Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Jamani jamani jamani ila wapemba kwa maneno hamna mpinzani umetafuta wee mpaka ukapata sababu ya kulalamika😂😂😂😂😂. Ilikua ugali mlenda ndo maana leo hujaona picha za madiko diko mitandaoni hali ngumuuuuu
mualiko umeletwa saa 8:30 mchana, hata hao mafukara kwa muda huo wameshajua kilichopikwa kwenye majiko yao. Nafikiria upya uamuzi wangu wa kutaka kuchumbia mwanamke wa kisukuma, si kwa uchoyo huu...
 
Copy and paste

arthadal chronicles season 2 inatarajiwa kuanza kushutiwa ila sasa cast wamebadilishwa kutoka song joong ki na kim jiwon hadi kuja wapya ambao ni lee joon gi wa kwenye moonlovers na shin sekyung..
 
Hahahha ile variety show yao
Jina lingine three meals a day
ni mzito sana wa kufuatilia hizo variety shows,
nikiwa na bando la kuharibu huwa napenda kuangalia variety show inayoitwa Home Alone (I live alone) inayoonyeshwa kupitia MBC, nafuatilia zaidi short clips zao zinazowekwa youtube na account ya kocowa tv (sijawahi kuangalia full episode) kwa sababu huwa wanazitafsiri.
==== >> is a reality show that portrays everyday lives of your favorite celebrities in the most intimate setting

nyota wengi wa korea hususani wale ambao hawajaingia kwenye ulimwengu wa ndoa wana maisha ya kawaida sana tofauti na vile tunavyowaona kwenye ulimwengu wa sanaa na wengi wao wanaishi kwenye apartments.

huwa navutiwa zaidi na design za nyumba zao.
 
Mambo ya kish..ga kwenye on going drama Military prosecutor ep10 yanakata sana stimu aisee, wakorea wanakwama aisee [emoji35][emoji35]
hata mimi nilidhani hivyo lakini imekuwa tofauti,
episode 11 na 12 yule kibonge alikanusha ya kwamba wanafanya pamoja mapenzi ya jinsia moja na yule mwanajeshi anayemtesa,

na alimwambia tae min nitakuja kukupa mkasa mzima wa kulala pamoja na yule jamaa mwanajeshi muonevu.
ngoja tuendelee kuangalia na kusubiria.

sijaangalia episode 13 na 14
 
Copy and paste

arthadal chronicles season 2 inatarajiwa kuanza kushutiwa ila sasa cast wamebadilishwa kutoka song joong ki na kim jiwon hadi kuja wapya ambao ni lee joon gi wa kwenye moonlovers na shin sekyung..
nimeona mashabiki wengi wanalalamikia uamuzi huo, tatizo kubwa ninaloliona ni kutokujitosheleza kwa taarifa yao kwani walipaswa kuelezea sababu ya msingi ya kutokuendelea kwa waigizaji wa mwanzoni.

halafu wakorea nao wana tabia ya kubebana na mara nyingi hutokezea kati ya muandishi au director dhidi ya muigizaji.

Itakuwa ni mara ya tatu kwa shin se kyung kufanya kazi na waandishi wawili wanaoshirikiana kazi zao ambao ni mwanamama Kim Young-Hyun na Park Sang-Yeon.
  1. six flying dragons
  2. tree with deep roots
  3. queen seondeok (hapa bado alikuwa ni mtoto mdogo)
je inatokezea kwa bahati mbaya?
ipo mifano mengi kama hiyo inayowahusu waigizaji wengineo
 
hii drama ndio muna mgomo nayo?
our blues drama
1650546629667.png
 
ni mzito sana wa kufuatilia hizo variety shows,
nikiwa na bando la kuharibu huwa napenda kuangalia variety show inayoitwa Home Alone (I live alone) inayoonyeshwa kupitia MBC, nafuatilia zaidi short clips zao zinazowekwa youtube na account ya kocowa tv (sijawahi kuangalia full episode) kwa sababu huwa wanazitafsiri.
==== >> is a reality show that portrays everyday lives of your favorite celebrities in the most intimate setting

nyota wengi wa korea hususani wale ambao hawajaingia kwenye ulimwengu wa ndoa wana maisha ya kawaida sana tofauti na vile tunavyowaona kwenye ulimwengu wa sanaa na wengi wao wanaishi kwenye apartments.

huwa navutiwa zaidi na design za nyumba zao.

Hizi ndo Zako unanipa ulevi alafu unakaa kuleee

Hata masked singer ulinitajia wewe sasa nimebakiza episode 30 kumaliza zote na wapo 350 huk0

Yani nlikua nashambulia kutokea chini na juu kote.
Ile fantastic duo nilitazama tatu tu.

Hospital playlist iliniacha na homa atleast baada ya ile variety nikakubali imeisha.

Sasa unanitajia home alone, alaf umemuweka nam goo min minafanyajee[emoji22]
 
Mimi naomba msaada wa namna y kuconvert episodes au movie nazodownload kutoka nkiri.com ziweze kuplay kweny TV pia
hizo video unatakiwa uzigeuze (convert) kutoka extension ya .TS kuelekea .MP4, kuyafanya hayo unahitajika kuwa na software ya VLC media player. Kuanzia leo tumia website ya (kimoitv.com) kupakua video kwa sababu video zao zote zipo kwenye format ya MP4. Nafikiri dvd na hata simu ndogo zinasupport kucheza video hizo. Pole sana
 
Huyu ni mr sunshine?
Ntaiangalia definetly
kuanzia leo tamka lee byung hun.umeshakuwa mtu mzima (legendary) kwenye huu ulimwengu wa hallyu stars. Unatakiwa uyajue majina yao kama unavyozijua nyimbo za diamond. Uzembe muachie Numbisa na wasukuma wenzake , kama huko kwao hawawezi kutamka neno urojo kwa usahihi wataweza kutamka majina ya wakorea, watakatika nyama za ulimi.
 
Back
Top Bottom