Bukondamoyo
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 458
- 490
Naipataje squid game
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nenda nkiri.comNaipataje squid game
usihangaike ni utopolo tu mle ndaniNaipataje squid game
Utopolo wake ukoje?usihangaike ni utopolo tu mle ndani
Young pal umeshaangalia? Doctor stranger je? Jaribu hizoBaada ya kuimaliza hospital playlist najikuta nataka kutzama medical drama zote [emoji91][emoji3]
Ahsante mkuu ngoja nianze na hyo Doctor StrangerYoung pal umeshaangalia? Doctor stranger je? Jaribu hizo
Napenda sana series zenye maadhi ya namna hiyo. Ukiachana na hizo ulizotaja, ipo pia HIDDEN IDENTITY.kwa sanaa ya korea zipo chache sana zenye maudhui mfano wa the veil, ninazozikumbuka kwa haraka ni
- iris 1
- iris 2
- athena goddess of war
Yan kuna ka feeling hata ikitajwa vipi unasikia raha kufahamikawatanzania munaitwa huku, munafuga wapelelezi wanaoitwa wakimbizi ndani ya nchi yenu wanaojificha kwenye mwamvuli wa ubalozi.
mwatutafutia balaaa ndani ya nchi yetu ya korea
teh teh teh
View attachment 1970763
Nimeicheki episode ya kwanza inaonekana ipo moto saa, jana numeivuta kupitia simu yangu na baadae nikitulia navuta nyingine hata mbili kwa leo.Mzee baba hiyo drama ni [emoji91][emoji91] hautajuta kabisa kupoteza mb zako alafu utakuja kunishukuru, baada ya kumaliza drama yangu nikawa nalazimisha kupata nyingine nzuri fortunately nimeipata hiyo na kizuri chake kwangu The Veil ndio best korea drama kwa mwaka Huu kwa upande wangu na pia imeshaingia kwenye list yangu ya best korean all time.Ni aina ya drama ambao mwanzo tu inapoanza unaona kabisa ni Kali na kizuri zaidi kila episode inapoisha unabaki na kimuemue Cha kucheki next episode.
Hatimae umeamua kuikubali I'd yako ya Innocent dependent .Ni website inaitwa nkiri.com unapata korean drama, Hollywood movies pamoja na series kwa mb ndogo Tena yenye video quality kubwa.Enjoy kijana anza tafuta korean drama moja hivi inaitwa " The Veil" ni ogoing drama ni Kali ile mbaya kama uliipenda Vagabond hii utaipenda zaidi ina story inayovutia, ina action ya nguvu mimi ni rafiki yako Innocent Dependent now natumia jina Hili SteveMollel
Hatimae umeamua kuikubali I'd yako ya Innocent dependent .Ni website inaitwa nkiri.com unapata korean drama, Hollywood movies pamoja na series kwa mb ndogo Tena yenye video quality kubwa.Enjoy kijana anza tafuta korean drama moja hivi inaitwa " The Veil" ni ogoing drama ni Kali ile mbaya kama uliipenda Vagabond hii utaipenda zaidi ina story inayovutia, ina action ya nguvu mimi ni rafiki yako Innocent Dependent now natumia jina Hili SteveMollel
Duh!, Huyo mzee kumbe ni konki kiasi hicho, ndio maana series zake, zinastori nzuri na hazichoshi.unaambiwa hakuna mwanadamu mgumu kufanya naye kazi kama director lee byung hoon (mzee ni mr perfect), hizi ni baadhi ya dondoo zinazomuhusu babu yetu lee byung hoon
tuanze na matengenezo ya Jewel in the palace drama (2003)
ushirikiano na muandishi Kim Young-hyun:
baada ya mapumziko ya muda mrefu director lee alirudi tena kufanya kazi ya utengenezaji wa drama mnamo mwaka 2000, lee alisimamia drama ya hur jun na sangdo ambazo ziliandikwa na muandishi anayeitwa Choi Wan Kyu, huyu bwana alikutana na balaa la director lee kupitia kazi yake ya hur jun, unaambiwa episode 1 ya hur jun alilazimika kuiandika mara 5 ndipo director lee akaikubali, muandishi choi akajiwekea nadhiri ya kutokufanya tena kazi na director lee ila cha ajabu baadae akabadili msimamo wake na hatimaye wakafanya tena kazi pamoja kupitia drama ya sangdo inayozungumzia maisha mfanya biashara tajiri kuwahi kutokea ndani ya joseon.
