Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

mm napenda zapolini km fraternity nk km kuna movie mpya ya poli km fraternity naomba nipatiwe jina niitafute
Sword fraternity- hawa ni watafsiri toka Arusha ndiyo wanabadili majina ya hizi series ili waonekane wao ndiyo wameanza kuzitafsiri, Dong yi niliitazama kwa mara ya kwanza 2011 ilikuwa imetiwa maneno ya kiswahili na Dj mark( Dj Black G machine toka acheche), 2018 nikairudia kwenye Dramacool, mwezi 12 wakati narudi likizo nikakuta my sisy anayo kwenye flash.
Inaitwa DONG YI instead of Sword fraternity.
Ingia Dramacool utaipata.
 
Screenshot_2019-04-29-09-27-22.png
List ya Philosopher wa Korea,kuna majina hapo si mageni kwenu, Jeong Mongju(Poeun) na Jeong Dojeon( Sambong)
 
SHIN DON
Kuna mdau yeyote humu ndani aliyewahi kuiangalia hii drama ya mwaka 2005 kupitia kituo cha MBC?
huyu jamaa alikuwa ni MONK nyakati zile za utawala wa GORYEO, uhusika wake pia umeelezewa kupitia drama inayoitwa THE GREAT SEER ya mwaka 2012 kupitia shirika la SBS.
sijawahi kuiona hii drama lakini kwa mujibu wa mwanadada Nifah ameipa alama 9/10.

kwa mujibu wa summary kupitia tovuti ya Asian wiki:
miaka ya mwishoni ya tawala ya goryeo aliwahi kuwepo mfalme aliyepewa jina la Gongmin ambaye kwa mujibu wa historia aliwahi kuchukuliwa mateka nchini YUAN kwa takribani miaka 10, YUAN ni taifa lilioanzishwa na watu wa mongolia ambao waliwatawala goryeo kwa miaka takribani 80 baada ya goryeo (korea) kukubali mpango wa kuachana na vita iliodumu kwa miaka takribani 30.

mfalme gongmin aliporudi nchini kwao alitaka kubadilisha mfumo mzima wa uendeshaji wa taifa la goryeo, aliamua kuchukua maamuzi hayo kwa dhumuni la kuondoa mfumo mbovu wa uendeshaji wa nchi ambao ulikwisha ota mizizi hususani kwa baadhi ya koo ambazo zilitumia vibaya nguvu zao za kimadaraka ( kwa mfano ukoo wa empress ki).

Shindon alikuwa ni buddhist priest aliyekuwa na urafiki wa karibu sana na mfalme gongmin pamoja na princess noguk kutoka Yuan. Huyu shindon alifikia hatua ya kuwa na nguvu kubwa sana ya kimaamuzi ndani ya nchi ya goryeo na nguvu hii aliipata kutokana na ukaribu wake na mfalme gongmin.

je ni kipi kilichopelekea shin don na mfalme gongmin watofautiane kimtazamo hali iliopelekea wawili hao wawe zaidi ya maadui?
je shin don alikuwa ni mwanamapinduzi wa ukweli aliyeumizwa na dhiki wanazokumbana nazo wananchi wa kipato chini?
au shin don alikuwa ni muhubiri tapeli aliyeutumia zaidi muamvuli wa kidini kwa dhumuni la kuyafikia malengo yake?

dakika 30 za mwanzo za hii drama imejaribu kuonyesha moja kati ya suala lililopelekea sintofahamu kati ya shin don na mfalme gongmin, baada ya kifo cha princess noguk mfalme alitaka kujenga shrine kubwa ndani ya nchi yake kwa lengo la kumuenzi mke wake lakini shin don akakataa mpango huo

empress ki drama nilishia ep 11 hivyo basi kupitia drama hii nitaweza kufahamu maisha ya huyu mwanamama, nimeangalia episode 2 za mwanzo za hii drama ya shin don muda huu nimeona jinsi gani ndugu zake empress ki wanavyoyatumia vibaya madaraka yao ndani ya goryeo, nimenusa harufu ya vita kali hapo baadae kati ya anti mongolia dhidi ya pro mongolia.

