Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hahahaha kiukweli ata mimi ninainywea amarula kuielewa,bangi ntazima.
Kweli apo nilichanganya mafile,nilikua namsemea eunseom.
Kwakweli kipawa ama talanta yako ya kulielezea Jambo nimeinyanyulia mikono juu. Yaan ata km mtu alikua amegoma kuielewa ataielewa tu kwa lazma.kwa kifupi in this uzi you're the best.haimanishi wengine hawako vizuri ila ur exceptional (sijui km ichi kimombo nimekipatia)

Turudi uku kwenye drama,Sanya ni kivuruge sijapata kuona.simwelewi sana dhamira yake.......ina maana hajui huyo anaemwita baba (tagon)ndie aliyeua kizazi chake!?yaan kiufupi simsomi kabsaaaaaa.anafanya matukio heavy alaf anaenda kujifungia ndani!ukiangalia hizo episode mbili naomba kujua amehamia upande wa Tanya ama,yaaan hayuko tena upande wa baba yake like let's rule the arthadal!?you will be the king and me nitakua mrithi!!?

Mubaek anatakiwa kumlinda nani mbona simwelewi na yeye!?Mana anamsnitch Tagon na huku niliona ameambiwa na Asa kan amlinde huyo mtu alomuua baba yake.

Episode ya 9 na 10 ni fire.nenthal Bado wanaexist na wanaonekana ni wababe.ebu zitazame nina maswali ya kutosha.
Ntakusumbua Sana nahis mpaka hii series ije iishe naomba tu ukuwe mvumilivu
 
Hahahaha tutakuchangia bas uende Seoul kabsaaa.
Hii kitu ndo niko episode ya pili.safari hii ongoing imenikamata........nimeona rate yake imefika 10 si kawaida.
 
Hahahaha tutakuchangia bas uende Seoul kabsaaa.
Hii kitu ndo niko episode ya pili.safari hii ongoing imenikamata........nimeona rate yake imefika 10 si kawaida.

Nitashukuru au Kukushukuru Mpaka Mwisho Wa Pumzi..
 
Shenzi kabisa wewe, unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.
Kwa sasa napambana na kina Goonyae na wang gun.nimeona kichwa chake kipo vizuri ( Goonyae) .
 

Wee Daemusin zote bila shaka ushaziona, ipi ni baba lao ipi ni ya kibabe zaidi.
 
Daah atamimi nimeshindwa kuivumilia
 
Nimempenda leo Jae In Ameujua Ubaya Wa Shemeji Yake,Na Kulifukuza Lile Li..... Nyumban kwa Dada yake...(Apa Choz kidogo Limenitoka 😒)
ja in baadhi ya nyakati ana tabia za ajabu ajabu lakini linapokuja suala linalowahusu dada zake anakuwa serious sana kuliko bwana yule anaposhuhudia mali ghafi zake alizoahidi kuzilinda zinachezewa.

episode 13 nimevutiwa zaidi na mazungumzo kati ya mama na mwana, daebak jung in kwa kuziweka wazi hisia zake mbele ya mama yake mzazi juu ya ji ho.

kadri muda unavyokwenda hukosa cha kuandika kuhusiana na hii drama, kwa ufupi tujiandae kisaikolojia kuzipokea episode mbili za mwisho ifikapo wiki ijayo inshaallah
 
Mubaek anatakiwa kumlinda nani mbona simwelewi na yeye!?Mana anamsnitch Tagon na huku niliona ameambiwa na Asa kan amlinde huyo mtu alomuua baba yake.

ngoja nikujibu hili kwanza kwa uelewa wangu dhaifu kwa sababu majibu yake yanapatikana part 1 ambayo ndio nimemaliza kuirejea.

tuanzie kwenye uvamizi wa ardhi ya IARK
mubaek alipokuwa anamtafuta eunseom baada ya kushindwa mbio za farasi alifika eneo fulani akakutana na kifaa kinachoitwa Byeoldaya, ndipo akamuuliza mwenyeji wake kuhusiana na asili ya hicho kifaa na akajibiwa
hiki kifaa tumekirithi kwa bibi yetu the Great mother White Wolf au jina lake halisi ni asa sin

kwa nini mubaek akashangazwa na majibu hayo?
ni kwa sababu kile kifaa kabila pekee lenye uwezo wa kutengeneza vifaa kama vile ni kabila la hae analotokea baba yake talha (mzee mihol) kwa sababu wao ndio wataalamu, hivyo basi vifaa vile vinapatikana ardhi ya arth pekee.
imewezekana vipi kifaa kile kuvuka mipaka hadi ardhi ya iark linakopatikana kabila la wahan na mengineo?
inawezekana vipi asa sin kufika kwenye ardhi ya iark?


ndipo akamtafuta yule bibi anayeitwa asa sakan anayefanya matambiko kwenye mapango ili amuulize maswali yake yanayomtatiza.

