Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Police Reportedly Collect Evidence Of Park Yoochun’s Alleged Drug Use + Ban Him From Leaving The Country

dah! ukisikia utajiri wa mikosi na umasikini wa bahati unaotokana na matendo yako ndio huu unaomkumba park yoo chun (actor na muimbaji).
huyu bwana siku za nyuma alijikuta akifikishwa kwa pilato kwa kosa la kuwafanyia vitendo vya kinyanyasaji wasichana lakini baada ya vita ya muda mrefu hatimaye mahakama ikatoa maamuzi ya kutokuwa na hatia kwa park yoo chun huku baadhi ya walalamikaji wakihukumiwa kifungo gerezani kwa madai ya uongo.

ishu iko hivi jamaa alikuwa na mahusiano na mwanadada anayeitwa hwang ha na ambaye hivi karibuni alikutwa na hatia ya kutumia madawa aina ya Philopon (a form of methamphetamine) tokea mwaka 2015.

binti baada ya kufanyiwa mahojiano kituo cha polisi akadai ya kwamba rafiki yake wa karibu wa kiume ndiye aliyemshawishi na kumtishia kutumia dawa hizo za philopon., namnukuu bidada hwang ha na
I wanted to stop using Philopon, but I continued to do so because ‘A’ pressured me into it .
ndipo polisi wakaanza kumtafuta huyo mr A ndio nani?​

mnamo April 10 muheshimiwa park yoo chun akafanya mkutano na waandishi wa habari kwa dhumuni la kukanusha madai ya aliyekuwa mchumba wake ya kwamba yeye ndio chanzo cha mwanadada kutumia madawa, alizungumza mambo mengi sana ya kujitetea na nakumbuka niliweka taarifa yake kwa muda lakini ilikuwa kwa lugha ya kiingereza.

baadhi ya maneno aliyoyazungumza bwana park
I have never used drugs let alone suggest it. I criticize myself every day as I endure pain and work hard to be able to act again and have activities. Therefore, I cannot even imagine that I would think of using drugs, which would make all of my efforts come to nothing. I will earnestly go to the police station and be investigated.”

sasa leo jeshi la polisi limefanikiwa kugundua ushahidi wenye kuonyesha jamaa alitumia madawa ambayo binafsi amekataa hajawahi kuyatumia na wameamua kuwasilisha ofisi ya muendesha mashtaka ushahidi huo ili kuzidi kufanya uchunguzi hii ni kwa mujibu wa MBC kupitia kipindi cha Newsdesk.

kwa mujibu wa shirika la SBS ni kwamba leo hii polisi pia wameamua kumpiga marufuku park yoo chun asitoke nje ya nchi.

3 days
rooftop prince
i miss you
the girl who see smell
sungkyunwan scandal
miss ripley


wenzangu mumeona drama ngapi za jamaa kati ya hizo hapo juu?
binafsi nimeona 3 days drama si mnajua hatujibii mitihani hizi drama

 
Kwa nini ulianzia njiani? Ila kiukweli kule nyuma walivyuta sana muda

Sent using Jamii Forums mobile app
ndio nilianza njiani halafu sikuwa na mzuka sana na queen seondeok kwa sababu nilikwishafahamu matukio yanayowahusu wahusika wakuu.

  1. nilishajua mwisho wa bidam utakuwaje kwa sababu hata ukiangalia drama inayoitwa dream of emperor (kings dream) bidam anakufa kwa usaliti unaotokanwa zaidi na tamaa ya madaraka.
  2. baadae kim chunchu anakuwa mfalme baada ya kifo cha queen Jindeok , fahamu baada ya kufa queen seondeok alitawala mwanadada mwengine aliitwa queen jindeok lakini hakuwa na undugu wa damu na queen seondeok.
  3. kwenye kings dream yumo malikia anaitwa Queen Seungman ni mbishi kuliko jiwe la msingi na alikuwa anashirikiana na bidam.
  4. kim chunchu ambaye uhusika wake ameigiza yoo seung ho ndani ya queen seondeok baadae anapewa heshima ya taejo muyeool, ndiye chanzo cha kuwakaribisha Tang china chini ya mfalme wao emperor taezong ndani ya three kingdom, kwenye kings dream uhusika wake ameigiza choi soo jong ahjusii akiwa na miaka 50 kama umeangalia emperor of the sea drama itakuwa unamfahamu.
  5. kim hunchu anafariki kabla ya goguryeo kuanguka na hatimaye kampeni ya kuingusha goguryeo inaongozwa na kim yu shin akipata amri ya mfalme ambaye ni mtoto wa kim chunchu
  6. kim chunchu anamuona dada yake kim yusin.
  7. kim yusin anaongoza vita ngumu dhidi ya baekje ikiongozwa na general gye baek na hatimaye baekje inadondoka tawala yake
  8. kim chunchu anafariki mwanzo akiwa na miaka 57
  9. kim yusin anafariki dunia akiwa na miaka 78
 
