Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!


Kama umegundua director ni huyohuyo ndio maana kawatumia characters wengi kutoka kwenye Jang Geum na akaendelea nao kwenye Dong Yi.
Artist Yi ana vituko sana na ile michoro yake ya magendo hahaaaaaa ila mimi namkubali yule mzee mwenye macho makubwa Uncle ake na Da Esu, mahusiano yake na yule mama wa bar huwa nacheka hata kabla hawajaongea.

Ila hakuna drama ambayo nimewahi kucheka kuzidi Queen Seondeok, Jukbang na rafiki yake Godo walijua kunipa afueni baada ya matukio mengine ya huzuni.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Hahaaaaa Jukbang sijui aliiba nini aiseeee ilikuwa balaa.
Na ile siku aliyombeba Deokman mgongoni kifua cha Deokman mgongoni mwa Jukbang kilimfanya Jukbang agundue Deokman ni mwanamke nilichekaaaaaaa, halafu akakausha kama hajajua vile.

Mkuu umenikumbusha machungu ya Bidam na Deokman, niliipenda couple yao sanaaaa. Bidam akazingua baada ya kulaghaiwa kuwa Deokman kamtumia watu wamuuwe ilhali wakati Deokman anamtuma ktk mission ile alimpa pete ambayo endapo angefanikiwa na kurudi walikuwa wafunge ndoa.
Nililia sana, sana.
Mwisho wa Bidam ni moja kati ya drama zilizouvunja moyo wangu baada ya Jumong [emoji24][emoji24].


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Chumong amepotelea wapi! Miaka inaenda sioni drama zake tena, huyu ndio amefanya nipende drama za kikorea! Popote alipo nipo

Sent using Jamii Forums mobile app

Mannnnnnnnnnn!
Kumbe kuna wapenzi wenzangu wa Song Ill Gook? Yule ndiye mfalme wangu wa Korea, kimya chake kinaniuma sana.
Nimebaki tu kumlilia instagram arudi walau na drama moja tu roho zetu zipoe.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Pale kwenye Dong yi walikuwepo wale Rafiki zake na Dong Yi kutoka Idara ya Muziki sasa walikuwa wananikosha pale watakapo-meet na mfalme na Dong yi, mfalme anawapiga pombe alafu jamaa wanaanza kutema shit, sasa yule mzee akijaribu kumzuia mwenzie asiongee pumba mbele ya Mfalme hapo ilikuwa inakuwa kasheshe, huku mfalme anaona raha.
 

Yule jamaa mrefu nae ni Comedian kimtindo, kama umewahi kuangalia City Hunter kule nako alifanya yake.

Hebu acha usinikumbushe, hakuna scene nilizokuwa nazipenda kwenye Dong Yi kama zile za Mfalme (Ji Jin Hee) na Dong Yi wakiwa kitaa na wale marafiki zake. Dong Yi alipoingia ktk palace kama concubine nilikuwa dissapointed, nilipenda zaidi walipokuwa wanakutana mitaani.

Unakumbuka siku ya kwanza kuonana Dong Yi hakujua kama yule ni mfalme? Akamkanyaga mgongoni akapanda ukuta hahaaaaa.
Na kule mitaani walipokuwa wanakunywa jamaa akamlisha mfalme ngozi ya nguruwe je?
Sasa siku walipomuona ktk palace kama mfalme ndio nilikufa kwa kucheka.

Dong Yi ni bonge la drama.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
😂😂 wote walikuwa hawa amnin kama ni yeye moja kwa moja wakajua ni mwendo wa kunyongwa tu, ila Dong Yi alipokuwa anatakiwa na Wachina katika kukimbia kwake akamuona Ofisa wa polisi kavaa kijeshi sasa hapo ndo niliamini bora kupigwa makofi kuliko kupigwa butwaa😂😂 She was surprised a lot. sasa mfalme mwenyewe hakufurahishwa na kujulikana kwake.
 
Nakumbuka jinsi walivyokuwa wanajifanya ma monk mbele Deok Man, wakampiga mchana kweupeeee!!, Ila walojuta walipoingia angaza Mishil.😁View attachment 1065531
Lee Moon Sik, Huyo Mzee Namkubali Sana Kwa Comedy Zake. Huyo Jamaa Ni Comedian In Real Sense! Alicheza Pia Katika Empress Ki. Kuna Kipindi Alijifanya Monk Kisha Akazamia Katika Ngome Ya Maadui Ili Kwenda Kuwalaghai. Kiongozi Wa Hiyo Ngome Alikuwa Mwanamke, Alijulikana Kama Batoru Ambaye Baadaye Alikuja Ku-Join Forces Na Mfalme Wa Goryeo (Wang Yoo).
 
Hahaha mzee mzinguaji huo na unaweza kumkuta kakaa mkao wa mtu wa Busara, na ukaamini kweli kuwa amejawa na hekma.
 
Jukbang Pamoja Na Kim Yusin Walishagundua Toka Kitambo Kuwa Deokman Alikuwa Mwanamke Ila Waliuchuna Tu, Tena Kim Yusin Alijuaga Mapema Sana Licha Ya Hivyo Akawa Anampa Deokman Mazoezi Magumu Ndani Ya Kikundi Chao. Ila Ni Afadhali Hiyo Siri Haikuvuja Kwenda Makundi Mengine Ambayo Ni Mahasimu Wao, Ingekuwa Balaa!

Kweli, Mwisho Wa Bidam Ulikuwa Mbaya Sana. Wafuasi Wanaweza Kuwa Chanzo Kikubwa Cha Kumjenga Mtu Ama Kumuangusha. Mtihani Kama Huu Uliwahi Kumkuta Kim Yusin Akafanikiwa Kuchomoka Ila Kwa Upande Wa Bidam Ilishindikana Kujinasua Katika Mtego Huu Mpaka Akaingia Kwenye Uasi Ambao Kiukweli Ilikuwa Ni Huzuni Kubwa.

Ingawa Wafuasi Wa Bidam Walifanikiwa Kumalizwa Baada Ya Kushiriki Katika Ule Uasi Lakini Inasemekana Baadhi Yao Walibaki Na Wame-Extend Kikundi Chao Mpaka Miaka Zaidi Ya 700 Baadaye Kipindi Cha Kuanzishwa Kwa Joseon. Hichi Kikundi Kipo Kwenye Drama Ya Six Flying Dragons Ambacho Kilikuwa Kikihusika Kwenye Mission Mbalimbali Za Mauaji Ya Watu Mashuhuri Na Kui-Control Serikali Behind The Scenes.
 
Hichi Kikundi Kipo Kwenye Drama Ya Six Flying Dragons Ambacho Kilikuwa Kikihusika Kwenye Mission Mbalimbali Za Mauaji Ya Watu Mashuhuri Na Kui-Control Serikali Behind The Scenes.
Kikundi kipi unachozungumzia?! Wale kina Gil Taemi na Gil Sumi, au wale ma- monk or ndugu zake na Chuk sagwa.?!
 
Kuna drama yoyote iliyokamilika inanifaa kuangalia katika kipindi hiki??? Suggestion please
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…