ina maana baadhi ya watu mashuhuri kama vile yi seong gye, choi young, jung do jeon a.ka.a sambong, lee in im, jeong moong jo, shin don na wengineo wote hawa walikutana nyakati moja, hmmmmmmm inaonekana ikulu ilikuwa sehemu moja ngumu sana nyakati hizo.
View attachment 1084182
  1. https://www2.ondramanice.tv/drama/shin-don-detail
Assignment nyingine hii hivi the Priest nitaitazama lini?! Maana hii ishaanza kujipendekeza kwangu, ila mpka ni malizane na Jeong Do-Jeon na Great King Sejong.
 
mutatufanya wengine tuikimbie hii thread, kiingilishi kinaelekea kutushinda mpaka muda huu unadhani tutakiweza kilugha cha wala tambi masaa 24 kama mbuzi na majani?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
sijawahi kukuuliza hili swali.
kipi hakijakuvutia ndani ya MR SUNSHINE drama?
Numbisa aliwahi kulalamika humu ndani amepoteza bando lake na sababu kubwa hakubahatika kushuhudia kiss scene muda wote alipoiangalia hii drama.

muandishi kim eun seok amekukera?
au eugene choi amekukera?
simba wa kike anayeng'ata pia amekukera, namkusudia go aesin.
kudo hina pia amekukera?
yule mvaaji madeera( madeepa) kama mwanamke wa kihindi pia amekukera, namkusudia goo dong mae?
vipi kuhusiana na lee wanik pia amekukera?
right army hawajakufurahisha?
ito hirobumi na undezi wake pia amekukera (waziri mkuu wa japan) after edo period au Tokugawa period.
takeshi mori
amekukera?

niliipenda ile drama kwa sababu nilifanikiwa kuona nguvu halisi ya jinsia ya kike mule ndani kuna nukuu fulani inadai ya kwamba:
mwanamke ni kama majani ya chai huwezi kujua nguvu yake mpaka uyachanganye kwenye maji ya moto.

Ae Shin
alikuwa ni mwanamke mkatili sana mule ndani, kwa kuwa anafahamu fika eugene choi alikuwa anampenda kuliko anavyoupenda mwili wake basi alikuwa anamwendesha kama amemroga kwa babu wa Tanga, eugene hakuwa na utofauti na wanaume wa Dar.

Aeshin : nipo tayari twende pamoja America
eugene choi: angalau si ungeliniambia unanipenda na upo tayari kuwa na mimi kimahusiano, laiti kama ningeliyasikia maneno hayo matamu japokuwa ni ya uwongo kutoka kwenye kinywa chako yangelinifanya nizidi kuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yako.
View attachment 1084220

Mimi kusema ukweli drama ya Kikorea ikishakuwa na mambo ya kizungu/uzungu ndani yake huwa sifurahii.
Mimi ni mnazi wa Korea haswaaaa, huwa sitaki uzungu uzungu kwenye ukorea.
Naelewa drama hii inaelezea yaliyotokea wakati huo wa mwisho wa Joseon wakati ‘mabadiliko’ ya kiwestern yanaingia kwao lakini sijavutiwa na hilo japo sio mbaya na nitaimaliza.

Juzi ulipoleta pendekezo jipya la drama nyingine ya My Mister nilijaribu kuiangalia ajabu nimeipenda zaidi, imenivutia kisa chake na hata casts wake nimewaelewa sana.

Ila wewe nae? Mwaka jana ulisema drama bora ya mwaka ule (kama nipo sahihi) ndio hiyo Mr. Sunshine ila juzi umesema hii My Mister ndio drama bora zaidi ya mwaka jana.
 
SHIN DON
Kuna mdau yeyote humu ndani aliyewahi kuiangalia hii drama ya mwaka 2005 kupitia kituo cha MBC?
huyu jamaa alikuwa ni MONK nyakati zile za utawala wa GORYEO, uhusika wake pia umeelezewa kupitia drama inayoitwa THE GREAT SEER ya mwaka 2012 kupitia shirika la SBS.
sijawahi kuiona hii drama lakini kwa mujibu wa mwanadada Nifah ameipa alama 9/10.

kwa mujibu wa summary kupitia tovuti ya Asian wiki:
miaka ya mwishoni ya tawala ya goryeo aliwahi kuwepo mfalme aliyepewa jina la Gongmin ambaye kwa mujibu wa historia aliwahi kuchukuliwa mateka nchini YUAN kwa takribani miaka 10, YUAN ni taifa lilioanzishwa na watu wa mongolia ambao waliwatawala goryeo kwa miaka takribani 80 baada ya goryeo (korea) kukubali mpango wa kuachana na vita iliodumu kwa miaka takribani 30.

