Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwenye ile series ya CLASH LANDING ON YOU, naona kama wasouth korea wameishushia sana heshima North Korea, yani wameonyesha kama watu wa North ni washamba sana na ni kama developing country kabisa.

Nawaza kama haikuawahi kuleta Conflicts.
 
Kwenye ile series ya CLASH LANDING ON YOU, naona kama wasouth korea wameishushia sana heshima North Korea, yani wameonyesha kama watu wa North ni washamba sana na ni kama developing country kabisa.

Nawaza kama haikuawahi kuleta Conflicts.

Ila drama nyingi zao huwa wanaonyesha kama north ni wakukunja au dhihaka flan hivi.

Atleast ile escape from mogadishu movie

Hata variety utan wao kwa wale defectors mmnh
 
Shangazi utakapokuwa na nafasi nakuomba uniandikie japo kwa ufupi hizo tips zikiwemo application munazotumia kwa dhumuni la kupata huduma ya mtandao wa internet bure.

nahisi uzito kurudi kurasa za nyuma na kusoma comment mulizojadili hii ishu..
nakusubiri kama huna ban.

kuna mtu wangu wa karibu anahitaji, amechoka kurambwa bando.

mimi bado ni mshamba wa smartphone
 
kiupande wangu namchukulia yi seong gye ni mfano wa mtawala wa muda (regent) wa tawala fulani, kwa kuziangalia hizi simulizi za drama takribani drama zote zinazogusia maisha yake zinatuonyesha zaidi ushujaa wake wa kuongoza wanajeshi kuliko ushujaa wake wa kulisimamia a kuliongoza ipasavyo taifa changa mfano wa joseon ambalo limetokanwa na sadaka za damu za watu wengi.

maamuzi yake yalitokanwa zaidi na fikra za kikundi fulani cha wanasiasa au wandani wake wenye maslahi binafsi juu ya ajenda husika wanayoipigania kuliko kuangalia taathira zitakazojitokeza siku za mbeleni jambo lililopelekea aonekane kuwa ni mfalme dhaifu ila si general dhaifu

bang won ndiye aliyejenga misingi ya muda mrefu iliopelekea taifa hilo liweze kudumu kwa karne kadhaa, kwani hakuona shida kuchukua uamuzi mgumu wenye maslahi na taifa kwa uliopo au ujao na hiyo ndio sifa ya kiongozi.

tunafanya makosa makubwa sana kuusifia utawala wa mfalme sejong bila ya kuonyesha heshima ya kilichofanywa na mtangulizi wake.
bang won alipaswa aitwe mfalme wa kwanza wa joseon ila ndio hivyo kila zama na watu wake.
 
Lee Bang Won, ni ana ukatili sana
Nimetokea kumkubali sana lee bang won situation zimemforce hadi awe vile sio kuwa anapenda yale mambo kuua kila anaziba njia yake ilikuwa ina m pain sana ila atafanyaje anaona anakwamisha kabisa

Sio ajabu alidumu sana madarakani hadi alimpokuja mkabidhi madarska sejong the great
 
Wiki kadhaa nyuma nilikua natumia ha tunnel plus files unapata groups za telegram sema stock imejaa nimetulia kwa wiretun kuperuzi tu zote unatumia ttcl. Adownload playstore wiretun haiitaji files(anaweza tumia kwa tigo au ttcl)

Kulikua na vpn nyingi sema wabongo hawana dogo si wakaenda kujitapa page za tigo ,airtel kuwa hawanunui bando wanapata bure kwa vpn. Vpn nyingi zimefungwa.
 
Zamani nilikuwa naangalia kdrama kupitia youtube lkn sasa hivi napata changamoto kuzipata mara hazionekani Mara zipo episode 4 zinaisha ukitafuta nyingine unakuta ni vipande tu vya dk 5 nyie mnaziangalizia wapi wakuu

Nimeona hiyo hapo juu king of tears Lee bang.... Nikasema niende youtube haipo
 
YouTube hupati kitu siku hizi mambo ya copyrights utabahatishans

Zama nkiri.com au kimoitv.com au naijanet.com
 
vp mmeamkaje humu?
naomba msaada kuna series moja ya kikorea ni historical drama nimeisahau jina ila ni ya muda kidogo kwa mwenye kuijua nikumbushe inaitwaje,
katika familia moja ya kifalme kuna msikaji alikuwa na kovu usoni so alikuwa anavaa mask upande mmoja wa uso maana hakutaka kuonekana, jamaa alikuwa serious sana sio mtu wa kuongeaongea ila alikuwa anapiga kinoma noma na kama sijakosea nguo alizokuwa anavaa ni rangi nyeusi, mwenye kuijua jina lake tafadhali naomba anikumbushe !!!!
 
Labda legendary daemushin atakusaidia
 
Inaitwa Moon Lovers: Scarlet Heart Ryeo
 
Kwenye ile series ya CLASH LANDING ON YOU, naona kama wasouth korea wameishushia sana heshima North Korea, yani wameonyesha kama watu wa North ni washamba sana na ni kama developing country kabisa.

Nawaza kama haikuawahi kuleta Conflicts.
Yaani umewaza kama mimi, sijui hata walijisikiaje, wamedhalilishwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…