M
imi binafsi najisikia fahari kuwashuhudia hawa waigizaji wawili
CHOI SOO JANG na
SONG IL KOOK, kwa kweli hawa jamaa wana vipaji vikubwa sana katika fani ya uigizaji.
tufahamu kuwa
CHOI SOO JANG ni mkubwa kwa miaka 8 zaidi ya
SONG IL KOOK kwa hivyo
CHOI SOO JANG alianza kuigiza mwanzo na kuwa maarufu .
SONG IL KOOK alianza kujifunza kuigiza 1998 akiwa na miaka 27 baada ya kushauriwa na
YOO DONG GEON ambaye alikuwa akifanya kazi ya uigizaji pamoja na mama yake song il kook pia alikuwa ni mwanafunzi wa mama yake, amecheza drama nyingi kama
YEON GAE SOMUN,ATHENA,JEONG DO JEON na GU FAMILY BOOK baada ya kumuona kuwa na umbile zuri la kuwa muigizaji,
kwa hivyo kwa mtu ambaye hakuwa na ndoto wala kipaji cha kuigiza anahitajika kuwa na jitihada kubwa sana ili kufuzu katika majaribio.
Wakati
CHOI SOO JANG anacheza historical drama ya
EMPEROR WAN GUN mwaka 2002 ambayo ilimpa mafanikio makubwa na tunzo mbali mbali na kuzidi kumpa umaarufu nchini korea
SONG IL KOOK bado alikuwa ni muigizaji wa kawaida tu.
Baada ya kumaliza drama ya
emperor wan gun CHOI SOO JANG ndipo alipopata ofa nyengine ya kuigiza historical drama ya
EMPEROR OF THE SEA (haeshin) mwaka 2004 akiwa na miaka 42 na akiwa ndio muigizaji mkuu
(goong bok baadae jang bogo).
Baada ya kuonesha uwezo mkubwa katika tamthilia ya
TERMS OF ENDEARMENT ndipo
SONG IL KOOK alipata ofa ya kuigiza
emperor of the sea akicheza kama
(yum mun / yum jang)ambaye alikuwa ni mpinzani wa
jang bogo, tufahamu kuwa kabla ya song il kook hajapata nafasi ya kuigiza kwenye haeshin tayari nafasi ya yum mun alikwisha chaguliwa muigizaji mwengine ambaye ni
HAN JAE SUK ambaye amecheza drama kama
LOBBYST na tayari walikwisha kuanza kushoot ila baadae jamaa akaamua kuacha na kuamua kuchagua ofa nyengine,
kivyovyote song il kook hakuwa na uzoefu katika historical drama (sageuk) kwa sababu ilikuwa ni historical drama ya kwanza kushiriki ila naamini 50% ya mafanikio ya
emperor of the sea yametokana na performance ya song il kook aliyoionyesha.
Nimeona baadhi ya watu waliotoa maoni yao wamesema
choi soo jang ni bora zaidi ya
song il kook kwa sababu
choi soo jang ni mkali katika mapigano (martial arts): nakubaliana na hoja yao kwa sababu tayari nisahamuona kwenye
DAEJO YOUNG, HAESHIN,
EMPEROR WAN GUN japo sijaimalizia na hata kwenye
THE GREAT KINGS DREAM.
Lakini mimi siamini kama uwezo wa muigizaji unapimwa kwa mapigano (martial arts) kwa sababu naamini wanaopanga mapigano ni team ya madirector kwa hivyo kivyovyote muigizaji anafuata ushauri wa director.Na hata wakati alipohojiwa director wa drama ya emperor of the sea alisema waliamua kuweka mapigano mengi ili kuonesha jinsi gani jang bogo alivyopambana sana na wateka nyara wa baharini wakati wa uhai wake,na pia waliamua kumfanya
jang bogo ni mpiganaji bora zaidi ya master wake na
yum mun ,na pia waliamua kumfanya
yum mun ni bora zaidi ya
yeon wanapopambana .kwa mfano ukiangalia drama kama
WARRIOR BAEK DONG SOO utagundua kuwa director alimfanya
Baek Song Soo kuwa ni zaidi ya
Sky Lord lakini kiuhalisia
sky lord alikuwa ni hatari kama
sword saints.
