ???
- Uyo alocheza kwenye bridal Mask si ndo anacheza now kwenye My sassy girl....
- Naombeni Muangalie FIGHT FOR MY WAY Hii drama kama kurelax na kuenjoy yaani apa ndo mahala pake, Ina vichekesho sana na ni nzuri pia, Forever Korean Drama
naomba uondoe khofu kwenye nafsi yako,namshukuru Mungu ni mzima wa afya mpaka muda huu
ahsante sana kwa kuwa zaidi ya rafiki dada yangu.
utabaki kuwa ni malikia wa kila siku tofauti na yule malikia wa siku 7
jeongmal gomabseubnida
ahsante sana
View attachment 875689
Nitaitafuta HiiUPCOMING DRAMA
Mama Fairy and the Woodcutter / Tale of Gyeryong Fairy
05/11/2018
beautiful lady moon chae won amerudi tena na stori ya kusadikika kupitia kituo pendwa cha TvN pindi itakapomaliza 100 days my prince drama
acha tu nianze na paukwa na nyinyi mutaitikia pakawa ila sijui maana yake ni nini na anayehisi anadanganywa akwende zake gymkhana au colassium guest house akapumzike (natania tu)
omo omo omo
View attachment 906698
hapo zamani za kale kwenye utawala wa Goryeo dynasty alikuwepo mwanadada mmoja anayeitwa Sun Ok-Nam ambaye ujio wake hapa duniani ulikuwa ni wa kimaajabu (fairy).
sasa basi siku moja huyu bidada alikwenda kwenye maporomoko ya maji yaliopo maeneo ya Gyeryong kwa dhumuni la kusafisha mwili wake (kukoga). Wakati akiendelea kukoga alitokezea mvulana mmoja ambaye kazi yake ilikuwa ni kutafuta nishati ya kuni au mbao akazichukua nguo zake kwa dhumuni la kuzificha.
Tukio hilo lilisababisha mwanadada Sun Ok-Nam kushindwa kurudi peponi hivyo basi akaamua kuishi maisha ya ulimwengu huu wa kidunia na bwana mkata kuni na hatimaye walifanikiwa kupata watoto wawili lakini bahati mbaya sana mume wake alifariki dunia baada ya kuanguka kwenye maporomoko ya milima. Sun Ok-Nam alihangaika sana kuzitafuta nguo zake alizokuja nazo ili aweze kurudi kwenye maisha yake ya asili lakini hakufanikiwa kuziona. Sun ok Nam aliamua kuendelea kuishi kwenye ulimwengu huu huku akiwa na matumaini ya kwamba siku moja mume wake atazaliwa tena kupitia mwili mpya (reincarnated).
baada ya miaka takribani 699 kupita siku moja akiwa kwenye milima ya gyeryong ambako alifungua biashara ya kuuza kinywaji aina ya kahawa alitembelewa na wavulana wawili hivyo basi akapata hisia ya kwamba mmoja kati ya wavulana hao wawili amebeba nafsi ya aliyekuwa mume wake ambaye ameshamsubiri kwa karne 7 tokea afariki dunia bahati mbaya sana kati ya wale vijana wawili hakujua ni yupi hasa aliyebeba nafsi ya mume wake, hivyo basi aliamua kuwafuata vijana wale hadi mji mkuu wa korea (seoul) kwa dhumuni la kuwachunguza.
hadithi yangu imeishia hapo na mwenye maswali akamuulize da mange 😡😡
View attachment 906697
nimemkumbuka Khantwe natumai ni mzima wa afya.
View attachment 906718
dah hizi hanbok siku za mbeleni itanilazimu nimtafutie my only one, itapendeza sana tukizivaa mtoko wa jioni kwa ajili ya chakula, natumai hatoniuliza
honey mbona unatumia sana, hivi umeshaweka hela ya kununua umeme na malipo ya watoto kwa ajili ya skuli na madrasa.