Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Mkuu Silla ya zamani ilikuwa upande upi
Isijekuwa ilikuwa kusini wakati mimi na ushoga ni kushoto na kulia
 
Mkuu Silla ya zamani ilikuwa upande upi
Isijekuwa ilikuwa kusini wakati mimi na ushoga ni kushoto na kulia
Ramani ya Nasaba( Dynasties) za KOREA kwa nyakati tofauti tofauti.ila jua tu hizo Nchi zote Kuna muhuni anaitwa Tam teok( King Gwanggaeto the Great) alizikonka wakati wa utawala wake. Ngoja
Daemusin aje atuhadithie zaidi miye nimeleta Ramani, sasa na yeye aje akamilishe jukumu lake la kutupa story.
Huyo muhuni(Daemusin) anafaa sana kuwa msimulizi wa Historical Drama za CHATO Empire.



 
NEWS

RapidVideo, a popular file-hosting service with millions of users, has thrown in the towel. The site faces legal pressure from lawyers representing the MPA and ACE, including a lawsuit from Warner Bros. and Netflix. Paired with dwindling revenues and a worsening legal climate, maintaining the site is no longer viable, according to the operator.

Mambo yanaanza kuwa magumu tena ilikua simple kuvuta movies kwa server ya Rapidvideo
 
ndio nini kutuwekea miramani yote hii humu ndani utadhani tunajifunza geographical science, cha kushangaza zaidi na kutustaajabisha kwenye nafsi zetu zilizojaa wasiwasi kutokana na matukio yaliorindima wiki iliokwisha ni hizo ramani zote ulizoziweka zimeshindwa kutuonyesha locations sahihi tutakayoweza kumpata kigogo 2020.

karibu biryani kwa maziwa ya paka nyauuu
 
halafu jana usiku nilipokuwa naipakua melting me softly drama sikuijaribu hiyo server, lakini mbona sever zipo nyingi za kushushia videos au ndio mazoea ya rapid video yameshakuletea athari ndani ya ubongo wako?
 
Hii rapid video zake hazizidi mb 300. Kuna server nyingine zipo juu hadi mb 700 na kuendelea hio episode moja tu,parefu sana hapo

Nikizoea kitu ni ngumu kubadili. Niliipenda sana dramania pamoja na kwamba ilikua na vipande viingii episode moja. Ilipobomoka nilipata tabu sana.

Server gani nyingine nzuri? isiyo na uzito mkubwa ili nihamaie huko
halafu jana usiku nilipokuwa naipakua melting me softly drama sikuijaribu hiyo server, lakini mbona sever zipo nyingi za kushushia videos au ndio mazoea ya rapid video yameshakuletea athari ndani ya ubongo wako?
 
Hii rapid video zake hazizidi mb 300. Kuna server nyingine zipo juu hadi mb 700 na kuendelea hio episode moja tu,parefu sana hapo
mara nyingi episode ikiwekwa mapema halafu ukaipakuwa ndipo unapokutana na mziki wa mb nyingi kama hizo 700- 1 gb kwa sababu unaweza kuikuta video quality yake iliopo ni 720 hadi 1082 full hd.

480 video quality ndio inatembea wastani wa mb 250 - 450 baadhi ya nyakati.
360 video quality inatembea wastani wa mb 120 - 250.

uzuri zaidi video nyingi unaweza kuzikuta video quality zote tatu kwa wakati mmoja
hapo ni wewe mwenyewe na chaguo lako pamoja na uwezo wako wa bando.
 
Huwa unaingia kwa kutumia browser gani?maana mie hio FE huwa hainipi hizo 360,480 naona inanitupia 720
 
Sorry kama ulishawahi kujibu swali hili hivi ni kwanini joseon ilihitaji ruhusa ya ging katika kusimika crown prince na baadhi masuala muhimu kwa serikali yao?
 
Kwa kawaida mie ni mpenzi mtazamaji wa drama zilizoisha kwa rapid mambo yalikua mteremko ila kwa sasa duh graceful family kila ninapogusa mb 600 na kuendelea

Hio 360 ipo vizuri mno,nikiidaka itakua poa
 
Huwa unaingia kwa kutumia browser gani?maana mie hio FE huwa hainipi hizo 360,480 naona inanitupia 720
google chrome browser kwa njia ya computer.
mbona nikibonyeza setting kwangu inakuja nilipojaribu ep 1 ya graceful family?
 
