Lax
JF-Expert Member
- Feb 10, 2022
- 4,740
- 7,179
Mo Palmo safi sana uyu mzee..tuachane na hizi hadithi za upendo.
=============
hivi wale wahindi wana mchekeshaji mwengine mwenye ubora kama johnny lever?
nimetoka kuimalizia project ya Dong Yi, jambo moja jengine kubwa lililonivutia humu ndani ni hii nguvu ya comedians
(wameonyesha uwezo mkubwa sana), kwa ufupi sikutegemea kumuona huyu mshkaji anayeitwa yeo ho min a.k.a oh yi from jumong drama
akiulainisha muda wangu kwa vituko vyake (sijawahi kumuona akiigiza comedy).
pembeni alikuwepo mo palmo
yule afande masharubu (ni mara yangu ya kwanza kumuona)
lee kwang soo
yule mzee aliyeigiza emperor of the sea
wenzetu wakorea sanaa yao itachukua muda sana kufifia na sababu kubwa hawa wavimba macho wamejaza utitiri mkubwa wa vipaji kwa kila eneo (sanaa yao haitegemei nguvu ya msanii fulani tofauti na wengineo)
ukitaka ahjummas wamejaa
ukitaka ahjussi wamejaa
ukitaka watoto kila siku wanazaliwa upya
ukitaka majambazi uchwara kila siku wanazaliwa
kongole kwao kwa huu uwekezajii walioufanya kwa miaka hii 20 ya mafanikio, safari ndio inaendelea na ni matumaini yangu wakorea hawatobweteka
🙏🙏🙏🙏🙏
nimekumbuka scene moja wadau wa south faction wapo kwenye kikao wanatoa point Mo palmo yy ikifika zamu yake anasema "older brother" tu. (kwa kikorea spelling zimepita kushoto)