drama ya sangdo ilipangwa kuwa na episode 40 tu na si 50 kama tulivyohuhudia jambo hili lilizalisha mgogoro wa muda kwa muandishi Choi Wan Kyu ambaye kwa wakati huo alikuwa tayari ameshafikia makubaliano na kituo cha SBS ya kuandika drama inayoitwa ALL IN (hiyo drama aliigiza lee byung hun, song hye kyo, ji sung, han ji min), hii drama ya All In kwa wale wapenda ubuyu ilizalisha couple ya lee byung hun na song hye kyo ila baadae waliachana (kwa sababu fulani fulani, shutuma nazo zikazaliwa hususani dhidi ya lee byung, zee la maskendo).
wewe utakayesoma unapaswa ufahamu kuna director lee byung hoon na muigizaji anayeitwa lee byung hun (hao watu hawafanani).
muandishi choi wan kyu akaamua kumpa kazi ya kuandika episode 41 na 42 muandishi wa kike anayeitwa Kim Young-hyun, kutokana na ubora wa script unaambiwa mwanzoni director lee byung hakugundua mabadiliko yeyote ya kiuandishi (lee aliridhishwa na kazi ya mwanamama). Huyu mama kielimu alisomea masuala ya uchumi na baadae akawa ni muandishi anayerepoti taarifa za kiuchumi lakini baadae akaamua kugeuza ubavu wa malengo kwa kuhamia kwenye kazi ya uandishi wa drama (kipindi hicho alikuwa ni unknown).
kwa asiyemfahamu huyo mama licha ya kuandika jewel in the palace pia ameandika drama hizi (the great queen seondeok, arthdal chronicles, tree with deep roots, ballad of seodong).
baada ya kufahamiana naye japo kwa ufupi kupitia drama ya sangdo ndipo baadae wakaamua kufanya kazi kwa pamoja kupitia jewel in the palace drama.
kuchagua maudhui ya hadithi
director lee hupendelea zaidi kumtengeneza muigizaji mkuu akiwa tabaka la chini kimaisha na hii ni kwa sababu rekodi za kihistoria hazijaandika sana taarifa za watu wanaotokea tabaka hilo, hali hii humpa uhuru zaidi director lee kumuandaa muigizaji mkuu vile apendavyo yeye, pia hali hii husaidia sana kuepukika kwa migongano ya kihistoria (distortion of history).
kwa mfano huwezi kuandika stori ya maisha ya mfalme sejong halafu ukamfanya awe kilaza (wakati jambo la kusoma lilikuwa ni hobbies kwake tokea udogoni).
yeye na muandishi walikaa chini na kufikiria waandae hadithi itakayokwenda na dhima itakayokidhi hadithi ya dae jang geum, tukumbuke mwanzoni director lee byung hoon tayari alishaandika hadithi ya hur jun ambaye naye alikuwa ni daktari wa mfalme, hivyo walihitaji hadithi ya dae jang geum ambaye naye alikuwa daktari wa mfalme tena mwanamke bila ya hadithi yake kufanana na na Hur Jun drama.
ndipo wakapata wazo la kutumia maudhui ya chakula bora kuwa ni njia kuu ya kutibu magonjwa yanayomkabili mwanadamu, wazo hili mwanzoni lilipingwa sana na kituo cha MBC kwa sababu tofauti zikiwemo za gharama za kuandaa chakula, ubora wa vyakula vya royal pamoja na miiko yake, pia walikuwa na wasiwasi mkubwa huenda watazamaji wasifurahishwe na maudhui ya vyakula.
uchaguzi wa muigizaji mkuu (mkubwa)
director lee hapendi kufanya kazi na muigizaji mkuu asiyekuwa na uzoefu(nawakusudia wale waigizaji wanaochipukia),hii ni kwa sababu ya ugumu wa kuigiza historical drama(historical drama kwa kiasi kikubwa sana location zinazotumika ni outdoor), sababu nyengine kuu ni khofu ya kutokufanya vizuri kwa drama husika (fikiria drama ina episode takribani 40 halafu ndio inafanya vibaya kila wiki, kivyovyote kwa muigizaji anayeyafukuzia mafanikio atakuwa kwenye wakati mgumu sana sokoni kwani haitokuwa rahisi kwa waandishi pamoja na directors wengineo kumpa nafasi ya kuigiza tena uhusika mkuu).
