Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!


Aiseeee wewe jamaa ni noma sana [emoji1487][emoji1487][emoji1487]
Kwa wengine wasiojua hizi mambo zetu za Korea mimi huwa naonekana najuaaaa ila hapa najiona kabisa sijui.

Sasa jana baada ya kumaliza kuangalia King Gwanggaeto nikajikuta namuuliza swali mtu ambaye hajui mambo ya Korea baada ya kugundua Houyan ndio Beijing ya leo China.

Swali nililomuuliza ni kwamba “Ni wazi Korea, Japan na China zilikuwa ktk muunganiko. Ilikuwaje zimejitenga kama ilivyo leo hii?”

Nimengalia drama nyingi ila sio ktk mtiririko, na ili upate kulifahamu hili vyema basi uweze kuunganisha drama hizo ktk mtiririko...

Naomba unipe mtiririko mzuri/sahihi wa hizo drama ambazo zinaelezea/kuonesha mgawanyiko huo.
Hata ukielezea kwa maandishi pamoja na hizo drama itakuwa vizuri zaidi, asante.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Nilikuwa nakumbuka hiyo ‘Sambong’ ila sikuwa na uhakika sana, asante.

Ujue Six flying dragons nimekuona mara nyingi ukiisifia hapa ila huwa hainivutii sababu imekaa kichina china hivi, na mimi ukitaka kunichefua niletee drama ya kichina, sizipendi kabisa maana zina mambo ya kichawi ambayo siyaamini, sipendi drama za mambo ya kufikirika.

Vipi ktk hii Sambong na six flying dragons nianze na ipi? Nimewahi kuona ukisema kuna kama muendelezo fulani baina ya hizo drama mbili.

Hiyo The Great Seer ipo ktk list yangu kitambo tu, Jin Jin Hee yupo tena? Hiyo ni lazima [emoji12]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Tunatofautiana ktk hili. Mimi hii miziki ya Kikorea ambayo naipenda sana ni mpaka niusikie ktk drama as OST ndio niutafute na kuudownload kabisa.

Ila hivihivi sifuatilii kabisa miziki yao. Huwezi amini wale madogo waliotikisa Dunia ktk charts za Billboard sijui wimbo wao hata mmoja! Kila mara huwa nasema nitafuatilia ila nasahau, mwisho nimeona niache tu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwani Siku Izi Hulali!??
 
Umeona Jinsi Territory ya Gogryeo ilivyokuwa Kubwa Chini ya Mfalme Gwanggaetto the Great, Ilikuwa inafika Korea Kusini,Korea Kaskazini(Chimbuko lake),China,Mongolia na Urusi. Ramani ya Sasa ya Korea ni ndogo sababu ya watu wapuuuzi toka Shilla waliungana na Tang dynasty ( China) wakaiangusha Gogryeo,Baekje na Gaya. Katika Suala la Kugawana Territory Nchi inayochukua eneo kubwa ni ile yenye jeshi Imara na iliyoombwa msaada hivyo Tang(China) wakachukua Eneo kubwa Shilla wakaachiwa hako karamani Baadae Shilla dynasty inaangushwa Ikaja Goryeo,Joseon,Korea Empire kisha North na South.

Humo kwenye hiyo King Gwanggaetto kuna wanatumia akili sana Ukimtoa the North Gost( Dam doek) kuna1 Murong Un na 2 Ha muji( the Military Advisor) yupi aliyekukosha kwa weledi wake?!, miye Ha Muji.

Nakumbuka tulianza wote Yi san miye nishaimaliza,Nikaja Jewel in the Palace tayari,nikaanza Joseon Gunman tayari, Emperor of the Sea tayari,Nikaenda kwa Princess Jammyung Go tayari na sasa niko likizo maana nilikuwa natazama episode 6-7 kwa siku nilikuwa nalewa, japo naenda mdogo mdogo Jang yeong Sil nafikiria Kuianza Sambong na the Great seer.
 
Vipi ktk hii Sambong na six flying dragons nianze na ipi? Nimewahi kuona ukisema kuna kama muendelezo fulani baina ya hizo drama mbili.
  1. jeong do jeon drama ni project ya mwaka 2014 kupitia shirika la KBS na six flying dragons ni project ya mwaka 2015 kupitia shirika la SBS na chakuvutia zaidi zote zimejengwa na takribani episode 50.
  2. zote zinazungumzia harakati za mwishoni za kuanguka tawala iliojaa rushwa ya goryeo na kuanzishwa joseon dynasty.
  3. six flying dragons kwa kiasi kikubwa imejaribu kuonyesha umuhimu wa lee bang won kwenye hizi harakati za kuiangusha goryeo akishirikiana na wanadamu wengine watano ambao ni lee seong gye, jung do jeon (sambong), lee bang ji, muhyul, na mwanadada boon yi.
  4. ukija kwenye jung do jeon ndio imeelezea kiuazi harakati za huyu jamaa kutoka kuwa mwanasiasa wa chini mpaka kuitikisa goryeo, ndani ya jung do jeon hutokuta uhusika wa lee bang ji, boon yi na muhyul, just ni wahusika wasiokuwa na rekodi yoyote muhimu kwenye harakati za kuiangusha goryeo kihistoria.
  5. kama ilivyokuwa kwa jing birok na admiral yi soon shin drama na hapa ndio hivyo hivyo ni marejeo ya matukio kwa kiasi kikubwa na kwa kuwa project ya jung do jeon ndio ya mwanzo kivyovyote itakuwa ni bora hata kibajeti.
  6. wengi wao wanaovutiwa na six flying dragons ni wale wapenzi wa mapigano lakini kwa wale wapenzi wa siasa za kibabe nakushauri itafute jung do jeon drama.
 
