DAEMUSHIN
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,428
- 120,464
mkuu umenichekesha sanaNdio nimeanza kuiangalia lakini summary nakuja kuifanyia kwenye maelezo yako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mkuu umenichekesha sanaNdio nimeanza kuiangalia lakini summary nakuja kuifanyia kwenye maelezo yako
Inachanganya sana mkuu ila ni nzuri sanamkuu umenichekesha sana
Hahahaha kiukweli ata mimi ninainywea amarula kuielewa,bangi ntazima.aigoooo hii sentensi yako umechanganya mchanga wa kawaida pamoja na mchanga wa makinikia unaoendelea kuleta msuguano kati ya beberu mweusi na beberu mweupe.
mubaek anamtafuta eunseom na si sanya kama ulivyoandika hapo juu, Sanya (ana nywele ndefu kama msichana wa kihindi) amekulia maisha ya mboga saba huku eunseom (lofa kutoka kolomije) amekulia maisaha ya dola moja kwa siku.
Aramun haesulla kizazi chake kimefikia mpaka maeneo ya Iark linakopatikana kabila la wahan anakotokea tanya ndio maana kabila la wahan pamoja na makabila wanaounda taifa la arthdal wanazungumza lugha moja, hata siku waliovamia ardhi ya Iark wanajeshi wa arthdal walishangaa kuona kabila la wahan wanazungumza lugha yao,
ushahidi mwengine umegundulikana ya kwamba mwanadada Tanya anatokana na kizazi cha bibi mbweha (asa sin jina lake kama nipo sahihi ambaye alikuwepo kwenye ardhi ya iark miaka 200 iliopita).
vugu vugu la wiki hii kwa mujibu wa uvumi imeonakanwa ya kwamba yule muhubiri mkuu wa dini (mzee asa ron) damu yake haijatokana na bibi mbweha( the Great mother White Wolf ) hivyo basi tagon kwa kuwa dhumuni lake ni kumuangusha yule mzee kuna uwezekano wa kutaka kumtumia Tanya ili abebe yale madaraka ya kuwa muhubiri mkuu kwa sababu tanya ni uzao halali wa bibi asa sin bila ya kusahau Tanya na yeye tayari ana mipango ya kutafuta nguvu ndio maana ameamua kumtumia sanya.
kwa nini mubaek anamtafuta eunseom haliyakuwa mwanzoni alikuwa anamwinda ili amuue?
inasemekana aramun haesulla atakuja kwa sauti mbili ya kike na kiume:
- ameshafahamu ya kwamba eunseom ni mtoto wa mwanadada asa hon
- eunseom ndiye mwenye kufahamu ni yupi muuaji wa ukweli wa sanung nirang (baba yake tagon)
- eunseom anafahamu siri ya tagon(mwanzoni mwa part 2 tuliona asili ya tagon kuwa ni igutu lakini ameficha siri mpaka muda huu)
- ana dalili za kuwa aramun haesulla mpya, namaanisha ya kwamba eunseom ndiye reincarnation ya aramun haesulla ambaye ndiye muanzilishi wa nchi ya arthdal.
kike = tanya
kiume = eunseom
na inasemekana aramun haesulla pia alikuwa ni igutu na huenda episode zijazo tagon atataka kuwadhihirishia watu ya kwamba yeye ndiye reincarnation yenyewe ya aramun haesulla kwa sababu na yeye pia ni igutu.
si hivyo tu aramun haesulla ana dalili nyengine zifuatazo:
Ionicera flower, The Hammer of Wind na farasi wa Kanmoreu.
farasi wa kanmoreu mpaka muda huu aliyewahi kumuendesha ni eunseom peke yake siku aliyofukuzwa na mubaek kwenye episode 2 na hata mubaek akawa anashangaa kwa nini kila nikiongeza kasi anashindwa kumfikia yule farasi wa eunseom akawa anajiuliza
inawezekana yule farasi ni kanmoreu?
na kama ni kanmoreu je yule aliyemwendesha ni aramun haesulla mpya kwa sababu farasi wa kanmoreu wameshatoweka kizazi chao.
si hivyo tu moja kati ya sifa ya farasi wa kanmoreu wana uwezo wa kuwavuta farasi wengineo, yaani kama farasi wa kanmoreu anaishi chato basi wale farasi wanaoishi kwa walima korosho watamfuta kanmoreu kwa lazima na hilo tumelishuhudia kwenye episode 3.