kupitia drama ya jewel in the palace unaambiwa mwanadada lee young ae alishika nafasi ya 7 kati ya waigizaji wa kike waliokuwa wamelengwa kuigiza uhusika wa jang geum, kwa mara nyengine tena director lee byung hun alitamani kufanya kazi na mwanadada anayeitwa Song Yun-ah (kwa aliyeangalia K2 drama atakuwa anamfahamu) ambaye mwanzoni alishamkatalia mara mbili (hur jun drama na sangdo) hatimaye kwa mara nyengine tena binti akaikata ofa ya kuigiza nafasi ya dae jang geum hiyo ikiwa ni mara ya tatu (baada ya hapo hakumtafuta tena)
![]()
director lee hakupenda kufanya kazi na lee young ae kwa sababu kwa wakati huo tayari mwanadada huyo alishakuwa maarufu nchini korea hivyo alikhofia lee young ae ataikataa ofa ya kuigiza sageuk (historical drama) na ni kweli mwanzoni binti alikataa lakini mbeleni akakubali kubeba uhusika wa dae jang geum (kilichofuata kimebaki kuwa ni historia kwake)
uchaguzi wa muigizaji mkuu (mdogo)
ili kuifanya hii drama itofautiane hur jun, director lee na timu yake waliamua kuyaanzisha maisha ya dae jang geum tokea akiwa ni msichana mdogo na tofauti ilivyokuwa kwa dokta hur jun aliyeanzia maisha yake akiwa ni kijana mwenye nguvu.
muigizaji anayeitwa Jo Chong Un ndiye aliyepata nafasi ya kubeba uhusika wa dae jang geum licha ya kwamba alikosa baadhi ya vigezo vilivyowekwa (walitaka muigizaji mwenye ufanano na lee young ae, ideally na pia awe na kipaji cha uigizaji).
director lee alivutiwa sana na binti kwa uwezo wake wa kuigiza halafu pia hakuwa akifanya makosa (hatimaye uhusika wa dae jang geum mdogo uliongezwa kwa episode 1 zaidi, mwanzoni zilipangwa episode 4 tu ndio zionyeshe maisha yake akiwa mdogo).
filamu (kurekodi drama) pamoja na uchaguzi wa location
kikawaida historical drama inaweza hata kuchukua hata miezi nane mpaka kukamilika kwake (nazungumzia zile za kibabe zenye episode nyingi), halafu ndio hivyo locations mara nyingi zinakuwa ni nje hivyo basi waigizaji wanakutana na adhabu ya hali ya hewa either baridi kali nyakati za usiku au jua kali. unaambiwa licha ya drama hii kufikia hatua ya kuangaliwa na 50% ya wakorea wote lakini bado director lee hakubweteka na mafanikio, zipo baadhi ya script za episode husika zilifanyiwa marejeo au marekebisho takribani mara sita mpaka muandishi wa drama hii akapatwa na msongo wa mawazo (kila anapojaribu kuandika director lee anaikataa script husika).
hali hiyo pia huzalisha uchovu kwa waigizaji na hata kwa director mwenyewe, kwa mfano kuna scene fulani ilimuhusu Jang Geum na Lord Min walipoondoka ikulu, walijikuta wanatembea masafa marefu kwenye milima bila ya director kusema cut (akiwa na maana scene imekamilika), kumbe director lee alipatwa na usingizi wakati anaendelea na kazi na ilibidi msaidizi wake ndio amuamshe.
kwa mfano episode 22 tulishuhudia dae jang geum na yule mlezi wake Court Lady Jeong wakipewa adhabu kwa kuondolewa kwenye jumba la kifalme na hatimaye wakiwa njiani court lady jeong alifariki, tukio la msiba wake lilichukua takribani dakika 3 lakini kiuhalisi mpaka kukamilika mchakato mzima wa kushoot tukio lile yalipotea takribani masaa 10, kwanza iliwachukua masaa matano kwa kazi ya kutembea milimani mpaka kufikia eneo husika linalopaswa kurekodiwa tukio lile na baadae walitumia takribani saa 1 kurekodi scene ile (changamoto nyengine za hali ya hewa huko milimani zilizidi kusababisha muda mwingi kupotea)
finally director lee hapendi kufanya kazi na muigizaji mkuu zaidi ya mara moja
Baada ya Jumong inafuatia the Land of Wind kisha Princess Jamyung.Mtiririko wa Series ya Jumong upoje wadau.
Nataka kuangalia muendelezo wa Jumong.
Ni series zipi zinafuata kwa mtiririko baada ya Jumong
Haipo kama inavyopewa promo but inatazamika..aitafuteusihangaike ni utopolo tu mle ndani
Imewahi kuisha yani mtu unabaki na hamuSquid games pressure imefanya niimalize fasta
Nzuri kila nikifikiria jinsi michezo ya utoto ilivyonipiga chenga (mchangizi) ndo nikutane nayo ukubwani, mchezo wa kwanza tu mi nshakufa [emoji16][emoji16]
Sema Yule Mzee kasema kweli ' Maskin na tajir sana hawana tofauti, watafanya chochote kuitafuta furaha/pesa
Kama ghafla yaniImewahi kuisha yani mtu unabaki na hamu