Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

nimevutiwa na speed ya hii drama katika kutuhadithia matukio ya kihistoria ambayo yamerekodiwa huko nyuma, ukijumlisha na mzuka wa kutokuangalia traditional epic sageuk kwa muda mrefu nimejikuta naitamani weekend ifike tena, hii ndio drama niliyoichagua kuiangalia katika safari yangu ya kumalizia mwaka (kuna drama nyingi nimezisamehe).

hadithi yake imeturudisha pale magenerali wawili (yi seong gye na jo min su) waliopewa amri ya kuanzisha vita dhidi ya Ming kwa lengo la kugomboa ardhi ya liaodong ambayo hapo zamani ilikuwa ni sehemu ya Goguryeo walipoamua kugoma na kurudi mji mkuu wa Gaegyeong.

kama umeangalia jung do jeon, the great seer na six flying dragons unajikuta unafanya mrejeo wa tukio hilo. Ila kwa kuwa jung do jeon drama ni traditional epic sageuk sina budi kuwapa credit kwa kutujuza kilichotokezea kwa ushahidi wa kihistoria tofauti na drama nyenginezo tajwa hapo juu.

fikiria episode 2 tu zimetupa matukio haya yafuatayo
  1. kushindwa vita kwa general choi yeong hatimaye kupewa adhabu ya uhaini: yeye ndiye alikuwa mstari wa mbele kumshawishi mfalme apeleke jeshi la kupambana na ming.
  2. kuondolewa madarakani kwa mfalme na hatimaye mwanawe mwenye miaka 9 kuirithi nafasi yake.
  3. general jo min su kutake power ya royal family.
  4. yi seong gye kumsambaratisha general jo min su (japokuwa tukio hili limeonyeshwa kwa sekunde chache)
  5. mfalme alioondolewa madarakani kutuma wauaji dhidi ya yi seong gye, tukio hili ndipo ilipoishia episode 2. Nafikiri hii itakuwa ni drama ya 4 kutuonyesha tukio hili (kwa aliyeangalia the great seer pia atakuwa analikumbuka hili tukio la mfalme kumpa mtumishi wake kisu)
what next huko mbeleni kabla hatujaingia kwenye upande haswa wa YI BANG WON
  1. Yi seong gye kuanguka na farasi
  2. kifo cha poeun
  3. kuanguka kwa goryeo
  4. kifo cha malikia
  5. mapinduzi ya yi bang won yaliopelekea kifo cha jung do jeon na wafuasi wake pamoja na watoto wa mke wa pili wa Yi seong gye.
ngoja tuweke oda ya ubuyu wa babu issa.
YI BANG WON alikuwa ni mtawala mwenye maarifa ya kutosha, lakini yote hayo hayaondowi ukatili wake usiomithilika
  1. aliwaua macomrade wake wengi aliopambanana nao pamoja kwenye mapinduzi ya kwanza na mapinduzi ya pili
  2. aliwaua ndugu zake
  3. aliwaua ndugu wa mke wake (Lady Min)
  4. alimuua baba mkwe wa mtoto wake (sejong)
  5. alimuua jung do jeon (sambong) na jeong meong jo (poeun)
  6. n.k yote hayo lengo kuu ni kuimarisha royal family.

View attachment 2047517
Bang won ni hatari na nusu[emoji2] nilimpenda sana kwenye six flying dragon na jang yangsil

Kwenye jang yangsil ndio alikuwa anakufa akijutia matendo yake na mwanae akatake over the throne

Akaruhusu tafiti za mwanasayansi wa kihistoria wa joseon jang yangsil zitumike.
 
Jioni ya Ijumaa nilishusha episode 7 za vicenzo drama (nimechoka kusifiwa) kupitia tovuti ya nkiri, usiku ulipoingia mwenyewe najikaza nataka kuziangalia.

episodes zote zinacheza sauti kama matangazo ya redio lakini video haionyeshi.
nilichafukwa kwa hasira zenye malalamiko ndani yake.
usawa huu wa kununua bando la GB 1 kwa shilingi 2000 hutakiwi kufanya makosa.
Hili swala hata mimi nimekutana kwenye pc sijui kwanini ila kwennye simu ziko poa picha unaona
 
Bang won ni hatari na nusu[emoji2] nilimpenda sana kwenye six flying dragon na jang yangsil

Kwenye jang yangsil ndio alikuwa anakufa akijutia matendo yake na mwanae akatake over the throne

Akaruhusu tafiti za mwanasayansi wa kihistoria wa joseon jang yangsil zitumike.
kwa mujibu wa drama ya the great king sejong, Yi bang won alimkabidhi madaraka mwanawe lakini bado akaendelea kushikilia masuala yote muhimu ya nchi mfano jeshi, kwa ufupi alimkabidhi mwanawe jumba tupu.
 
kwa mujibu wa drama ya the great king sejong, Yi bang won alimkabidhi madaraka mwanawe lakini bado akaendelea kushikilia masuala yote muhimu ya nchi mfano jeshi, kwa ufupi alimkabidhi mwanawe jumba tupu.
Hahahahaah ila bang won mtata sana[emoji2]
 
wakorea wana misimamo sana hadi raha ila kuna saa ni karaha wanatupunguzia uhondo
Mambo ya historical inaccuracy kuhusu historia zao enzi za Dictatorship tule miaka ya 1980's na kuingia kwa spies toka North Korea yaani mambo mengi viewers zaidi ya laki 2 wamesign petition ya kucancel drama.

Pia makampuni yaliyokuwa kwenye sponsorship yameanza kujitoa yaani uwezekano wa hii drama kuendelea ni 1% yanakuwa kama ya Joseon Exorcist
 
Wire Tun now iko moto
Screenshot_20211223-210511.jpg
 
Back
Top Bottom