Kwa wasomi wa vyuo vikuu na elimu ya mazingira

Kwa wasomi wa vyuo vikuu na elimu ya mazingira

British economist

Senior Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
104
Reaction score
14
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif] MAZINGIRA:
CHANGAMOTO KWA VYUO VIKUU KUTOA KIPAUMBELE MAFUNZO YA MAZINGIRA, KUTUMIA MTAALA ENDELEVU
[/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]

"Asilimia 80 ya watu waishio vijijini wanategemea sana maliasili ya mazingira. Na maisha yao hutegemea zaidi hifadhi ya mazingira ili kutimiza lengo la Milenia ya kupunguza umaskini", alisema Blandina Cheche, Mratibu wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dar es Salaam, 22 Julai (IPS) - Hayo aliyasema hivi karibuni katika kongamano la wadau wa mazingira la kutengeneza mtaala katika vyuo vikuu vya uandishi wa habari, lililofanyika Mwanza chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kuratibiwa na Chuo Kikuu cha St. Augustine Tanzania. Wadau hao ni vyuo vikuu kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Iringa; idara mbalimbali za serikali zinazoshughulikia mazingira, wadau wa habari, vyombo vya habari na jamii lenye lengo la kupitia upya hali inayosababisha mapungufu ya mawasiliano katika masuala ya mazingira na kutafuta mbinu endelevu kupunguza mapungufu hayo. Kwa kiasi kikubwa mazingira hayatunzwi kama inavyostahili kutokana na mapungufu yaliyobainishwa kutokana na kutoelewa dhana ya mazingira na kukosa elimu ya kutosha ya kuhifadhi mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Miti inakatwa hovyo na kusababisha uharibifu mkubwa wa ardhi na mabadiliko ya hali ya hewa kwa ajili ya matumizi ya mkaa na kuni, hakuna mahusiano baina ya maendeleo endelevu, mazingira na mafuriko; afya na matumizi ya dawa. Yote haya yanahitaji mkakati wa unaoeleweka ili kuhakikisha kuwa taarifa sahihi zinatolewa, kueleweka na kuwapa uwezo watu kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na mazingira. Kwa mfano, ni jambo la kusikitisha pale unapoona kwamba jitihada za serikali za kukusanya uchafu kwa kutenga sehemu maalum zinakwama kutokana na uzembe wa kutoa tenda kwa makampuni binafsi yanayokusanya na kutupa uchafu huo katika madampo bila ubora wa magari yanayosomba taka ngumu na kuelewa mfumo husika unaolinda usafi wa miji na watu wake. Magari mengi hasa yale yanayosomba uchafu kuelekea dampo la halmashauri ya manispaa ya Ilala, eneo la Pugu Kinyamwezi huwa mabovu na mara nyingi huegeshwa katika sehemu hatari za barabara kwa muda mrefu bila kuhudumiwa wakati yakisubiri huduma ya matengenezo. Hata hivyo wakati mwingine magari hayo hulazimika kutupa takataka njiani bila kujali athari zinazoweza kutokea kama vile kuharibu mazingira na sura ya mji, harufu mbaya kwa wakazi wanaozunguka sehemu hiyo na pia magonjwa ya maambukizi yanayosababishwa na nzi wanaotua katika takataka hizo. Wakati mwingine utaona baadhi ya magari ambayo hayakufunikwa na nyavu ili kudhibiti usafi wa mazingira kwa kuzuia uchafu kuanguka au kumwagika barabarani. Kitu kingine cha ajabu ni pale unapoona katika matuta ya barabara kuelekea katika dampo, wanadandia mateja, na mara wanapokuwa juu ya uchafu wa magari hayo huanza kuchakura kama kuku anayetafuta chakula katika mchanga kwa lengo la kutafuta chuma chakavu kwa ajili ya kujipatia riziki. Matokeo yake huangusha viroba vinavyohifadhi uchafu uliokusanywa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa jamii, uharibifu wa mazingira na vile vile kunaweza kusababisha ajali iwapo kiroba hicho kinaweza kumwangukia mpita njia au gari lililoko karibu na gari lililobeba takataka. Kupata na kutoa habari kwa kupitia vyombo vya habari ni dhana muhimu katika jamii kwa kutumia mbinu mbalimbali za mawasiliano, kuieleza jamii masuala muhimu ya mazingira yanayowazunguka, kutafuta taarifa hizo kupitia mitandao