Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

mm napenda zapolini km fraternity nk km kuna movie mpya ya poli km fraternity naomba nipatiwe jina niitafute
Sword fraternity- hawa ni watafsiri toka Arusha ndiyo wanabadili majina ya hizi series ili waonekane wao ndiyo wameanza kuzitafsiri, Dong yi niliitazama kwa mara ya kwanza 2011 ilikuwa imetiwa maneno ya kiswahili na Dj mark( Dj Black G machine toka acheche), 2018 nikairudia kwenye Dramacool, mwezi 12 wakati narudi likizo nikakuta my sisy anayo kwenye flash.
Inaitwa DONG YI instead of Sword fraternity.
Ingia Dramacool utaipata.
 
Assignment nyingine hii hivi the Priest nitaitazama lini?! Maana hii ishaanza kujipendekeza kwangu, ila mpka ni malizane na Jeong Do-Jeon na Great King Sejong.
 
mutatufanya wengine tuikimbie hii thread, kiingilishi kinaelekea kutushinda mpaka muda huu unadhani tutakiweza kilugha cha wala tambi masaa 24 kama mbuzi na majani?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Mimi kusema ukweli drama ya Kikorea ikishakuwa na mambo ya kizungu/uzungu ndani yake huwa sifurahii.
Mimi ni mnazi wa Korea haswaaaa, huwa sitaki uzungu uzungu kwenye ukorea.
Naelewa drama hii inaelezea yaliyotokea wakati huo wa mwisho wa Joseon wakati ‘mabadiliko’ ya kiwestern yanaingia kwao lakini sijavutiwa na hilo japo sio mbaya na nitaimaliza.

Juzi ulipoleta pendekezo jipya la drama nyingine ya My Mister nilijaribu kuiangalia ajabu nimeipenda zaidi, imenivutia kisa chake na hata casts wake nimewaelewa sana.

Ila wewe nae? Mwaka jana ulisema drama bora ya mwaka ule (kama nipo sahihi) ndio hiyo Mr. Sunshine ila juzi umesema hii My Mister ndio drama bora zaidi ya mwaka jana.
 

The great seer ni bonge la drama, kisa chake ni kikali na waigizaji wamefanya vizuri sana.
Sijui kwanini haikuwa drama kubwa labda sababu kipindi kile kulikuwa na drama nyingine kali kama The Great King Gwanggaeto.
 
The great seer ni bonge la drama, kisa chake ni kikali na waigizaji wamefanya vizuri sana.
Sijui kwanini haikuwa drama kubwa labda sababu kipindi kile kulikuwa na drama nyingine kali kama The Great King Gwanggaeto.
Drama kali zilianza kuadimika 2015 kija mbele kipindi the seer inatoka kulikuwa na vyuma vikali ndiyo maana sikuwahi kuitazama, maana nyakati hizo kulikuwa na drama kama Bridal Mask n.k zilikuwa drama zilizopikika na zikaiva.nakumbuka nilikuwa nimemaliza kuitazama King Gwanggaeto, Dae Joyong, Gaeuchoggo, Military official , the Comrade( Korean Civil war), na Empress Chunchu, kichwa changu kilikuwa kimeathirika na drama za kivita, sasa hizi ambazo zilikuwa na story sana nilikuwa sizifuatilii sana.
Mwisho tu Great seer ilitoka kwenye era za dhahabu.
 

Wale waandishi na directors sijui walifia wapi jamani! Dae Joyoung niliishia kama episode ya 40, nitaitafuta niicheki upya.
Tatizo ni ndefu sana na yenyewe 🤦🏻‍♀️

Ila drama za kivita za Korea ndio mambo yote, hizi nyingine tunaangalia tu maana kuangalia sana historical huwa nachoka sometimes.
 
Umeeahi kuiona Empress Chunchu?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…