Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Wa ʿalaykumu s-salam (وَعَلَيْكُمُ ٱلسَّلَامُ)
na wewe pia amani iwe juu yako
==========
waendeleaje huko uliko pyeongyang, anayetawala huko ni kaka au dada?
kuna wajinga wanadanganyana kila siku, wengine wanasema dada mtu kawa kaka mtu kasoro sehemu ya siri tu amemuachia mapanki.
hebu tupe kinachojiri huko.
Yule Dada kasoma na Kaka yake Mr. Chairman( Kim) Swisland. na anaonekana kuwa mjeuri zaidi yake.
Haya nipe habari ninyi washirika wa Mabepari( Mabeberu)
 
Kama ni kofi tumepigwa lile la shavu na likafikia sehemu husika. Sio kwa maumivu haya. Mmmh sasa sie wavuta movies hali imekua hivi je wafanya online business kazi wanayo. Nawasubiria voda kesho sijui watapunguza mpaka wapi
Airtel huduma yao ya internet si ya uhakika kwa huku nilipo, baadhi ya siku naipata vizuri sana huduma yao ila siku nyengine naingia hasara. bei mpya za vifurushi haziendani kabisa na uhalisia wa maisha ya watanzania walio wengi, sidhani kama serikali ilifanya tathmini ya kina juu ya uamuzi huu.
 
jamani amkeni, amkeni wizara mpya ishafanya ya kwake.
sasa ni rasmi tumestaafishwa kufuatilia movies, series na drama kwa njia ya mtandao.
  1. bando la usiku limeondoshwa
  2. kifurushi cha siku kwa GB 1 kimeondoshwa
  3. vifurushi vyenginevyo vimerambwa mnoooo
halotel hongereni kwa hichi mulichotufanyia
============

upande wa zantel kwa huku zanzibar
kutoka GB 3 kwa siku kwa shilingi 2000 hadi mb 900 kwa shilingi 2000
na mabadiliko mengineo
===========

watu wa Airtel na vodacom vipi huko tunaweza kuhamia?
sisi wengine tunahitaji japo kifurushi cha usiku
=========
kikao kimeanza rasmi chenye lengo la kujadili haya mabadiliko, kama huamini ingia kwenye menu yako.
aminas mlevi mwenzangu uliyebobea
Numbisa mlinzi mwenzangu wa usiku tunatokaje
talnam mfukuza upepo kimya kimya
missyrose mlevi mwengine wa korea
Great Conqueror huko kaskazini huduma zenu ni nzuri?
na malegendary wengineo mukipata wasaa muhudhurie kwenye kikao

dah! bye bye wakorea?
Jamaan
 
Mmmh maskini uhondo wa you tube bye bye. Ni mwendo wa kurudi kwa wachomesha cd kupata vikorea japo siku hizi vimetafsiriwa na picha mbovu balaa.

Hapa nasubiria mabadiliko ya voda kesho huku nikiset mitambo ya kulinda usiku kuagana na airtel kama nao watafuta kifurshi cha usiku nimalizie family drama ya wang's family

Kuna kioindi nilikua naenda kwa mwendo huo ila bado bando la gb moja likawa halitoshi kwa sasa sijui itakuwaje
kwa ufupi hakuna atakayesalimika na huu mbinyo, kuna baadhi ya dhoruba/changamoto zinapokuja hazichagui status ya mwanadamu na moja wapo ni hili suala la teknolojia ya mawasiliano.

kwa sasa njia pekee ya kudumu na hilo bando lako dogo ni kuperuzi JF na tovuti nyenginezo zisizohusuiana na uangaliaji wa video ukiwa online.

mtihani wa makusudi umetuingia
 
Kwenye CD pagumu maana wanaikata kata.ntahamia kwa wachina wana vidrama hadi vya mb 50 ila quality wameiwekeza kwenye kusambaza corona duniani
hapo youtube wengine itatulazimu tutembelee huku hesabu zikiwa mbele zaidi, unawaza kissasian na video quality yao huku mfukoni una GB 1 ya buku 2.

upande wa kununua CD sifikirii kurudi tena
 
Habari, tunakufahamisha, Tutasitisha Ofa ya ASUBUHI kuanzia 2/4/2021. Endelea kufurahia vifurushi bora, Piga*149*01#>Nunua vifurushi. Vigezo kuzingatiwa

Mmh utadhani walikua wanatoa gb kumbe mb 50 na sekunde za kuongea na visms 5
 
Kama una stock ya kutosha hongera sana.
ngoja niendelee kuziangalia hizi nilizokwishazipakua baadae nitajua cha kufanya.
kwa mwendo huu nitaendeleza mfumo wa kutoangalia 2021 drama labda Airtel waendelee kuwa msaada japokuwa network haitabiriki.
 
Back
Top Bottom