Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Mkuu andika hizo za jeseon nataia kuzijua aisee Mr daemushin
 
@Damushin nimemaliza kumtazama ha hyun woo kwenye mask singer doh sio poa Yule binaadam

Naamin walimchoka au nae alichoka, Yule alomtoa hakuwa mkali kiivo kuzid Yule dada( nshawasahau)
basi itakuwa walichokana, mtu kama yule unamshindaje?
lazima uwe gwiji kuliko yeye, waimbaji wa korea pamoja na televisheni show zao usiziendekeze sana kama tonge ya pilau kwa muhindi, khofu yangu watakuja kukulaza na njaa.
huo ndio ushauri wangu
 
New Drama Lost Ina Mahadhi Ya My Mister (Najua We Nishabiki Namba Moja Wa Hii) Unaeza Angalia Na hii Pia Japo Iko Nzito Na Emotional.
Lost drama yaelekea kunishinda, episode 1 nimeiangalia kwa dakika 30 na hatimaye nikaamua kusimama ndipo nikazitupa kwenye recycle bin episode zote 4 zilizobakia, (sijajua kama nitaziangalia huko mbeleni au ni kuzifuta kabisa)

maisha ya yule ahjumaa (jina lake halisi ni jeon do yeon) yananiacha na taathira kubwa sana ndani ya kiwiliwili changu bila ya kujali utofauti wa jinsi zetu. Akijiangalia umri umekwenda kwa kasi kubwa kama muangaza, vijana wadogo na wakubwa wamtuma yeye na kumkejeli kwa maneno ya dharau, msongo wa mawazo wamtafuna yeye na kumuacha na maumivu makali zaidi ya sumu ya nyoka inayotembea kwenye mishipa ya mwilini, ndoa yake nayo tafarani tupu na wazazi wake umasikini wazidi kuwatafuna. Ana kazi kubwa sana ya kuitafuta furaha pamoja na pumziko la moyo

yule mvulana (ryu jun yeol) mwenzangu naye ni tafrani tupu, mji wote autembea yeye kama gari ya ambulance inayotafuta mgonjwa wa dharura, sababu hataki kuonekana wa ovyo, miaka 30 yamnyemelea lakini hana alichokikamilisha wakati wapo vijana mfano wake yeye kiumri wameshalivuka daraja la umasikini.

bado tu wataka niiangalie drama hiyo inayonasibihiana na maisha yangu?
kwa sasa nasema Hapana, kwa sasa nahitaji zaidi kuangalia drama zenye sifa ya upepo na sitaki kuangalia drama zenye sifa ya kovu ya kidonda.

upepo ukishapita haurudi, kovu ya kidonda utabaki nayo labda utumie tiba maalumu kama zipo.
mambo ya kukaa muda wote nayawaza matukio ya kwenye drama sitaki.
ngoja tuone, pengine huko mbele naweza kuirudia
 
kilingeni 2021, mpaka tarehe ya leo hizi ndio drama nilizoziangalia kwa ukamilifu

  1. My sassy girl
  2. Temptation
  3. Second to last love
  4. Good doctor
  5. I have a lover
  6. One warm word
  7. Jewel in the palace
  8. Undercover - 2021
  9. Taxi driver -2021
  10. 3 days
  11. Mine -2021
  12. Rain or shine
  13. The great seer
  14. Master’s sun
  15. Hospital playlist - 2021
  16. Move to heaven - 2021
  17. memory
  18. the good wife
  19. the devil judge -2021
  20. you are my spring -2021
  21. mouse -2021
  22. the road the tragedy of one -2021
  23. hur jun
  24. sangdo
  25. DP -2021
 
@Damushin nimemaliza kumtazama ha hyun woo kwenye mask singer doh sio poa Yule binaadam

Naamin walimchoka au nae alichoka, Yule alomtoa hakuwa mkali kiivo kuzid Yule dada( nshawasahau)
uliwahi kufuatilia fantastic duo miaka minne nyuma?
assignment nyengine hiyo

huyo bwana muimbaji anaitwa lee moon sae, amezaliwa miaka 62 iliopita lakini chakula chake si chipsi kavu.
wimbo unaitwa only her laughter, ameuimba mwaka 1987.........huyo binti hakuwa na nia ya kuzaliwa

Fantastic Duo is a South Korean television show where fans can sing a duet with their favorite singer using their cell phones.
 
Leo nimezikumbuka drama ambazo nimewahi na zikanikonga moyo mpaka leo sitaweza kuzisahau.

East of Eden
The Giant (korean drama)
Hidden Identity
Iris
Athena
Hidden roots
Goodbye Mr Black
Goo family book
I'm sorry I love you.
Scarlett heart.
The clowned crown.
Vagabond.

Hizi movie nazipenda sana.
 
Ndomna Nikatanguliza Kua Ni Drama Ambayo ni too Dark Na too Emotional.

Ni Sie Magwiji Ndo Zetu Hizi (Sijui Kwanini Napenda Aina Hii Ya Drama Ama Movie).

Nikiangalia Ivyi Kuna Sehemu Inanipeleka Na Hasa Nikishatoka Chozi Najipiga Kifuani Nakujisemea Mapambano Yaendelea Futa Chozi Hauko Peke Yako.

Ila Una Maneno Sana..
 
basi itakuwa walichokana, mtu kama yule unamshindaje?
lazima uwe gwiji kuliko yeye, waimbaji wa korea pamoja na televisheni show zao usiziendekeze sana kama tonge ya pilau kwa muhindi, khofu yangu watakuja kukulaza na njaa.
huo ndio ushauri wangu
Basi Kwa hali Nilo nayo nilale tu njaaa
Hii niko nayo hadi nimalize episode zote niende nao sambamba

Hivi bongo hamna matajiri wa kufranchise hii kitu

Naisubiri na variety show ya 99'ers, ndo utakua ugonjwa mpya.

Miaka miwili nyuma nlikua sielewagi mkisema ost , saiv YouTube nashinda kuzitazama hizo na nyimbo za kikorea
 
Sijawah niongezee tu hizo assignment niwe mkorea kamili.

Natii kuifatilia hii pia kwenye plan ya variety
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…