Sorry kama ulishawahi kujibu swali hili hivi ni kwanini joseon ilihitaji ruhusa ya ging katika kusimika crown prince na baadhi masuala muhimu kwa serikali yao?
hayo maswali yako kamuulize mr gogoli naamini hatokuangusha πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€.
ngoja nikujibu kutokana na uzoefu wangu wa kuangalia joseon historical drama ( mimi ni mvivu na mjinga nisiyependa kusoma machapisho haijalishi yameandikwa kwa kiswahili).

kwa ufupi joseon walikuwa na ukaribu mkubwa sana na taifa la MING dynasty kutoka china na walikuwa wanashabihiana kwa mambo mengi sana kwa sababu wote hao waliwahi kunyanyaswa na Mongolia.
  • fahamu pia joseon ilikuwa ni tributary states kwa Ming dynasty, ina maana hata hao wafalme wa mwanzoni pamoja na crown princes pia walihitaji baraka kutoka ming ili waweze kutawala joseon. Tokea mwanzo joseon walishajificha kwenye kivuli cha Ming China baada ya lee seong gye kuiangusha goryeo.
  • joseon na ming wote walikuwa ni waumini wa Neo confucianism na ndio mfumo walioutumia kwa ajili ya kuendeshea serikali zao.
  • kwa nyakati tofauti nchi mbili hizi mpinzani wao mkubwa alikuwa ni japan na jurchen.
  • mwanzoni wajoseon walikuwa wanatumia lugha ya Ming na ndio iliopewa heshima zaidi na matajiri kuliko hangul.
  • baadae Ming china iliangushwa na wahuni wanaoitwa jurchen na hatimaye kuanzishwa tawala ya Qing dynasty na kwa kiwango kikubwa waanzilishi wa taifa la Qing walionekana ni barbarians wasioheshimu civilization mbele ya joseon na ndipo hapo ikakataa kuitambua Qing kama ni rafiki mpya
  • pia baada ya kuanguka kwa Ming dynasty taifa la joseon likawa linajitambulisha kama ni taifa pekee lenye chembe chembe za uchina ndani yake (sojunghwa = "Little China" )
  • balaa ndio likaanzia hapo baada ya joseon kukataa kuitambua Qing kama ni taifa rasmi (joseon wakiongozwa na mfalme Injo waliichukulia poa Qing dynasty)
  • mnamo mwaka 1636 taifa la Qing wakiongozwa na mfalme wao hong taiji walifanya uvamizi ndani ya joseon na kilichotokezea baadae ni kitendo cha mfalme wa joseon kumpigia magoti mfalme wa QING baada ya kipigo kuwa kizito kama kile cha japan ya togugawa (nyakati zile za uvamizi wa japan waliokolewa na MING ambayo baadae ndio hivyo ilisambaratishwa na QING)

  1. joseon hawakutakiwa tena kutamka au kulitumia jina la Ming, muhuri wa ming na kila kitu kinachohusu ming yakiwemo mavazi na hata machapisho
  2. mtoto wa kwanza na wa pili wa mfalme Injo walichukuliwa mateka pamoja na watoto wa mawaziri.
  3. joseon walilazimika kutumia calendar za Qing
  4. joseon walitakiwa walitambue taifa la Qing kama ndiye baba wa maamuzi (hapa ndipo lilipo swali lako)
  5. joseon walitakiwa kutoa meli za kivita kwa ajili ya kuwasafirisha wanajeshi wa Qing
  6. joseon hawakutakiwa kujenga ngome yeyote ile
  7. joseon walitakiwa wasiwapokee mateka kutoka Qing (mateka wa vita waachiwe huru)
  8. viongozi wa joseon na Qing wawe na uhusiano wa damu (wafunge ndoa)
 
Nimeelewa mzee baba shukrani sana.
 
Kumbe computer, ntajaribu leo. Huwa natumia simu kwa uc browser huwanavuta hadi gb 8 kisha nahamishia kwenye laptop
hiyo simu matangazo huwa hayakukeri au zipo software za kublock matangazo?
tafuta software ya IDM baadae uingize kwenye PC.
hizo gb 8 utaziona kama ni upuuzi na utabaki kulaumu kwa nini muda ni masaa 6 tu.
teh teh teh
 
Hii browser ninayotumia huwa inapunguza matangazo. Ila sasa speed ya ka halotel huwa ndogo balaa. Dramania nilikua navuta hadi movies tatu kwa wakati mmoja pamoja na kwamba ilikua na matangazo ya kutosha.

Hahaha hata saiv huwa nalaumu muda mchache sana. Shukran ntafata ushauri wako
hiyo simu matangazo huwa hayakukeri au zipo software za kublock matangazo?
tafuta software ya IDM baadae uingize kwenye PC.
hizo gb 8 utaziona kama ni upuuzi na utabaki kulaumu kwa nini muda ni masaa 6 tu.
teh teh teh
 
Acha niendelee kuamini kwamba Gogyureo ni ya Korea
Sitaki usumbufu wa watang
 
Una kipaji cha ualimu maana nimekuelewa vizuri sana tu pamoja na bongo langu kuwa gumu
 
Kuna series inaitwa kill me,heal me ni noma ni ya 2019 inahusu jamaa mmoja ambaye ana tatizo la kuingiliwa na nafsi mbaya asipopata dawa ya kutoingiliwa na nafsi anageuka kuwa katili na anafanya mambo mabaya baada ya tu nafsi kutoka anarudi kuwa normal na hali yake ya kawaida ya kuwa mpole na anapoteza kumbukumbu ya kitu gani alichofanya.kuna wakati anashangaa anavamiwa na watu anapigwa bila kujua kwanini watu wanampiga kumbe anashindwa kujua aliingiliwa na nafsi ilisababisha kuwapiga hao watu kwa kutumia mwili wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…