Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Haswa, yule Joeng Jo(정 조) alitaka kuonyesha kuwa ni mzalendo kuwa yeyote anaweza kupitiwa na sheria. Kifo cha Sado{사도) inasemekana chanzo chake ni tata sana wengine wanadai kuwa waliframia kesi na wengine wanadai kuwa alikuwa na matatizo ya akili hivyo alikuwa anawabaka M-Cort lady na Ma-Maid(both are female servants) Ingawa mfalme alifanya maamuzi magumu sana. Katika utawala wake Joeng Jo(정조) suala la kuwawa Mwanae Prince Sado(사도) ndiyo doa .
 
Great Conqueror nimefika ep ya 15 sasa, ningeshafika zamani sema ile site inazingua so nahamia kwenye Yi San ikikaa poa narudi tena kuendelea.
Itoshe tu mimi kusema ni nzuri, tena nzuri kwelikweli.

Ila hivi kwanini Prime Ministers wa Korea wanakuwaga wanoko sana? Maana hapa kwenye King Gwanggaeto waziri huyu Mkuu hana tofauti na yule wa kwenye Jumong, japo wa kwenye Jumong alizidi jamani! Japo huyu sijafika mbali ila afadhali yeye ana kauzalendo kidogo.

Kama kawaida nimeendelea kuvutiwa na ‘adopted brothers’ wa Prince Damdeok kama ilivyokuwa kawaida ya kwenye historical drama lazima wawepo.
Kiukweli huwa nawapenda mno ndugu hao wa hiyari maana huwa na upendo wa kweli tofauti na ndugu zao ambao baadae hugeukana.
Hapa nawazungumzia akina Bil Disu, Seokgae, Hwang Hoe.

Upande wa wapinzani nao wamenifurahisha pia hahaaaaa, harakati zao za kutaka kumuua Daemok zimeniacha hoi.
Temper la baba Murong Chui na mwanae mimi hoi!
It’s worth watching...

Damushin jana niliona quote yako hapa ila naona umeiondoa, sio mbaya nikikujibu anyway maana nilishaisoma [emoji12]...
Niliwahi kujaribu kuongeza bae mmoja kama Khantwe ...nae si mwingine bali Kim Soo Hyun ila baadae akanishinda, nimeona nibaki tu loyal kwa Il Gook Sung Maana nimeshindwa kabisa kupata mbadala wake.
I like the way he is calm, yani jamaa huwa anaigiza akiwa relaxed mnoooo.
Hadi unasahau kama anaigiza, hii ndiyo uniqueness yake inayofanya nimkubali sana.

Kuhusu Terms Of Endearment niliwahi kuona umeandika mwaka jana au juzi hivi, ilinivutia nikajaribu kuitafuta kwenye site yangu pendwa sikuipata nikaamua kuachana nayo kwa muda ila lazima tu nitaiangalia, na hivi tena Oppa bae yupo huko? Hiyo ni must watch.

Haya jamani ngojeni nirudi kuangalia Gwanggaeto na Yi San mie... [emoji327] [emoji897]



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mpaka sasa kwenye Historical drama mtu aliyenikosha na mapigo yake ni Gukson Muno(the Great Queen)

Hebu acha usinikumbushe Gukseon Munno bhana, nililiaaaaaaaaa alipouawa kizembe sababu ya ujinga wa Bidam.
Ila ile drama ilijua kuniliza Wallah, episode ambazo sikutoa machozi ni chache sana.

Ndio maana hadi leo drama zangu 3 bora za wakati wote ni Jumong, Queen Seondeok na Dong Yi.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huyo waziri mkuu alianzisha mapinduzi lkn mwisho wake ulikuwa wakutisha. Pia hapo mbeleni atatokea Mchawi mmoja anaitwa Ha muji ambaye atakuwa ni military advisor huyu mtu anaakili nyingi mno

Yi san miye nimefika ep. 27 kifupi ni nzuri.

Site(drama cool) ina matatizo gani?!
 
Ndugu unaweza kunisaidia Source ya hiyo historia ya kina Sambong nami nikajifunze zaidi kuhusu wao?!
 
Hii Queen Sandeok ndio ameigiza yule dada wa kwenye 49 days? Huwa naitamani ila ndefu sana khaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji12][emoji12][emoji12] mimi nina bae wengi wewe karibu kila drama natoka nae mmoja japo huwa sidumu nao, halafu mimi mara nyingi huwa navutiwa na second lead sijui kwa nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wengi wao wanaochukua maamuzi ya kuacha wenzi wao kwa sababu dhaifu zinazoweza kutatuliwa hufikiria wametatua matatizo yao kumbe ni kinyume chake, mara nyingi wanaoacha kwa sababu nyepesi husukumwa zaidi na hasira za kimaamuzi kuliko sababu zenyewe za kuachana ndio maana hufikia hatua hutamani kurudiana lakini ndio hivyo muda unakuwa umeshaenda mbali na maamuzi yake.
hata wale wasiotaka kurudia mara nyingi husukumwa zaidi na kiburi kilichochanganyika na aibu lakini kiasili hakuna hata mmoja asiyemkumbuka mwenzake, kibaya zaidi kadri unavyokuwa mbali basi ndio huzidi kumkumbuka mwenzako tofauti na wale wanaokutana mara kwa mara.
maamuzi yanabaki kwa aliyeachwa either kutoa nafasi kwa mara nyengine tena kwa kutegemea yale yaliowafanya waachane watayatatua or atafute mwengine wa kumliwaza.