View attachment 1145655
episode 9 na 10 usiniulize maswali sijapata muda wa kuziangalia kwa umakini😛😛😛
arthdal chronicles kama hujavuta bangi wakati unaifuatilia huwezi kuambulia chochote
Aramun Haesulla: God of Harmony and Unification who brings Arthdal together.
Hahahaha tutakuchangia bas uende Seoul kabsaaa.Nimetoka Kuiangalia One Spring Night Muda Huu Episode ya Leo Yaani! Nikatamani Kama Nami Niingie Kwenye Screen....(Kivipi Sijui)
Ila episode ya leo Ni Balaa....
Ndugu yako Gi-Seok Naona Agekua tanzania angepewa Kabila la Wasukuma, kaka Mbishi Yule,Kaka Hakubari Kushindwa Yaani...
Nimempenda leo Jae In Ameujua Ubaya Wa Shemeji Yake,Na Kulifukuza Lile Li..... Nyumban kwa Dada yake...(Apa Choz kidogo Limenitoka 😒)
Ukweli Episode ya Leo Imekua Tamuu
Yah Waliwah Kusub..Raw Hata Hainogi.umeangalia bila ya subtitle au imewekwa mapema?
Hahahaha tutakuchangia bas uende Seoul kabsaaa.
Hii kitu ndo niko episode ya pili.safari hii ongoing imenikamata........nimeona rate yake imefika 10 si kawaida.
Shenzi kabisa wewe, unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.
- emperor wang gun drama : episode 200
- age of warriors drama : episode 158
- admiral yi soon shin drama: episode 134
- jang hee bin drama 2002: episode 100
- gwanggaeto the great : ep 92
- emperor of the sea drama : episode 51
- jumong drama :episode 81
- jing birok the memoir of imjin war : episode 51
- jung do jeon drama : episode 50
- sejong the great drama : episode 83
- kings dream :episode 70
- jewel in the palace :episode 54
- Empress Myeongseong : episode 124
- yi san : ep 77
- god of war : ep 56
- nibakishie na mimi ulevi
endelea kunywa mpaka watengenezaji ulevi pendwa waishiwe malighafi
- emperor wang gun drama : episode 200
- age of warriors drama : episode 158
- admiral yi soon shin drama: episode 134
- jang hee bin drama 2002: episode 100
- gwanggaeto the great : ep 92
- emperor of the sea drama : episode 51
- jumong drama :episode 81
- jing birok the memoir of imjin war : episode 51
- jung do jeon drama : episode 50
- sejong the great drama : episode 83
- kings dream :episode 70
- jewel in the palace :episode 54
- Empress Myeongseong : episode 124
- yi san : ep 77
- god of war : ep 56
- nibakishie na mimi ulevi
endelea kunywa mpaka watengenezaji ulevi pendwa waishiwe malighafi
Daah atamimi nimeshindwa kuivumiliaWapendwa msaada wenu!siangaligi ongoing series ata siku moja lakn hi arthadal chronicle imenishinda kusubiri.......yaaaaan uvumilivu umegoma kabsaaa.sasa Basi nakuitazama kote mpk episode ya 8 bado nimetoka kapa kwa kiasi kikubwa naombeni mnifungue macho vzuri niianze upya au nitaielewa mbele kwa mbele!?
ja in baadhi ya nyakati ana tabia za ajabu ajabu lakini linapokuja suala linalowahusu dada zake anakuwa serious sana kuliko bwana yule anaposhuhudia mali ghafi zake alizoahidi kuzilinda zinachezewa.Nimempenda leo Jae In Ameujua Ubaya Wa Shemeji Yake,Na Kulifukuza Lile Li..... Nyumban kwa Dada yake...(Apa Choz kidogo Limenitoka 😒)
Mubaek anatakiwa kumlinda nani mbona simwelewi na yeye!?Mana anamsnitch Tagon na huku niliona ameambiwa na Asa kan amlinde huyo mtu alomuua baba yake.