Maumbile yao na Uwezo wa kucheza nafasi tofauti : kwa mtazamo wangu
choi soo jang ni hodari zaidi anapocheza kama mtu wa chini kimaisha na baadae akaibuka kuwa ni shujaa kwa mfano kwenye
emperor of the sea alianza kama mtumwa na baadae mpiganaji mwisho akawa ni mfanya biashara mkubwa sana,pia kwenye
Daejo young alikuwa ni mtu wa chini sana mpaka akawa general mkubwa mpaka akafanikiwa kuanzisha taifa la
BALHAE,kiukweli sijavutiwa na uwezo wake kwenye
dream of emperor ambapo alicheza kama ni member wa royal family (prince chunchu) huwa nampenda choi soo jang anaposimama kama ni mpigania haki aliyepitia maisha ya shida kwa sababu sura yake inaonekana kama ni mtu ambaye muda mwingi anakumbana na matatizo .kitu chengine nilichokigundua kwa
choi soo jang ni kuwa umbile lake halimpendezi anapocheza kama mfalme.
Kwa mtazamo wangu mimi ukimwondoa
JANG HYUK ambaye ameigiza drama kama
SLAVE HUNTER,
DEEP ROOT TREE, ,
SHINE OR GO CRAZY yeye ndie pekee ambaye naweza kumlinganisha na
song il kook linapokuja suala la kucheza nafasi mbali mbali kutokana na umbile lake.
Mimi binafsi nashindwa kufahamu ya kwamba
song il kook ana sura ngapi kwa sababu anabadilika kutokana na uhusika anao uvaa tofauti na
choi soo jang.ukimwangalia kwenye
emperor of the sea sura yake,umbile lake na uzungumzaji wake ni tofauti kabisa na kwenye
PRINCE OF THE LEGEND wakati alipokuwa ni prince wa
buyeo ni tofauti na alipokuwa ni general wa kikosi cha
DAE MUL ARMY na pia ni tofauti na alipokuwa mfalme unaweza kusema ni watu wa tatu tofauti, hata kwenye
KINGDOM OF THE WIND na
JANG YOUNG SIL ameonesha uhusika tofauti. Pia umbile lake anavutia anapokuwa mfalme na hata anapokuwa general.
Love chemistry (Couples): nampa
song il kook 80% dhidi ya
choi soo jang 20% naamini hata team
choi soo jang mutakubali kuwa
song il kook ni zaidi katika sekta ya mahusiano. kwa mfano ukiangalia
emperor of the sea CHOI SOO JANG alipata nafasi nyingi sana za kukutana na
LADY YUHWA (soo ae) kuliko
song il kook lakini uzungumzaji wake na uwasilishaji wa hisia zake ulikuwa hauvutii .hata kwenye
DAE JO YOUNG alipokuwa akikutana na
lady chullin au
princess sukyoung alikuwa anaboa sana, naweza kusema
choi soo jang na waigizaji wengine wa korea watasubiri sana kufikia uwezo wa song il kook linapokuja suala la love chemistry.
Naamini kila aliyeangalia
emperor of the sea hata kama ulikuwa ni
Team Choi soo jang (jang bogo) ulikuwa unatamani kila episode wakutane
song il kook (yum mun) na
soo ae (lady yuhwa) naweza kusema ilikuwa burudani sana wakizungumza japo kuwa
soo ae alikuwa slow sana akizungumza ila song il kook alimfutia sana makosa yake. Mpaka leo nazikumbuka baadhi ya nukuu (quote) pindi walipokuwa wakizungumza.
