hivi ulifikiri hii siku nitaisahau?
heri ya kuzaliwa iwe juu yako na natumai hukunidanganya kwa njia ya keyboard kwa sababu sidhani kama una tabia hiyo ya kuongopa,
Asubuhi nilipoamka jambo kwanza nililiangalia jua llililokuwa linajiandaa kuchomoza kwa dhumuni la kuiangaza dunia na vilivyomo ndani yake, nikabaki najisemea huenda yule binti aliyezaliwa tarehe kama ya leo miaka telee iliopita hata wazazi wake walikuwa na ndoto ya kumuona binti yao pindi atakapopevuka awe na uwezo wa kuiangaza dunia yake na wenzake kwa kutumia kifikra zake zitakazoongozwa zaidi na utulivu wa nafsi iliojaa furaha ndani yake.
kama mpaka leo umeshindwa kuiangaza dunia yako unaonaje ukaianza siku ya leo kwa kufikiria zaidi yajayo kuliko matukio yale yote yaliopita yaliokufanya ushindwe kuing'arisha dunia kwa mikono yako miwili, kama aliweza Oprah Winfrey aliyekuwa na historia mbovu pengine kuliko wewe kwa nini iwe vigumu kiupande wako?
unadhani Mungu anakuchukia?
unadhani Mungu amekupangia uwe hivyo maisha yako yote?
unadhani Mungu amekupangia uteswe na wajinga wajinga kama daemusin kihisia?
hapana hapana sitaki kuamini hivyo kwa sababu Mungu hana wivu wa kijinga jinga na roho mbaya ya mafanikio kama aliyonayo daemusin.
tafadhali anza upya kuanzia leo naamini kwa nguvu na uwezo wakebwana Mungu hatakupuuza.
hizi zawadi ninazokutumia usije ukazivamia zote kwa siku kama mfungwa aliyelazwa na njaa kwa wiki nzima, kufanya hivyo utalipelekea tumbo lako liwe kubwa kama pipa la lami.
🍏🍎🍐🍊🍋🍌🍉🍇🍓🍈🥦🥑🍅🍅🥝🥥🍍🥭🍑🍒🥬🥒🌶🥕🥐🥖🍞🍟🍔🌭🍤🥙🌮🌯🥗🍚
japokuwa ulimtuma dada yako
Prishaz aje anirushie kichambo na vitisho juu siku ile kama mwanamume niliyefumaniwa na
mbuzi meee kwa sababu dhaifu ya kukuita ahjummaaa naomba ufahamu ya kwamba mjinga mimi sikuchukia lile tendo na kiukweli sitoacha kukuita ahjummaaa mpaka itakapofika siku ya harusi yako na yule niliyemuota usingizini mwenye upara kichwani kama zidane 🏇🏇🏇.
mfikishie taarifa hii yule dada yako aliyekuja na mishale yake kama jumong
View attachment 1242797 pamoja na sindano kama daktari wa wanyama
View attachment 1242798, mwambie mimi ni mbabe na mtemi nisiyeogopa hata hashuo la kuku mzazi kuliko
gogo la muembe 2020.
==============================================
dah! viumbe wengine tuna bahati mbaya kweli utadhani tumezaliwa na bundi, tunapoteza pambano tukiwa kwenye ndoto na hata tukiwa macho.
nimewasilisha zawadi nyengine kwako kwa njia ya burudani, yawezekana haya maneno yananihusu mimi au wewe kwa njia tofauti japokuwa kwa akili ya haraka unaweza kudhani yanamhusu mwanamke pekee aliyemtelekeza jamaa
lee moon sae = Only The Sound Of Her Laughter
huu wimbo ameuimba mnamo mwaka 1987 ikiwa ni album yake ya 4, ina maana hata hicho kibinti hakikuwa na matumaini ya kuzaliwa, pengine wazazi wake walikuwa hawajakutana vichochoroni kama mbuzi.
HAPPY BIRTHDAY aminas