Yaani Nimeona Preview Yake! Naona Mambo yaenda Kombo! Mi Hata Sitaziangalia.ja in baadhi ya nyakati ana tabia za ajabu ajabu lakini linapokuja suala linalowahusu dada zake anakuwa serious sana kuliko bwana yule anaposhuhudia mali ghafi zake alizoahidi kuzilinda zinachezewa.
episode 13 nimevutiwa zaidi na mazungumzo kati ya mama na mwana, daebak jung in kwa kuziweka wazi hisia zake mbele ya mama yake mzazi juu ya ji ho.
kadri muda unavyokwenda hukosa cha kuandika kuhusiana na hii drama, kwa ufupi tujiandae kisaikolojia kuzipokea episode mbili za mwisho ifikapo wiki ijayo inshaallah
ngoja nikujibu hili kwanza kwa uelewa wangu dhaifu kwa sababu majibu yake yanapatikana part 1 ambayo ndio nimemaliza kuirejea.
tuanzie kwenye uvamizi wa ardhi ya IARK
mubaek alipokuwa anamtafuta eunseom baada ya kushindwa mbio za farasi alifika eneo fulani akakutana na kifaa kinachoitwa Byeoldaya, ndipo akamuuliza mwenyeji wake kuhusiana na asili ya hicho kifaa na akajibiwa
hiki kifaa tumekirithi kwa bibi yetu the Great mother White Wolf au jina lake halisi ni asa sin
kwa nini mubaek akashangazwa na majibu hayo?
ni kwa sababu kile kifaa kabila pekee lenye uwezo wa kutengeneza vifaa kama vile ni kabila la hae analotokea baba yake talha (mzee mihol) kwa sababu wao ndio wataalamu, hivyo basi vifaa vile vinapatikana ardhi ya arth pekee.
imewezekana vipi kifaa kile kuvuka mipaka hadi ardhi ya iark linakopatikana kabila la wahan na mengineo?
inawezekana vipi asa sin kufika kwenye ardhi ya iark?
ndipo akamtafuta yule bibi anayeitwa asa sakan anayefanya matambiko kwenye mapango ili amuulize maswali yake yanayomtatiza.
bibi akamuuliza unafahamu kuhusiana na cheonbuin?
mubaek akamjibu ndio kwa mujibu wa mungu arijun alivileta vitu vitatu kutoka mbinguni ambavyo ni upanga, kioo, na mfano wa kifaa kinachotoa sauti (labda niseme firimbi, ngoma, kengele) na kutumia vifaa hivyo atavitumia pindi atakapotaka kuiangusha dunia.
akaendelea kumsimulia miaka 20 iliopita vifaa hivi vilijitokeza kwa mara ya kwanza hapa duniani na vyote vilijitokeza kwa siku moja (vilizaliwa), bibi akaendelea kumhadithia aliyefanya mauaji ya baba yake (alikuwa tagon) jana usiku ndiye atakayeongoza mapambano dhidi ya vifaa hivi vitatu hivyo basi ndio akamuomba mubaek ashirikiane na tagon kuviangamiza vifaa vitatu hivyo kabla havijaiangusha dunia.