bibi akamuuliza unafahamu kuhusiana na cheonbuin?
mubaek akamjibu ndio kwa mujibu wa mungu arijun alivileta vitu vitatu kutoka mbinguni ambavyo ni upanga, kioo, na mfano wa kifaa kinachotoa sauti (labda niseme firimbi, ngoma, kengele) na kutumia vifaa hivyo atavitumia pindi atakapotaka kuiangusha dunia.
  • upanga (eunseom) = kwa ajili ya kuichinja dunia
  • kioo (sanya) = kwa ajili ya kuingarisha dunia kama nipo sahihi (illuminate)
  • kengele (tanya) = kwa ajili ya kuihamisisha dunia
akaendelea kumsimulia miaka 20 iliopita vifaa hivi vilijitokeza kwa mara ya kwanza hapa duniani na vyote vilijitokeza kwa siku moja (vilizaliwa), bibi akaendelea kumhadithia aliyefanya mauaji ya baba yake (alikuwa tagon) jana usiku ndiye atakayeongoza mapambano dhidi ya vifaa hivi vitatu hivyo basi ndio akamuomba mubaek ashirikiane na tagon kuviangamiza vifaa vitatu hivyo kabla havijaiangusha dunia.

dunia iliokusudiwa hapa ni nchi ya arthdal ambayo inatokanwa na muunganiko wa makabila tofauti yaliopiga hatua kubwa sana kimaendeleo ya fikra (civilizations) ukilinganisha na makabila mengineo, taifa hili la arthdal limejengwa kwa mfumo wa kugawana madaraka kwa makabila hivyo basi ili kuepusha ardhi hii ya arthdal isisambaratike kimfumo wake wa utawala tagon na wenzake wanapaswa waviangamize vifaa hivyo vitatu tishio.

sababu ya mungu kuvileta vifaa hivyo vitatu ni dalili tosha ya kwamba amechukizwa na yale yanaoendelea kufanyika kwenye ardhi ya arthdal, tumeshuhudia ubabe kwa baadhi ya makabila, maonevu dhidi ya makabila yasiokuwa na hatia kunyang'anya ardhi yao pamoja na mauaji holela dhidi ya jamii nyengine (neanthal)

si hivyo tu mungu amevileta vifaa hivyo vitatu kwa dhumuni la kusambaratisha mfumo wa uendeshaji nchi uliopo nyakati hizi (madaraka kugawanywa kwa makabila na asili ya mtu) kwenye ardhi ya arthdal na tutashuhudia mfumo mpya wa uendeshaji nchi (watu wote kuwa sawa haijalishi uwe ni igutu, saram, neanthal, masikini, tajiri, lofa).

ili kuzuia hayo yasitokee kwenye ardhi ya arthdal ndio bibi akamuomba mubaek amsaidie tagon kuiokoa dunia, alichokisahau yule bibi ni uwepo wa utabiri wa Daraburu ambao umeshatabiri anguko la arthdal kupitia mikono ya tagon.
si hivyo tu kitendo cha kumwambia mubaek amsaidie tagon ni kitendo cha aibu kwa muhubiri kama yeye kuongozwa na hisia za kipumbavu na si kutafuta ukweli na atakuwa amekwenda kinyume na mungu aliyevileta hivyo vitu vitatu na haijawahi kutokezea mungu kushindwa na binadamu.

safari ya mubaek kwenye ardhi ya IARK ilikuwa ni kama destiny kwa sababu ni yeye pekee aliyefanikiwa kushuhudia mambo ya ajabu.
  • amemuona farasi wa kanmoreu
  • amemuona mtoto wa asa hon
  • amefanikiwa kukiona kifaa cha ukweli kilichokuwa kinamilikiwa na asa sin
  • amefanikiwa kufahamu chimbuko la asa sin, yule bibi mbweha mweupe asili yake ni kutoka ardhi ya IARK na si kwenye ardhi ya arth ndio maana mrithi wake wa ukweli anatokea kabila la Wahan na si kabila la ASA.
 
Yaani Nimeona Preview Yake! Naona Mambo yaenda Kombo! Mi Hata Sitaziangalia.

Na Ile Scene ya Jin Min Alipokua Anabishana Na Baba Kigegu Yule! iko Kiuhalisia Sana

Wamefanya Kazi Nzuri Sana Hongera Zao
 

Ivi Bweha Ni Myama!?
 
Yaani Nimeona Preview Yake! Naona Mambo yaenda Kombo! Mi Hata Sitaziangalia.

Na Ile Scene ya Jin Min Alipokua Anabishana Na Baba Kigegu Yule! iko Kiuhalisia Sana

Wamefanya Kazi Nzuri Sana Hongera Zao
ji ho hafurahishwi na tabia za mama yake kumwazia mzazi mwenzake kila mara, si hivyo tu pia amepata taarifa zinazomuhusu mzazi mwenzake kufunga ndoa,
tendo hilo limemuumiza sana kiasi ambacho amefikia hatua anajihisi kama ni mwanamme asiyekamilika.
kama kweli yeye ni mwanamme aliyekamilika kwa nini amekimbiwa na mzazi mwenzake.

ndio maana baada ya kugonga chupa 8 za soju aliamua kumuuliza jung in kuhusiana na mustakabali wao wa maisha hapo baadae.
je jung in hatogeuka kama mama yake eun nu kwa kuamua kunikimbia?
inaonekana swali hilo limemkera jung in

jana ilikuwa ni sherehe ya kuagana kwa crew nzima ya one spring night
 
Nimempenda Ji Min Kapendeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…