Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kirahisi Ivyo! Kwani ndo inavyokua!?
 
Hmmm!! ndo ufanyavyo..
si unamuona asali ya warembo anavyotembeza kipigo kila anapokwenda kama stering wa kihindi

kiupande wangu sina tabia hiyo, changamoto za kimahusiano haziondoshwi kwa kuyavunja mahusiano yenyewe.
 
Katika drama nilijutia kupoteza bundle langu basi ni hii
Duh niliipenda hii
Gu Family Book kiukweli inategemea na mtazamo wa mtu binafsi kama vile usemavyo ule usemi wa "Beauty is in the eye of the beholder" kwa maana ya kwamba kila mtazamaji anaweza ama asiweze kuuona uzuri wa hiyo Drama machoni pake.

Ila kwa upande wangu nili-Experience hali zote; Kuichukia na pia kuipenda.

Nadhani wengi wasiyoipenda ni pengine kwa sababu ya maudhui yake ya kutisha na kukosa uhalisia. Yaani uongo uongo mwingi kama uchaguzi wa nchi fulani hivi (jina silitaji).

Na wanaoipenda, nafikiri ni kutokana na washiriki katika Drama hiyo, kuanzia Lee Sung-gi mwenyewe na pia mwanadada Bae Suzy. Hiyo Chemistry haikuwa mbaya na mashabiki wao waliipenda kwa namna jinsi walivyoweza kuuvaa uhusika.

Kwa upande wangu naipa 5/10
 
Umefanya analysis nzuri
 
Shikamoo Master.
Asante kwa Highlight yako mzee kwanza n nipo episode ya 40,
Nakuuliza Emperor Wang Gun( King Taejo of Goryeo) Vs Yi Songgye( King Taejo of Joseon). Unamchangua nani na kwanini.
 
Huyu Mshikaji wako mara ya kwanza nilimuona kwenye Time Between Dog and Wolf, Princess Jamyunggo na Heartless City.
Yupo Vizuri kinoma.
 


Moja ya Drama Bora kuzishuhudia.
Story nzuri( Story nzuri na Kipacho Heavy).
Ujue niliumia sana pale Oh Mok Dan alipopigwa Risasi na Kimura Shunji. Tukio hilo lilipelekea Binti huyo Mok Dan kupoteza Maisha Siku ya Harusi Yake.
Afande Koiso nilikuwa simpendi.
Ila alikuwa anachezea kichapo sana pale Jang'o Police station.
Story ni ya miaka ya 1930- 1940.
Sijui kama hii story ni ya Maktaba au ni Utunzi. Kwako King Daemusin
 
Time between Dog and wolf. Drama bora kabisa ya wakati wote...sijasema kuliko zote maana Daemusin ataanza kunipopoa
Bila shaka ni drama nzuri. Drama za mjini za kipindi kile zilikuwa hazichoshi kama za siku hizi.

Achana nae huyo Daemushin anashabikia timu za kurithishwa( Thimba na Yanga) toka kwa babu yake.
 
Bila shaka ni drama nzuri. Drama za mjini za kipindi kile zilikuwa hazichoshi kama za siku hizi.

Achana nae huyo Daemushin anashabikia timu za kurithishwa( Thimba na Yanga) toka kwa babu yake.
Ila bwana hii title sikuielewa kabisa naomba unifafanulie kama hutojali
 
Ila bwana hii title sikuielewa kabisa naomba unifafanulie kama hutojali
Loo! Sasa hivi Network imekuwa shughuli kidogo ni mwendo 2G hata kuingia humu ndani ni vigumu.

Time Between Dog and Wolf.
Hiyo👆Title ni Ubunifu wa Hali ya juu wa kisanaa ulitumika ili kusadifu ujumbe uliyo ndani ya drama yetu na mwandishi ametumia Lugha ya picha, na hii itakupa hamu ya kutaka kujua kipi kilicho ndani humo. Mwandishi anawasilisha Ujumbe kuwa Ifikapo usiku, Uangavu hupotea sababu ya Giza hivyo inakuwa vigumu sana KUMTOFAUTISHA (Mbwa na Mbwa Mwitu) akiwa na maana. Kuto kuona Vizuri hupelekea kutomjua Rafiki na Adui. Kwahiyo Title yetu Imebeba Ujumbe ulio ndani ya Drama yetu.

Nadhani umepata mwanga japo ni kwa asilimia 5.


Hizi shughuli za Uchambuzi Dae Mushin ndiyo mtaalam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…