- upanga (eunseom) = kwa ajili ya kuichinja dunia
- kioo (sanya) = kwa ajili ya kuingarisha dunia kama nipo sahihi (illuminate)
- kengele (tanya) = kwa ajili ya kuihamisisha dunia
dunia iliokusudiwa hapa ni nchi ya arthdal ambayo inatokanwa na muunganiko wa makabila tofauti yaliopiga hatua kubwa sana kimaendeleo ya fikra (civilizations) ukilinganisha na makabila mengineo, taifa hili la arthdal limejengwa kwa mfumo wa kugawana madaraka kwa makabila hivyo basi ili kuepusha ardhi hii ya arthdal isisambaratike kimfumo wake wa utawala tagon na wenzake wanapaswa waviangamize vifaa hivyo vitatu tishio.
sababu ya mungu kuvileta vifaa hivyo vitatu ni dalili tosha ya kwamba amechukizwa na yale yanaoendelea kufanyika kwenye ardhi ya arthdal, tumeshuhudia ubabe kwa baadhi ya makabila, maonevu dhidi ya makabila yasiokuwa na hatia kunyang'anya ardhi yao pamoja na mauaji holela dhidi ya jamii nyengine (neanthal)
si hivyo tu mungu amevileta vifaa hivyo vitatu kwa dhumuni la kusambaratisha mfumo wa uendeshaji nchi uliopo nyakati hizi (madaraka kugawanywa kwa makabila na asili ya mtu) kwenye ardhi ya arthdal na tutashuhudia mfumo mpya wa uendeshaji nchi (watu wote kuwa sawa haijalishi uwe ni igutu, saram, neanthal, masikini, tajiri, lofa).
ili kuzuia hayo yasitokee kwenye ardhi ya arthdal ndio bibi akamuomba mubaek amsaidie tagon kuiokoa dunia, alichokisahau yule bibi ni uwepo wa utabiri wa Daraburu ambao umeshatabiri anguko la arthdal kupitia mikono ya tagon.
si hivyo tu kitendo cha kumwambia mubaek amsaidie tagon ni kitendo cha aibu kwa muhubiri kama yeye kuongozwa na hisia za kipumbavu na si kutafuta ukweli na atakuwa amekwenda kinyume na mungu aliyevileta hivyo vitu vitatu na haijawahi kutokezea mungu kushindwa na binadamu.
safari ya mubaek kwenye ardhi ya IARK ilikuwa ni kama destiny kwa sababu ni yeye pekee aliyefanikiwa kushuhudia mambo ya ajabu.
- amemuona farasi wa kanmoreu
- amemuona mtoto wa asa hon
- amefanikiwa kukiona kifaa cha ukweli kilichokuwa kinamilikiwa na asa sin
- amefanikiwa kufahamu chimbuko la asa sin, yule bibi mbweha mweupe asili yake ni kutoka ardhi ya IARK na si kwenye ardhi ya arth ndio maana mrithi wake wa ukweli anatokea kabila la Wahan na si kabila la ASA.
mbweha ni mnyamaIvi Bweha Ni Myama!?
yeah that was great, nairudia sana siichokiNiliipenda IRIS sijawahi kuona mfano wake
ji ho hafurahishwi na tabia za mama yake kumwazia mzazi mwenzake kila mara, si hivyo tu pia amepata taarifa zinazomuhusu mzazi mwenzake kufunga ndoa,Yaani Nimeona Preview Yake! Naona Mambo yaenda Kombo! Mi Hata Sitaziangalia.
Na Ile Scene ya Jin Min Alipokua Anabishana Na Baba Kigegu Yule! iko Kiuhalisia Sana
Wamefanya Kazi Nzuri Sana Hongera Zao
Kwaiyo Kiongozi Wao Alikua Mnyamambweha ni mnyama
ji ho hafurahishwi na tabia za mama yake kumwazia mzazi mwenzake kila mara, si hivyo tu pia amepata taarifa zinazomuhusu mzazi mwenzake kufunga ndoa,
tendo hilo limemuumiza sana kiasi ambacho amefikia hatua anajihisi kama ni mwanamme asiyekamilika.
kama kweli yeye ni mwanamme aliyekamilika kwa nini amekimbiwa na mzazi mwenzake.
ndio maana baada ya kugonga chupa 8 za soju aliamua kumuuliza jung in kuhusiana na mustakabali wao wa maisha hapo baadae.
je jung in hatogeuka kama mama yake eun nu kwa kuamua kunikimbia?
inaonekana swali hilo limemkera jung in
jana ilikuwa ni sherehe ya kuagana kwa crew nzima ya one spring night