kutoka mwaka 391 chini ya go damdeok hadi 668 chini ya bojang ilipoangushwa goguryeo ni miaka takribani 270 imepita, uhusiano wa shilla na Tang ulianza miaka 660 hivyo ukisema shilla ndio imechangia goguryeo/ korea kupoteza eneo kubwa sidhani kama ni sahihi kiupande fulani.
 

Nimeiona Chief
Damdeok nimemkubali sana hasa kwa kupendelea kwake kusikiliza maoni ya washauri wake tofauti na wafalme wengine ambao wako kama ‘jiwe’ letu.

Hakuna shaka Ha Muji ndio alikuwa genius kuliko hao wengine wote sababu mipango yake asilimia kubwa ilifanikiwa. Director amefanya kazi nzuri sana kumteua mhusika wa Ha Muji, amevaa uhusika kwa namna iliyovutia sana.
Jana machozi yamenitoka alipouawa ktk episode 89, ilikuwa episode chungu sana kwangu.

Watu ambao niliumia kwa vifo vyao ktk series hii ni Sagal Hyeon na Ha Muji.

Vilevile nimevutiwa sana na swordsmanship ya Damdeok, vile anavyorusha sword na kuidaka katikati ya mapambano alinivutia.
Mtu niliyekubali mapigo yake humo ni Sagal Hyeon, jamaa alikuwa anapigana kitaalam sana. Alinikumbusha Gukseon Munno wa kwenye Queen Seondeok.

Yi San nachechemea nayo kama unavyoenda mdogomdogo na Jang Yeong Sil, na hizo zote ambazo umeziangalia ikiwemo hiyo Jang Yeong Sil nimeshaziona zote.
Utanipiga gape ukianza kuangalia Sambong na Great Seer pekee.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Kuna siku uliwahi kusema ktk King Gwanggaeto kuna mapungufu mengi ikiwemo kutokuoneshwa uhalisia wa maisha ya wananchi wake kwa nyakati zote alizokuwa vitani maana drama yote imetawaliwa na vita mwanzo mwisho...

Well, nafikiri walitumia eneo lile la bar pamoja na wale jamaa wafua vyuma (iron smiths) kama kuelezea hilo. Nadhani unakumbuka kuwa majadiliano mengi ya ‘kijiwe’ kile yalibase kwenye namna ambavyo maisha yanavyoendelea mitaani.

Ile drama ina matukio mengi sana, mengine Director amejaribu kuyaondoa ili kupunguza wingi wa episodes kama harusi n.k


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
yes niliwahi kusoma taarifa kupitia special thread ya soompi kwa mujibu wa KBS ilitakiwa kuwa na episode 100 lakini ikapunguzwa hadi 92.
 
maisha yote muathirika wa vita vya mara kwa mara ni fukara, na kwa mfumo wa korea ulivyokuwa ni walalahoi ndio walimaji wakuu huku ujira wao ni mdogo.

ardhi ya goguryeo kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni ya milima na baridi kali hivyo basi kilimo nacho ilikuwa ni shida, kivyovyote licha ya goguryeo kujitanua sidhani kama wananchi walikuwa na maisha bora ya kujivunia.
 
halafu mkuu si kila muda unatakiwa uonyeshe ubabe wako mbele ya jamii, jaribu kujishusha zaidi na zaidi kwa dhumuni la kufikia lengo lako na hiyo ndio silaha walioitumia shilla.

Kim Chun-Chu alikuwa ni zaidi ya mwanadiplomasia anayejua kutumia ulimi wake ipasavyo kwa dhumuni la kuyafikia malengo yake, alishaona kwa nguvu ya shilla hawakuwa na uwezo wa kusimama na goguryeo na hata Baekje hivyo solution ni bora tuwe mbwa wa Tang china kuliko kuvamiwa na ndugu zetu.

hatimaye alifanikiwa malengo yake kwa sababu baekje iliangushwa, ikafuata goguryeo baadae shilla na tang wakageukiana na hatimaye tang akachapwa kwa ushirikiano wa wanajeshi waliokuwa wa goguryeo, baekje na shilla.

shilla wakafanikiwa kuziunganisha kingdom 3 kwa mara ya kwanza kwenye historia, ndipo takribani miaka mingi kupita ikawa ni zamu ya goryeo kuziunganssha tena kingdom 3 baada ya shilla kuanguka pamoja na balhae kuchapwa na KHITAN.
 

