Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa Kwa kuwa ni wewe mkuu umeongea hivyo wacha niendelee kuiangalia
 
Alinikosha alipocheza kwenye " King Gwanggaeto The Great Conqueror " alikuwa anaitwa Teoli Pisu alikuwa anapiga mawe huyo!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Muno alikuwa kiboko yao ila tu aliniudhi alivyokuwa anamtreat Bidam
Munno aliwekeza vitu vingi sana kwa Bidam ili baadaye aje awe Mfalme kwa kumuoa Deokman ili kuutimiza ule 'utabiri' wa kuanguka kwa Mishil pamoja na mpango wa kuyaunganisha mataifa matatu.

Lakini baada ya lile tukio la mauaji la Bidam kule kwenye mapango lilimdhoofisha sana na kumvunja moyo Munno kiasi cha kuanza kumbadilikia Bidam na hata kubadili mpango wake na kutafuta mtu mwingine (Kim Yusin) kuchukua nafasi ya Bidam.

Ni kweli naweza kusema kuwa pamoja na mabaya ya Bidam aliyoyafanya sidhani kama ilikuwa sahihi sana kwa Munno kumchukia kupita kiasi na kumshambulia kwa maneno Bidam kutokana na kosa la utotoni.

Ila ni ngumu sana kwakweli katika hali ya kibinadamu kwa mtoto mdogo kuwaua watu wote wale tena kwa kudhamiria, inatisha sana na kuna funzo kubwa sana hapo ukizingatia kwamba Munno naye alikuwa binadamu pia.

Lakini yote kwa yote Munno alikuja kujirudi kwa Bidam nyakati za mwisho wakati anakufa na akamwambia kuwa daima yeye (Bidam) atabaki kuwa mwanafunzi wake na pia akampatia fursa ya kujiunga na Hwarang.
 
Kwenye drama ya Queen Seondeok majembe wangu walikuwa no hawa hapa
 

Attachments

  • download%20(4).jpeg
    7 KB · Views: 27
  • download%20(3).jpeg
    7.3 KB · Views: 23
  • download.jpeg
    8.7 KB · Views: 19
  • images.jpeg
    11 KB · Views: 24
  • download%20(2).jpeg
    8.4 KB · Views: 24
  • images.jpeg
    11 KB · Views: 16
Ni kazi nzuri sana walifanya hasa kusimama katika nafasi zao na kuubeba uhusika vilivyo ili kuhakikisha kazi inakuwa bora sana machoni pa watazamaji (yaani sisi).

Bila kuwasahau pia walioigiza katika Characters wengine kama vile;
  • Misaeng
  • Mishil (Seju)
  • Jukbang (The Mighty)
  • Godo
  • Alcheon
  • Kim Seohyeon (Baba yake Kim Yusin)
  • Sejong
  • Princess Cheonmyeong
  • Hajong
  • Bojong
Na wengine wengi waliohusika bila kusahau Character mkubwa kabisa aliyebeba Drama na Storyline kwa ujumla, Deokman kuanzia utoto hadi 'utu uzima'.
 
Ama kweli kwangu mimi hata chronicles haingii kwa hapa
 
Ni kweli lilikuwa tukio baya sana lakini mimi naona zilikuwa akili za utoto tu na kama alivyofanikiwa kumshape katika mengine angeweza kumuelimisha na hilo pia na kwa vile alikuwa bado mdogo angerekebika tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…