 
umeona eeehhhhhhh!!!!
tokea nianze kuwafuatilia wakorea sijapata kuona muigizaji mwenye uwezo wa kumshinda song il kook kwenye kuzungumza kwa utaratibu hususan akiwa na mwanamke, yaani hujisahau kabisa kama naangalia maigizo.
nasisitiza sijapata kumshuhudia muigizaji anayemshinda song il kook kwenye mazungumzo dhidi ya mwanamke.
wengi wao wanavurumisha lakini jamaa mhhhhhhh ni sheedah utatamani huyo binti anayeshushiwa vidonge uwe ni ukweli na si drama.

lakini dada yangu unaonaje nifanye maandalizi ya kukutambulisha kwa huyu ahjussi mtarajiwa anayeitwa JO/CHO SANG WOO?
ulishawahi kuangalia project yoyote ya huyu mwanadamu?
uzungumzaji wake na yeye ni taratibu utadhani hotuba za bwana yule.
fanya haraka kabla yule mbeba vya wenziwe hajamuona.

anaye wa kwake anaitwa JO SANG WOOK basi pindi atakapomuona na huyu huenda akamchanganya kwenye daftari lake la mahudhurio
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sunbae unapenda kunichokoza mimi sasa hivi wananitosha Jin Goo wa mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jang Hyuk in talks to appear in new JTBC's historical drama 'My Country',​
kama atakubali kushiriki drama hii ataigiza uhusika wa yi bang won ambaye baadae anakuwa mfalme wa tatu wa joseon. Lee bang won alimsaidia baba yake kwa kiasi kikubwa sana kuiangusha tawala ya Goryeo akishirikiana na jung do jeon (sambong).
mpaka sasa yang se jong na woo do hwan ndio wamethibitisha ushiriki wao ndani ya drama hii.

huyu ahjussi msamiati wa likizo kwenye ubongo wake hautambulikani kabisa, hongera Khantwe kwa kupata ahjussi wa ukweli.
mwanamme lazima apambane bila ya kuchoka kwa ajili ya kumpa ahueni mwenza wake, sisi wengine tukipata 30000 kwa siku tunapumzika huku tukijipa majina ya ovyo kama DON wakati Jang hyuk anamiliki mjengo wa kibiashara eneo nyeti kabisa lakini bado anafanya kazi kama kichaa.
🙂🙂🙂😱😱
Habari hii iwafikie wapinzani wote wa khantwe, ngoja niwakumbuke kama bado wapo na huyu ahjussi.
scalethat + talnam

  1. Yang Se Jong Confirmed To Appear In Upcoming Historical Drama
  2. Woo Do Hwan Confirmed To Join Yang Se Jong In New Drama
  3. AOA’s Seolhyun In Talks For New Drama With Yang Se Jong And Woo Do Hwan
 
Aigoo aigoo ndio maana mi nampendaga, hakuna mwanamke asiyependa mwanaume mpambanaji aisee. Oppa, fighting [emoji123][emoji123]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aigoo aigoo ndio maana mi nampendaga, hakuna mwanamke asiyependa mwanaume mpambanaji aisee. Oppa, fighting [emoji123][emoji123]

Sent using Jamii Forums mobile app
awe na muda angalau wa kukutembeza maeneo ya seoul, jeju, song do, busan n.k
mwanamme kila siku anaonekana kwenye TV huoni wapinzani wako watakupindua wakimuona amependeza kwa makeup au unajiamini kuliko bwana yule wa Auditing.
shauri yako.
 
awe na muda angalau wa kukutembeza maeneo ya seoul, jeju, song do, busan n.k
mwanamme kila siku anaonekana kwenye TV huoni wapinzani wako watakupindua wakimuona amependeza kwa makeup au unajiamini kuliko bwana yule wa Auditing.
shauri yako.
Bwana eeh najiamini yuko bize na kazi atachepuka saa ngapi? Maisha yake ni kazi na mimi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi kuna yeyote anayechukia humu ndani pindi ninapokuja na stori za sky castle drama?
kama yupo basi anyanyue mguu juu kama majeruhi wa shambulio la aibu.
sielewi kwa nini kuna watu bado wanateseka mpaka muda huu kwa kufuatilia drama zisizo na ladha nzuri kuliko juisi ya mgonjwa wa kisukari, wako wapi team mr sunshine, team goblin, team reply 1988 n.k
kimyaaaaaaa kuliko panga boy za sheikh maguvu method.

tulianza na 1.7% lakini episode ya juzi tumegonga hadi 21% kwa kuangaliwa mji wa seoul na tumegonga 19% kwa kuangaliwa nchi nzima na bado wiki hii huenda tutagonga hadi 23%
wanaochukia watapata tabu sana.​
kuna watu humu ndani wanahangaika na ahjussi uchwara, ngoja na mimi nihangaike na ahjumma.
si nasikia kulipiza kisasi ni sahihi kama hutovunja mipaka?

hivi ni nani asiyetaka mwanawe asome UDSM wakati ni kilaza kama mimi?
hivi ni nani asiyetaka aonekane ana fedha wakati ni empty kama mimi?
hivi ni nani asiyetaka aonekanwe ni Great Thinker hali yakuwa ubongo wake ni kama wa kuku?
sote tunadanganyaaaaaaa ili tupewe heshima na wenzetu.
  1. “SKY Castle” Sets New JTBC Record As Ratings Soar To All-Time High
  2. “SKY Castle” Cast To Go On Reward Vacation
  3. “SKY Castle” Responds To Script Leak And Rumors Regarding Final Episode
  4. “SKY Castle” Characters That You Would Not Want As Part Of Your Family
  5. “SKY Castle” Tops List Of Buzzworthy Dramas For 5th Week In A Row
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…