Ni kweli kabisa, zaidi ya amani na imani iliyotokana na kuwa na mfalme ambaye ni mwamba wa vita ni wazi maisha yalikuwa ya taabu.

Hata wafanyabiashara wakubwa na wakulima wakubwa nadhani nao walionja makali ya vita maana lazima walikuwa wanatoa vipande na rations kulingana na namna wanavyozalisha.

Hapa nawaza tu ndio sisi tungekuwa ktk nchi ile ya Goryeo yenye milima na baridi kali + vita visivyoisha kwa aina ya viongozi wetu sijui ingekuwaje! Mungu Mkubwa [emoji1488][emoji1488][emoji1487]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
drama zinazozungumzia taifa la joseon zipo nyingi sana dada yangu kwa makadirio zinafika 100, kwa kuwa hatujibii mtihani wa fasihi nyengine nyingi sijaziangalia.

  1. jung do jeon + six flying dragons 🙁kuanzishwa kwa joseon kuanzia mfalme taejo hadi taejong) the greet seer sikuifuatilia kwa sababu haipo kiuhalisia wa matukio. Ni sawa na kuangalia king gwaggaeto drama baadae ukafuatilia the legend drama japokuwa zote zimemzungumzia go damdeok.
  2. the great king sejong + tree with deep roots + jang yeong sil drama:(ukiiangalia sejong the great drama basi utakuwa umeshajirahisishia kila kitu, utayafahamu maisha yake taejong na utawala wake, maisha ya sejong, maisha ya jang young sil na ushirikiano wake mkubwa na sejong katika kuifanya joseon kuwa ni nchi ya sayansi, harakati za sejong kuanzisha herufi za korea(hangul) na mengine mengi sana) + (Jang yeong sil umesema umeshaiangalia, + tree with deep roots ndani yake kuna kikundi fulani kinaitwa milbon kama nipo sahihi ambao walitaka kulipiza kisasi cha mauaji ya sambong, pia imezungumzia harakati za sejong kuanzisha hangul letter) Cha kuvutia aliyeigiza uhusika wa mfalme sejong na taejo ndani ya sejong drama ndio hao hao waliyoigiza uhusika wa sejong na taejong ndani ya jang yeong sil drama.
  3. the princess man drama: romeo and juliett kutoka korea, love story kati ya mtoto wa mfalme na kijana ambaye baba yake alihukumiwa kwa usaliti
  4. queen for seven days drama : malikia aliyekaa madarakani kwa siku saba, sijui kama itakuvutia kwa sababu ni love story kwa kiwango kikubwa inayombatana na uchoyo wa madaraka, wivu kati ya ndugu wawili.
  5. ukiangalia jingbirok + admiral yi soon shin utakuwa ushamfahamu seonjo na vita ya imjin, zipo nyengine lakini ndio hivyo hatujibii mtihani wa fasihi
  6. heo jun drama: maisha ya daktari wa mfalme seonjo na familia yake nzima aliyeitwa heo jun, mtaalamu wa tiba aliyebobea nyakati hizo.
  7. the crowned clown, goddess of fire, the kings face, hong gil dong (maisha ya gwanghae ambayo pia utayapata kwenye no 5 na no 6) hii jung yi goddess of fire inazungumzia maisha ya mwandada fulani aliekuwa ni genius kwa utengenezaji wa vyombo vya kigae huku kwetu tunaita kaure, cha ajabu wenzetu wametengeneza miaka karne ya 16 ila sisi mpaka leo tunashindwa.
  8. dong yi, yi san, haechi, jang ok jung, jackpot (maisha ya mfalme sukjong, mfalme yi san, yeong jo), ongezea warrior baek dong soo, secret door
  9. joseon gun man, mr sunshine :nyakati za mwisho wa utawala wa joseon kabla ya kutawaliwa rasmi na japan.
  10. comrade, seoul 1945 : vita ya korea
 
The main objective of an audit is to enable the auditor to report on the truth and fairness of the financial position shown by the statement of financial position, of the profit or loss shown by the income statement, statement of cash flows, statement of changes in equity and of any other information required to be disclosed in the financial statements, in accordance with an identified financial reporting framework, legislation or relevant professional board.

kwa msaada wa mr google jamani:
nimemaliza kuziangalia episde 2 za drama inayoitwa the banker, haikuwa na rate kubwa lakini ni best drama kutokana na mtiririko wake.
veterani katika ubora wao
 

Jana nimejaribu kuangalia Waikiki 2 maana sio kwa sifa mnazoimwagia hapa lakini inanisumbua, Memories of Alhambra ndio kabisaaaaa inazingua kinoma.

Naendelea kujikongoja na Yi San, ngoja nijaribu na hii maana jana nimeiona pia KissAsian ila sikushawishika japo nilimuona mzee wangu.
Ngoja niicheki inibust kuangalia drama nyingine maana nakosa hamasa.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…