Ni kweli usemavyo jamaa uigizaji wake mi pia uliniboa kwenye Emperor of the sea, ila hiyo jumong kacheza vizuri mno. Itafute huto jutia mda wako ni episodes +80
nyinyi watu wawili (kee na mee) mumeanzisha vita na mnywa urojo, mumenifanya nitafute PC nije niwatie adabu kama mpemba yule na basi la abiria
teh teh teh
=========================
kwa nini uhusika wake ulikuboa big boss?
basi kiupande wangu uhusika wa
yeom mun ulikuwa ni bora zaidi kuliko husika nyenginezo alizowahi kuigiza.
- kama nayahisi maumivu yake yaliotawala nafsini mwake mpaka muda huu (ndio raha ya sanaa bwanaa, inakuhamisha kwa lazima)
- muhanga wa mapenzi, what a sacrifice
- hakuwahi kuwa na rafiki wa kumfanya ajisikie faraja na amani ya kuwepo duniani, hata huyo rafiki aliyempata kwa muda mfupi walijikuta wakiwa kwenye majaliwa tofauti
- si wanaume pekee wanaopewa limbwata, hata wasichana hufanyiwa huduma hiyo....mfano jang bogo na jung hwa agassi.
- bila ya yeom mun asingelikuwepo jumong
je wajua ilikuwaje?
Shall we say Song Il Kook and Han Jae Suk are fated with each other?
unamkumbuka yule mshikaji aliyeigiza lobbyist drama pembeni ya song il kook (anaitwa han jae suk), sasa ndiye aliyepaswa kuigiza uhusika wa yeom mun na tayari walishaanza kushoot picha za drama
turudi nyuma,
kuna drama inaitwa
All About Eve, humo ndani huyo bwana alikuwa ni muigizaji mkuu na song il kook alikuwa na uhusika mdogo mnooooooo ni kama sekunde chache (alikuwa hana heshima yeyote kwenye sanaa)
mwaka 2004 kuna skendo kubwa sana iligubika nchini korea, kuna waigizaji walicheza dili na madaktari au wapimaji ili wafoji taarifa zao za kiafya (wafeli vipimo) ili wasiende jeshini kama sheria inavyotaka (millitary enlistment) na miongoni mwa waigizaji hao alikuwemo han jae suk, song seung hun(rafiki yako wa kwenye black drama) na jang hyuk, pia inasemakana walilipa won milllion 200-300.
Kipindi hicho jamaa alishapata offer ya kushiriki emperor of the sea ila ndio hivyo tena ubuyu ulivyosambaa ilibidi aondolewe kwenye project na aende jeshini na hao wahuni wenziwe.
nani wakuziba nafasi yake kwa haraka bila ya kuathiri production drama?
wakati director na timu yake wanahangaika kumtafuta yeom mun mpya ndipo mwanamama chae sira (ameigiza madame jami humo ndani) akampendekeza song il kook kwa bwana director (sababu kubwa ni ile performance yake ndani ya terms of endearment walioigiza pamoja, chae aliamini jamaa akipewa nafasi ataweza kumudu uhusika huo).
kilichotokezea humo ndani imebaki kuwa ni historia.
wewe umeona wapi muigizaji msaidizi kushinda tuzo tatu kwenye drama moja huku muigizaji mkuu akishinda tuzo moja,
is it a coincidence?
hapana bwana.
emperor of the sea ndio iliomfanya song il kook ahame kutoka ulimwengu wa underdog to jibwa la juu akiwa na miaka 34.
- jumong ndio project yake ya kwanza kuigiza main character akiwa na miaka 35 (jamaa alistruggle sana)
- emperor of the sea ndio project iliomtambulisha kwenye ulimwengu wa A hallyu stars
- emperor of the sea imemfanya song apate offer nyingi za endorsement (matangazo ya biashara)
- emperor imemfanya song avune fans wengi duniani hususani wasichana
- hao wasichana wa kibongo waliompenda song kupitia jumong walichelewaaaaa......hahahahahahaaaaaaa chezea mama mwenye phd ya sheria.
alitongozwa siku moja tu, sheria kuleee.
sasa nikupe ubuyu mwengine(muliyataka na dada yako Numbisa).
jamaa anaunda kundi la watu wale introvert
kipindi anaanza mahusiano na mama daehan ndio nyakati za jumong kuwa trending.
bwana yeye alishapanga promise na mama kijacho amchumbie hoteli fulani na walishabooking kila kitu.
kwenda hotelini anakuta watu wamejaaa(unajua tena fans selfie jumong)
jamaa akamchumbia binti kwenye gari.
teh teh teh
=======================
kwa ufupi maisha ya song il kook ni funzo tosha kwetu ndio maana nampenda sana...
- hakutegemea umaarufu wa mama yake kutafuta ushawishi kwa wazalisha filamu na drama (mama yake alikuwa ni muigizaji mkubwa kabla hajaingia kwenye siasa kufuata nyayo za baba yake na babu yake)
- hakutegemea umaarufu wa babu (kim du han, tafuta historia ya huyu bwana) wala baba wa babu yake(general kim jwa jin mwanadamu aliyewatwanga wajapani, mwanadamu aliyepiga vita utumwa nchini korea kwa vitendo kwa kuwaachia huru zaidi ya familia makumi walizokuwa wakizimiliki na kuwapa ardhi, tafuta historia yake huyu jamaa umfahamu mpaka kuuliwa kwake)
- hakuwa na akili kubwa darasani (alifeli mara kwa mara na hajawahi kuficha) ila hakukata tamaa
- licha ya kupoteza ndoto yake ya kuwa mchoraji mkubwa lakini hakukata tamaa sehemu nyenginezo
- licha ya kuachwa nyuma na wenzake hakukata tamaaa hata kidogo, song alifanya mtihani wa kuigiza akiwa na miaka 27, hakuwa na talent ila alipewa umbile na ameendelea kulitumia ipasavyo.
huyu ndiye mwanadamu aliyemshauri song il kook ajaribu fani ya uigizaji,
yoo dong geun alikuwa ni kama mtu wa karibu na mama yake song il kook kwenye tasnia ya sanaa.
musinichokoze tena nikiwa na hasira za halima na rashidi