mwishoni mwa episode 20
lady min (mke wa bang won) na kabila lake(min clan) ni suala la muda tu kabla na wao hawajaingia kwenye mdomo wa mamba, bang won amekuja na mkakati wa kuondoa vikosi binafsi vya ulinzi vinavyomilikiwa na makabila pamoja na familia maalum(tumeona huko nyuma mfalme taejo aliwatunuku wanawe wanajeshi kwa ushauri wa malikia aliyekuwa na lengo la kuwatengenezea mazingira ya kupumbazika na kufanya uhaini). hapo nyuma sambong alikuja na wazo la kufuta wanajeshi binafsi(military disbandment) lakini akapata upinzani mkali kutoka kwa lee bang won, leo hii bang won anataka kupita mule mule alimopitia adui yake sambong ndio maana kabila analotokea mke wake hawamuelewi juu ya mpango wake huo na khofu yao bila ya shaka wanaamini kutokuwa na majeshi ya kulinda kabila lao ni sawa na kuchomolewa maarifa na ufahamu kwenye vichwa vyao na watakuwa chawa wa mfalme milele, wakati baba mkwe dhumuni lake haswa ni kuitawala joseon kupitia sketi ya mwanawe wa kike (wanaume wa scotland nao wanavaa sketi) huku wakipata msaada wa kiulinzi na kifedha zitakazowawezesha kutawala nafasi zote nyeti za kiserikali.wakati yeye anawaza hivyo upande wa pili anaamini kwenye uendeshwaji wa serikali itakayoongozwa na nguvu ya mtu mmoja (hata kuwa kama baba yake aliyetawaliwa zaidi na sambong pamoja na malikia sindeok). lady min anamwambia bang won nyakati za shida tulikuwa pamoja, tulicheka pamoja pale tulipopatwa na jambo la kufurahisha, tulikejeliwa na kudhihakiwa pamoja. leo wachukua maamuzi muhimu ya kuongoza nchi peke yako, kama huwezi kuishawishi familia yangu juu ya mpango wako wa kuondoa majeshi binafsi basi nishawishi mimi, utakaponishawishi mimi ni sawa na kuwa umeishawishi familia yangu. hivi umesahau kuwa nusu ya mafanikio yako yametokanwa na mimi(akiwa na maana ya kabila lake).aigooo marehemu khadija baramia aliwahi kuimba wimbo wake wa taarab asilia..... njoo njoo mpenzi wangu njoo, rudisha yako imani wachochea moto ukija kuwaka mzimaji nani, eti lady min?....umeshasahau kuwa mume wako amewaua ndugu zake, amemfungia baba yake na kumuondoa ndani ya mji kaka yake. mara hii atazitafuta shingo za ndugu zako wawili na baba yako..... nilifikiri naongea na lady min. kumbe naongea na mkorea wa makunduchi. basi naambatanisha na samahani isiyoonyesha kujutia kosa langu.