FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Nami pia kuna projects kadhaa za miaka ya nyuma ambazo kiukweli sikupendezwa nazo na zipo ambazo sikukamilisha kuzitazama lakini wakati mwingine baadaye huwa nafanya maamuzi magumu ya kuzitazama (kwa lazima) na bahati nzuri ninapomaliza kuzitazama, huwa napata kupendezwa na vitu fulani fulani ndani yake.iruhusu nafsi yako ikutawale na si kipande cha moyo wako.....
mwaka jana niliangalia search: www drama mpaka episode 4 nikashindwa kuiendeleza, mwaka huu nimeirudia mwanzo mwishoooooo.
moyo ulishindwa kuikubali project hiyo, nikairuhusu nafsi nayo iamini hivyo.
nilikuwa siwezi kuangalia family drama lakini kwa sasa nimejizowesha.
nilikuwa siangalii project za kimagharibi ila ndani ya mwaka huu nimeshangalia series 5 (changamoto kubwa ni mfumo wa series unanipa tabu, nahitaji niangalie series imalize na si kupigwa kalenda)
Kuna msemo fulani unasema "kisichokufaa leo huenda kikakufaa kesho".
Na hili nimelithibitisha kabisa na kwa muda mrefu tu katika projects kadhaa nilizowahi kuziweka pembeni hapo awali kisha nikaja kuzitazama hapo baadaye na kupendezwa na vitu kadhaa ndani yake. Moja wapo ya kazi hizo ni ile maarufu kabisa iitwayo Gu Family Book.