Reflection of You / Person Who Looks Like You drama: episode 1 imenivutia sana licha ya pace yake kuwa ni ndogo, ni aina ya zile drama unazoangalia kwa nusu saa baadae unatafuta kitanda, sports au chakula kilipo. Lengo kuu ni kuitafuta nguvu mpya itakayoshajihisha au kukuhamasisha kuendelea tena kuingalia project husika. Ni drama zinazohitaji uvumilivu kwa sababu ya upungufu wa matukio yatakayokufanya muda wote utamani kuyashuhudia.
Ngoja niisubirie episode 2, kwa masikitiko hii drama sijafanikiwa kuiona kwenye tovuti ya nkiri (imenibidi nirudi dramanice)
====================
Niwakumbushe tu huyu
gong hyu jung ana miaka 50, wakorea walivyo na maajabu yanayochangizwa zaidi na matunzo yao ya ngozi pamoja na ulaji wao mwanamke mwenye miaka 50 unaweza kumwita dada (binti), huku kwetu upembani na ungujani mwanamke mwenye miaka 50 anaitwa bibi (kashaozesha mwanawe, keshajukuu).
ngozi imeshakunjana kama chapati ya bifatuma kibuno kwa sababu ya ukosefu wa matunzo ya mwili wake kwa kuanzia na lishe yake (kushiba hashibi, atapata nguvu ya kununua vipodozi), na mwanaume mwenyewe mfano wa daemushin muda wote yupo kibarazani anakunywa supu ya pweza lakini fedha ya kununua lotion kwa mkewe hana.
====================
Gyeoul (shin hyun bin) where are you?
nakuona humu ndani jinsi unavyomtambisha dada mkubwa (mishil), inaonekana kuna mkasa mkubwa sana unaowahusu wawili kati yenu uliotokea miaka ya nyuma.
=====================
Jeong Hui-Ju (Ko Hyun-Jung) had a poor and fierce time during her youthful days. She is now a successful painter and essayist. Her husband is the successor of a hospital and they have two children. Her family life seems enviable, but Jeong Hui-Ju feels like she spends her time meaninglessly. At that time, Jeong Hui-Ju meets a woman. The woman is poor, just like Jeong Hui-Ju in her younger days, but she still shines.