mbalimbali na pia kuzungumza na watu kabla ya kuandika taarifa husika. Lakini vimekuwa vikiyafumbia macho matatizo hayo au kutoyafuatilia kwa undani ili kutoa ufafanuzi na ufumbuzi. Hayo na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa waandishi wa habari kuhusiana na suala la mazingira na hali ya hewa ni mapungufu makubwa yaliyojitokeza katika kongamano hilo. Kukosekana kwa elimu hiyo kunatokana na kutokuwepo kwa mtaala bayana katika vyuo vya mawasiliano na uandishi wa habari katika ngazi ya elimu ya juu na waalimu wataalamu katika fani hiyo. Mapungufu mengine ni waandishi wa habari kukosa ubunifu wa kuandika habari endelevu na ukosefu wa ari na hamasa ya wahariri kwa waandishi kutoa motisha ya kuandika habari za mazingira na badala yake hutoa kipaumbele katika masuala mengine hususan siasa, afya, masuala ya wanawake, uchumi na biashara. "Nina imani kwamba vyombo vya habari vina uwezo mkubwa wa kubadilisha mazingira kwa kutoa habari sahihi na endelevu kwa sababu vimefanya kazi kubwa katika masuala mbalimbali hususan kupambana na vita dhidi ya adui rushwa", anaendelea mratibu huyo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais. Kumekosekana pia uratibu wa pamoja katika ngazi mbalimbali baina ya serikali, wadau wa mazingira, vyombo vya habari na jamii kuhusiana na masuala ya mazingira, kukosa uwezo na kukosekana kwa mtaala maalum wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari na mawasiliano. "Ni muhimu kutathmini hali halisi ya ufundishaji masuala ya mazingira katika vyuo vyetu, kukusanya mrejesho kuhusiana na masuala ya mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa kutoka kwa wadau na kutambua maeneo ya ushirikiano yatakayofanikisha kuboresha hadhi ya ufundishaji masuala ya mazingira", alisema Mtaalam wa Mawasiliano kutoka ofisi ya UNESCO nchini Tanzania inayoratibu nchi nne katika Bahari ya Hindi. Vyuo Vikuu ni muhimu katika kuhimiza elimu hiyo kwa sababu ndivyo vinavyowatayarisha waandishi wa habari, vyombo vya habari ni mhimili wa nne wa taifa hivyo ni muhimu kuvijengea uwezo wa kuyafahamu masuala hayo katika ufundishaji. Ilifahamika kwamba ni Chuo Kikuu cha St. Augustine Tanzania ambacho pekee kinajitahidi kufundisha masuala ya mazingira. Wananchi wana haki ya kujua na kupata habari kwa kuelimishwa na vyombo vya habari vina uwezo mkubwa katika kutekeleza hilo kwa kubuni mbinu endelevu hususan kuandaa mtaala wa pamoja ambao ni shirikishi, kutabainisha mazingira halisi ya kufundishia katika vyuo mbalimbali vitakavyotoa elimu hiyo kwa waandishi wa habari ambao watakuwa tayari kujifunza kwa nadharia na vitendo. Wahariri nao wana mchango mkubwa katika kufanikisha hilo kwa kutoa motisha kwa waandishi wenye ari ya kuandika makala ya mazingira na kuyachapisha badala ya kuwatumia kwa kuandika masuala ya siasa, afya na uchumi. Waandishi wa habari pia wanatakiwa kuwa na ubunifu mkubwa katika kuandika makala ambazo zitahusisha mahusiano na athari ya mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa katika jamii kwa maendeleo ya taifa letu. Lakini jitihada hizo zinaweza kufanikiwa iwapo serikali itakuwa tayari kupokea mapendekezo ya mabadiliko yatakayowasilishwa kutoka kwa wadau, kwani uzoefu umeonyesha kwamba mazoea yamejijengea mfumo fulani katika ubadilishaji wa sera ya masuala mbalimbali jambo ambalo linasababisha uzoroteshaji katika kuchochea mabadiliko kutokana na woga, ukosefu wa ubunifu au umangimeza katika kutekeleza jambo ambalo lina manufaa katika jamii. Ni matumaini yangu kwamba mapendekezo yaliyotolewa na wadau wa kongamano hilo yatafanyiwa kazi kwa ufanisi ili kuhakikisha kwamba suala la mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa linapewa kipaumbele katika ngazi zote kuanzia bajeti, mitaala, ufundishaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini yake. (END/2010)
[/FONT]
 
Back
Top Bottom