Kuna Baadhi Ya Waigizaji Ambao Wanapendezea Sana Kuigiza Bad Guys Ama Villains, Conmen, Watu Makatili n.k. Na Miongoni Mwa Hao Ni Huyu Mzee-Kijana Jung Woong-In.

Unaweza Kuta Kuna Projects Ambazo Unakuta Muigizaji Anaigiza Kama Villain Lakini Hafananii Kabisa Na Kile Anachoigiza Na Anakuwa Kama Amelazimika Tu Kuigiza Uhusika Huo Kutokana Na Sababu Mbalimbali.

Katika Projects Nyingi Alizohusika Huyu Jamaa Na Nyingine Zijazo, Kwa Maoni Yangu Ana-Fit Sana Akiigiza Kama Villain Kutokana Na Muonekano Na Uwezo Wake Wa Kuuvaa Uhusika Wa Namna Hizo.


 
hizi drama mashirika ya SBS, KBS pamoja na MBC tokea ulipoanza mgogoro wao wa kimaslahi kati ya korea na china wamekuwa wakiweka matangazo kila baada ya nusu saa ya kipindi tofauti na drama za zamani.

halafu sheria za korea haziruhusu kuweka matangazo katikati ya kipindi ndio maana viongozi wa mashirika hayo matatu wakamua kuja na mpango wa 30 minutes per episode ili waweze kuweka matangazo ya biashara wapunguze gape la gharama, si unajua wafanyabiashara wote duniani wanaangalia soko la china sasa jamaa kaamua kuwaekea ngumu na inasemekana ishu ilikuwa ni THAAD.
sijui kama kwa sasa mahusiano kati yao yamesharudi kama mwanzoni hata sielewi.

ukiniambia upo episode ya 11, 12 mimi naelewa kiuhalisia upo episode ya 6, ndio maana nikakwambia unisimulie si kwamba nimemaanisha unisimulie episode ya 5, 6 ambazo ni sawa na episode ya 3 kiuhalsia.
  1. https://www.soompi.com/article/9532...roadcasters-considering-60-minute-rule-dramas
  2. https://www.koreaboo.com/news/china-begins-lift-ban-hallyu-content-country/
 
Rooftop Prince, Sungkyunkwan Scandal
 
Aisee kumbe uko kama mimi, nikishajua drama inaishaje huwa siangalii hiyo drama labda nikose kabisa ya kuangalia napo iwe iko downloaded, siwezi kuunguza mb zangu kwenye drama ambayo najua inaishaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye Queen Seondok alitisha, Faith kama sikosei
 
Yeah anafit sana ingawa nimeona drama mbili tu ambazo ni Empress Ki na hii ya Deokman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miye niliitazama six flying dragon na nilishasoma history inasemaje kuhusu uanzishwaji wa Joseon lakn bado naifuatilia yenye visa sawa na hivyo, at the same time nimekwisha iona Jang yeong sil inayoelezea kisa kimoja kwa asilimia 70% na the Great king sejong.
 

Ohoooooooo sasa nimekuelewa vizuri. Wewe unafaa kuwa mwalimu, unaelezea vizuri sana.
Bado sijaiona, naangalia upangwaji wa magroup AFCON [emoji4]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Huu moto wa Sambong na The Great King Sejong ni hatari, wee Bidam tulia kwanza nimalize Assignment zangu muhimu.

Hebu niacheni jamani, mnanipa wakati mgumu natamani ningeweza kuzuia usingizi niangalie zoteeeeee [emoji24][emoji24][emoji24]
Nikimaliza The Great Seer inafuata Fiery Priest, Sambong ndio nyingine.
Nihurumieni kidogo.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hahahaha hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…