Kwa mfano katka episode ya 22 baada ya jang bogo kukamatwa katika kambi ya YISADO ilibidi
lady yuhwa atumie udhaifu wa kupenda aliokuwa nao
yum mun na kumuahidi kuwa yupo tayari amtumikie kama mume wake ila amwachie jang bogo, na nilipenda majibu ya
yum mun (song il kook) nakumbuka alimwambia
“tafadhali simama, ni mara ngapi nimekuomba uwe mwanamke wangu lakini hutaki, leo hii unasema upo tayari uwe mke wangu, labda unafikiri nitajisikia furaha,hali ya kuwa mimi sipo ndani ya moyo wako, si unasema utakuwa mke wangu basi sawa hata kama nitashindwa kuuteka moyo katu sitakubali kuupoteza mwili wako “
Katika episode ya 24 wakati
yum mun anamwaga
LADY YUHWA kwa ajili ya kwenda vitani na kumuomba aondoke arudi
YANGZHOU lakini
YUHWA akakataa na akamwambia
yum mun “
nitakusubiri naamini utarudi salama vitani”.
Yum mun alitabasamu na baadae akamjibu
“laiti kama maneno hayo ningeliyasikia tulipokuwa Mujinju ningelijiona ni mwanamme mwenye bahati sana na ningeliachana na ukorofi wote nilionao,lakini wewe moyoni mwako yupo jang bogo tu,mama yangu alikuwa mtumwa na alifariki kwenye jahazi ndipo master yi akaamua kunilea yeye ni kama baba yangu,mwanzo niliwahi kukwambia kuwa niliwahi kukuona ulipokuwa mdogo maeneo ya Chunghae, urembo wako,tabasamu lako niliamini vingeliniondolea upweke na huzuni nilionao kwa kukosa mapenzi na malezi ya mama ila nimeshindwa kumuondoa jang bogo ndani ya moyo wako kwa hivyo tafadhali nakuomba uondoke uwende kwa jang bogo kwani yeye ndie pekee unayemuona atakupa furaha”
Halafu chakuvutia zaidi ilikuwa
yum mun na yuhwa wakizungumza inatumika
Korean ost aliyoimba
Lee hyun sup inayoitwa
prayer (gido) beti ya kwanza.
Pray let her stay by my side, Even if I can't have her heart Until she sees the tears in my heart . pray let her look back once, So she can see me by her side whenever that may be Give me the patience to wait, So that my longing for her doesn't become a sin, Pray let her know someday that my love was anything but small Answer my prayer....
Kupitia drama hii ya HAESHIN
song il kook alishinda tunzo tatu
(best couples,excellency actor,popular actor) na
choi soo jang alishinda tunzo moja.
(best actor) hata kwenye tamthilia ya
PRINCE OF THE LEGEND love chemistry kati ya
soseono(han hye jin)na jumong(song il kook) ilikuwa ni ya kuvutia na pia love chemistry kati ya
jumong na yesoya(song ji hyo) ilikuwa inavutia.song il kook alishinda tena tunzo tatu kupitia tamthilia ya jumong.
pia kwenye kingdom of the wind licha ya mwanadada yeon (choi jung won) kuonesha uwezo mdogo sana wa kuigiza jambo ambalo lilisababisha katika tunzo za mwaka 2008 mashabiki wengi kuhisi alipendelewa baada ya choi ji won kushinda tunzo mbili akimpiku mwanadada
SUNG YURI ambaye alicheza kwenye
HONG GIL DONG kama YINOK ambaye alitegemewa atabeba yeye tunzo.
kiukweli song il kook akicheza kama
prince muhyool (king damushin muhyool) alimbeba sana choi jung won na song il kook alishinda tena tunzo tatu mfululizo kupitia historical drama zote tatu.
Kwa mtazamo wangu mimi
song il kook ndie “
king of historical drama’”.