Hahaha Drama ya Jeong Do Jeon na Great King Sejong
zilikuwa zinaendana na maandiko ya kihistoria.
Mh! Wacha niendelee na Wang Guhn.
utofauti mkubwa niliouona kupitia hiyo
drama ya emperor wang guhn kati ya waigizaji wakuu ni kwamba bwana wang guhn alizungukwa zaidi na wanadamu ambao walikuwa na fikra hai zilizomfanya wang guhn afanikishe malengo yake kwa urahisi zaidi,
jaribu kufikiria takribani asilimia kubwa ya magwiji wa elimu tofauti walikuwa upande wa bwana wang guhn ukimlinganisha na mfalme kyuhyun.
choi ung = aliingia serikalini akiwa na miaka 14 ya kuzaliwa nyakati za utawala wa gong yae, alikuwa ni zaidi ya genius aliyefanikiwa kusoma machapisho mbali mbali ya kielimu akiwa na umri mdogo sana, alikuwa ni nguzo kubwa sana ya fikra na ushauri kwa bwana gong yae hadi kwa bwana wang guhn. Choi ung alifariki akiwa na miaka 35 na kifo chake kilimwachia maumivu makubwa sana bwana wang guhn kwa sababu aliondokewa na kipenzi chake haliyakuwa bado hawajafanikisha ndoto yao ya kuziunganisha three kingdom.
choi jimong = huyu bwana mdogo nayeye alikuwa ni zaidi ya genius kwenye elimu ya nyota hadi nimebaki najiuliza hivi wanadamu kama hawa wapo kweli nyakati hizi au wamebaki wale wale jamii ya sheikh yahya husseni.
hakuna ndoto hata moja au utabiri aliowahi kuufanyia tafsiri ikawa kinyume chake, kuna vita fulani kuanzia episode za 150 alimtabiria bwana wang guhn atakutana na dhoruba kali sana hatimaye ikawa ni kweli ndipo wang guhn akaanza kuufanyia kazi ushauri wake,
kuna vita nyengine bwana wang guhn alipigwa na jeshi la baekje pona yake aliamua kutafuta nguo za wanajeshi wa baekje ili apate kukimbia na hatimaye mavazi yake ya kifalme akavalishwa rafiki yake wa karibu waliekula pamoja kiapo cha undugu (jina namuhifadhi kwa sasa).
kilichotokezea wanajeshi wa baekje wakamkata hyung nim wakidhani kuwa ndiye wang guhn, hasira zake bwana kyuhyun aliamua kumkata kichwa hadharani kwa hasira na kuitupa maiti yake.
bwana wang guhn alipofanikiwa kuiona maiti ya ndugu yake aliporudi mji mkuu alitoa amri ya kuchinjwa kila mwananchi mwenye asili ya makabila yaliovunja uaminifu kwake pamoja na koo zinazotokea taifa la baekje.
tukio hilo ndio pekee lililorikodiwa kwenye vitabu vya kihistoria katika tawala yake kuwa ni tukio la mauaji ya kinyama kulifanya bwana wang guhn
bila ya kumsahau millitary advisor bwana tae pil nayeye pia alikuwa ni zaidi ya genius, kuna vita fulani nayo pia ilirekodiwa kwenye vitabu vya kihistoria inasemekana jamaa alitabiri ndani ya siku saba zijazo upepo utabadili muelekeo baharini hivyo basi goryeo wasianzishe kampeni ya vita kwa siku saba mfululizo kufnaya hivyo wataipa faida baekje kwa sababu upepo kwa siku saba hizi kwa jinsi unavyovuma kimuelekeo itakuwa ni faida kubwa sana kwa baekje endapo watakaposhambuliwa.
ebwana weee alipofariki tae pil bwana wang guhn alimwaga chozi kuliko bwana yule lia lia anayekimbilia kanisani kuombewa baada ya kuanzisha vita asiyokuwa na uwezo wa kushinda