hii laana ya thread hata mimi pia inaendelea kuniandama na kila ninapojaribu kuitelekeza huwa nashindwa, baadhi ya nyakati naweza kutafuta kisingizio chochote ili nisiweze kutembelea humu ndani lakini wapiiii naishia kuchukua wiki moja hadi mbili then narudi uchawini.
baadhi ya nyakati nikiwa likizoni nakutana na notification za wadau mbali mbali hivyo basi nashindwa kuwapuuzia,
baadhi ya nyakati naandika then nafuta, comment zangu nyingi za mwanzoni nimeshazifuta.
kali zaidi kuna siku nilikwishafikia maamuzi ya kuwablock baadhi ya wadau muhimu wanaotembelea hii thread, niliamini kufanya hivyo kutaniwezesha kutokuwa na mawazo ya kutembelea humu ndani, nikatafakari nikaona yatakuwa ni maamuzi ya kipumbavu zaidi ulimwenguni.
nilichojifunza ya kwamba ili niweze kuachana rasmi na ulimwengu wa korea ni lazima nipate starehe nyengine itakayoniburudisha zaidi, bahati mbaya kwa sasa sijakutana na starehe pendwa kama hiyo.
hivyo basi mkuu endelea kuwa mlevi wa hii thread mpaka mapafu yako yaharibike au peleka malalamiko JF uzi huu usiwe pinned.