WAIGIZAJI WA KIKE WASAIDIZI (SUPPORTING ACTRESS) WANAONIVUTIA KWENYE TAMTHILIA ZA
KOREA.
Mara ya mwisho nakumbuka niliweka listi ya waigizaji wa kiume ambao (wenye umri wa Zaidi ya miaka 40) ambao mara nyingi huigiza kama supporting actors ambao tokea nianze kufuatilia Korean drama wamekuwa wakinivutia kutokana na uwezo wao wa kuigiza haijalishi nafasi gani wanaigiza.Leo ni zamu ya wanawake, inawezekana siwafahamu wengi sana ila hawa wafuatao ni baadhi ya wanaonivutia kutokana na uwezo wao katika tasnia ya uigizaji.
1)
Song Ok Sook:
kama ni mfuatiliaji mzuri wa Korean drama ni lazima utakuwa unamfahamu mwanamama huyu ambaye amezaliwa miaka 56 iliyopita.Ni mwanamama (ahjumma) mcheshi sana na anayeheshimu kazi yake,miongoni mwa kazi alizoigiza ni BIG MAN,
TREE WITH DEEP ROOTS,
QUEEN SEONDEOK,
MISSING YOU,ROOFTOP PRINCE.
2)
Lee Il Hwa:
inawezekana ameshakuwa ni mtu mzima ila bado ni mrembo na mara nyingi anaigiza kama ni mama.ameigiza tamthilia kama QUEEN OF AMBITION,
YOU WHO COME FROM THE STAR,ILJIMAE,UGLY ALERT.
View attachment 373321
3)
Kim Sung Ryung:
mara ya mwanzo nilimuona kwenye tamthilia ya YOU ARE BEAUTIFUL alikuwa mkorofi sana,baadae nilimuona kwenye Princess Jamamyung ambayo aliigiza kama mke wa mfalme wa taifa la Nakrang ambaye pia ni mama wa Jamyung,pia nilimuona kwenye THE HEIRS,IL JIMAE,
QUEEN OF AMBITIONS, ana miaka 49.
View attachment 373323
4)
Oh Yeon Soo: ana miaka 44 aliigiza tamthilia ya
PRINCE OF THE LEGEND kama ni mama wa Jumong,chakuvutia na kushangaza yeye na
Song il kook ambaye aliigiza kama
jumong wamezaliwa mwaka mmoja.kwenye tamthilia ya
GYE BAEK pia aliigiza kama ni Queen wa taifa la Baekje,tamthilia nyengine ni
TRIANGLE na IRIS 2.
View attachment 373326
5)
Kim Mi Kyung: ana miaka 52,ana kipaji na ni mbunifu haijalishi ni nafasi gani anaigiza katu hatomkera mtazamaji.nimemuona kwenye tamthilia nyingi sana kama vile
FAITH,
THE HEIRS,
ITS OKAY THAT’S LOVE,
MISSING YOU,
MASTERS SUN,
SUNGYUKNWAN SCANDALS.
View attachment 373331
6)
Kim Soo Mi: ana miaka 64 alinivutia sana kwenye ,
VAMPIRE IDOL, LEGENDARY WITCH,KING AND I,INCARNATION OF MONEY ni mtaratibu sana anapozungumza.
View attachment 373332
7)
Bae Jong Ok:ana miaka 52 na ni miongoni mwa waigizaji ninaowakubali sana haijalishi nafasi gani anaigiza nilimpenda sana kwenye
KIM SO ROO,pia ameigiza tamthilia kama
THAT WINTER THE WIND BLOWS,na
SPY ambayo alicheza kama mpelelezi wa taifa la Korea ya Kaskazini.
View attachment 373333
8)
Kim Hae Sook: ana miaka 60 ni ahjumma,unaweza kumuweka katika kundi lolote unalotaka ikiwa ni ukorofi,upole,vichekesho.nilimpenda kwenye
WINTER SONATA ambayo aliigiza kama ni mama wa Choi Jin Woo.tamthilia nyengine alizoigiza ni
CAIN AND ABEL,
HOTEL KING,
I CAN HEAR YOUR VOICE, PINOCCIO
View attachment 373334
9)
Ban Hyo Jung: ana miaka 73 nimebahatika kuangalia drama mbili tu alizoigiza yeye ambazo ni
SHINING INHERITANCE na
ROOFTOP PRINCE.
10)
Im Ye Jin: ana miaka 56 alinivutia kwenye
BOYS OVER FLOWER,
MY PRINCESS na
QUEEN SEONDEOK.
View attachment 373336
11)
Kyun Miri:ana miaka 52 aliigiza drama ya jumong kama ni mama wa daeso na young po,pia ameigiza tamthilia ya
JEWEL IN THE PALACE.
View attachment 373339
12)
Go Hyun Jung: ana miaka 45 ila bado ni mrembo na alikichafua sana kwenye
QUEEN SEONDEOK
View attachment 373337
13)Lee Bo Hae:ameigiza drama kama vile AMAN CALLED A GOD,IRIS 2,KING GWAGGAETO,terms of endearment
14)kim mi sook:kwa maoni yangu yeye ndio bridget bardot wa korea naamini kama ni mfuatiliaji wa korean drama utakubali,ameigiza tamthilia nyingi tu kama vile CITY HUNTER,FLOWER IN PRISON,QUEEN INSOO,ALL ABOUT MY MOM
15)Choi Ran :nilimpenda kwenye HONG GIL DONG katika harakati za kugombamia madaraka ya kifalme,ana miaka 56.tamthlia nyengine alizoigiza ni POSEIDON,SWALLOW THE SUN,GYE BAEK,YOU ARE BEAUTIFUL.
16)Chae Sira:jee umepata nafasi ya kuangalia tamthilia ya HAESHIN(emperor of the sea) EMPRESS CHUNCHU,TERMS OF ENDEARMENT,QUEEN INSOO,UNKIND LADIES,ni mwanamama ngangari anayejua nini maana ya uigizaji.ana miaka 49 ila mimi nimempenda kwenye tamthilia ya FIVE FINGERS
View attachment 374452