mfalme gongmin aliporudi nchini kwao alitaka kubadilisha mfumo mzima wa uendeshaji wa taifa la goryeo, aliamua kuchukua maamuzi hayo kwa dhumuni la kuondoa mfumo mbovu wa uendeshaji wa nchi ambao ulikwisha ota mizizi hususani kwa baadhi ya koo ambazo zilitumia vibaya nguvu zao za kimadaraka ( kwa mfano ukoo wa empress ki).

Shindon alikuwa ni buddhist priest aliyekuwa na urafiki wa karibu sana na mfalme gongmin pamoja na princess noguk kutoka Yuan. Huyu shindon alifikia hatua ya kuwa na nguvu kubwa sana ya kimaamuzi ndani ya nchi ya goryeo na nguvu hii aliipata kutokana na ukaribu wake na mfalme gongmin.

je ni kipi kilichopelekea shin don na mfalme gongmin watofautiane kimtazamo hali iliopelekea wawili hao wawe zaidi ya maadui?
je shin don alikuwa ni mwanamapinduzi wa ukweli aliyeumizwa na dhiki wanazokumbana nazo wananchi wa kipato chini?
au shin don alikuwa ni muhubiri tapeli aliyeutumia zaidi muamvuli wa kidini kwa dhumuni la kuyafikia malengo yake?

dakika 30 za mwanzo za hii drama imejaribu kuonyesha moja kati ya suala lililopelekea sintofahamu kati ya shin don na mfalme gongmin, baada ya kifo cha princess noguk mfalme alitaka kujenga shrine kubwa ndani ya nchi yake kwa lengo la kumuenzi mke wake lakini shin don akakataa mpango huo

empress ki drama nilishia ep 11 hivyo basi kupitia drama hii nitaweza kufahamu maisha ya huyu mwanamama, nimeangalia episode 2 za mwanzo za hii drama ya shin don muda huu nimeona jinsi gani ndugu zake empress ki wanavyoyatumia vibaya madaraka yao ndani ya goryeo, nimenusa harufu ya vita kali hapo baadae kati ya anti mongolia dhidi ya pro mongolia.

ina maana baadhi ya watu mashuhuri kama vile yi seong gye, choi young, jung do jeon a.ka.a sambong, lee in im, jeong moong jo, shin don na wengineo wote hawa walikutana nyakati moja, hmmmmmmm inaonekana ikulu ilikuwa sehemu moja ngumu sana nyakati hizo.
View attachment 1084182
  1. https://www2.ondramanice.tv/drama/shin-don-detail

The great seer ni bonge la drama, kisa chake ni kikali na waigizaji wamefanya vizuri sana.
Sijui kwanini haikuwa drama kubwa labda sababu kipindi kile kulikuwa na drama nyingine kali kama The Great King Gwanggaeto.
 
Drama kali zilianza kuadimika 2015 kija mbele kipindi the seer inatoka kulikuwa na vyuma vikali ndiyo maana sikuwahi kuitazama, maana nyakati hizo kulikuwa na drama kama Bridal Mask n.k zilikuwa drama zilizopikika na zikaiva.nakumbuka nilikuwa nimemaliza kuitazama King Gwanggaeto, Dae Joyong, Gaeuchoggo, Military official , the Comrade( Korean Civil war), na Empress Chunchu, kichwa changu kilikuwa kimeathirika na drama za kivita, sasa hizi ambazo zilikuwa na story sana nilikuwa sizifuatilii sana.
Mwisho tu Great seer ilitoka kwenye era za dhahabu.
 
Wale waandishi na directors sijui walifia wapi jamani! Dae Joyoung niliishia kama episode ya 40, nitaitafuta niicheki upya.
Tatizo ni ndefu sana na yenyewe 🤦🏻‍♀️

Ila drama za kivita za Korea ndio mambo yote, hizi nyingine tunaangalia tu maana kuangalia sana historical huwa nachoka sometimes.
 
Umeeahi kuiona Empress Chunchu?!
 
Back
Top Bottom