wasemaje mjaluo wewe utokae pyongyang (lafudhi ya kipemba)?
=================
- yeon gaesomun alikuwa ni miongoni mwa mashujaa wa goguryeo wa kukumbukwa na vizazi (rejea ushindi wake dhidi ya Tang)
- yeon gaesomun pia alikuwa ni chanzo cha kuanguka kwa goguryeo kutokana na maamuzi yake ya ovyo (kwani alishindwa kusoma alama za nyakati, pia alishindwa kujenga misingi sahihi itakayoifanya foundation ya gogoryeo mpya iendelee kudumu angalau kwa karne moja) historia ya bwana yeon gaesomun itaendelea kuleta mgawanyiko wa kifikra mpaka ulimwengu utakapokwisha.
===============
mara nyingi wale wanaojivika muamvuli wa kuwa na uchungu na nchi husika ndiyo huishia kuwa madikteta wa fikra na matendo (yawe ni mema au ovu).
==============
historia yatufunza na kutukumbusha:
madaraka ni ugonjwa hatari sana kuliko ugonjwa wa kisukari ambao hukufanya ukatwe kila kiungo kilichoathirika zaidi.
na nchi yoyote itakayoendeshwa bila ya kuwepo kwa maridhiano kati ya pande zinazokinzana kimtazamo haiwezi kufanikwa kwa jambo lolote na hilo ndio liliifanya goguryeo ijikute kwenye wakati mgumu miaka yake ya mwishoni.
- kulikuwa na upande ambao ulitaka goguryeo ianzishe mahusiano ya kirafiki na Tang kama alivyofanya kim chunchu wa SILLA (pro tang) ili kuondoa minyukano ya kila mara kati ya mataifa hayo mawili, upande huo uliongozwa na koo zenye nguvu pamoja na mfalme , waliamini goguryeo na Tang wakiwa marafiki basi mahusiano ya kisiasa, kitamaduni na kibiashara yatakuwa makubwa zaidi, kama tunavyofahamu china ndio kituo cha biashara duniani, siasa na elimu kwa kanda ya ASIA.
- upande wa pili ni wale ambao walipinga goguryeo wasiwe na urafiki wa karibu na Tang kwa sababu waliamini kuikaribisha TANG ni hatari zaidi kwa maslahi ya goguryeo kuendelea kuwepo kwa sababu tawala zote za china ziliinyemelea goguryeo kwenye vita nyingi (rejea vita ya HAN enzi za jumong, SUI DYNASTY walipochapwa na general eulji mundeok, gwanggaeto dhidi ya ukoo wa murong xi n.k) hawa waliamini goguryeo bado ina nguvu ya kujilinda dhidi ya vitisho vya mabeberu.
=====================
wenye movie zao watuhadithia
baada ya sintofahamu ya muda mrefu na kila upande kudhamiria kusambaratishana ndipo siku moja ya mwaka 642 shujaa yeon gaesomun na wafuasi wake walifanya sherehe kwa ajili ya kumpongeza yeon gaesomun kuchaguliwa kuwa governor wa mashariki. kwenye sherehe hizo aliwaalika wapinzani wake takribani 100 na ndipo akawaua wote kwenye sherehe hiyo na baadae kuelekea ikulu ambako alimuua mfalme
yeongnyu. baadae yeon gae somun akamchagua mpwa wa mfalme ambaye ni mfalme
bojang awe mfalme wa 28 wa goguryeo ambaye ndie mtawala wa mwisho.
yeon gae somun akajipa cheo cha
mangniji (superior commander) hivyo basi goguryeo ikawa inaendeshwa kwa akili ya mtu mmoja(de facto control) na mfalme alibaki kuwa kama mbwa koko. uwepo wa yeon gaesomun kama mkuu wa nchi kulizidi kuchochea mgogoro wa Tang na goguryeo na ndipo lishimin akajaribu kuivamia goguryeo lakini mara zote alishindwa vibaya sana.
moja kati ya ushindi mkubwa wa yeon gaesomun ni kwenye vita ya sasu river mnamo 662 baada ya kumdhibiti general Pang Xiaotai na jeshi lake, kwenye vita hiyo alimuua pang xiaotai na pia aliwachinja watoto wake 13. vita za mara kwa mara zilipelekea uchumi wa goguryeo kudorora na miaka mitatu baadae yeon gae somun alifariki dunia.
kifo cha yeon gaesomun kilichochea anguko la goguryeo kwa sababu watoto wake waliwaniana madaraka na kusahau dhamira na lengo kuu la baba yao kuwa mangniji.
=================